Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Mkuu kabla hilo la kwanza halijafanyika utakuwa umepigwa kibao umepoteza fahamu. Halafu unaandikiwa ulitaka kuwapiga askari na kutoroka chini ya ulinzi! Si unajua utendaji wa vyombo vyetu?

Ni wajibu wetu kuwaelimisha watu na dola ili kuondoa hiyo hali. Kama sisi tusipofanya hivyo, hiyo tabia itaendelea vizazi na vizazi.
 
Raia unayo haki ya:-

*Kumwomba Askari ajitambulishe kwako.
-Muulize Jina lake.
-Muulize namba yake ya
Uaskari.

*Kujulishwa ni kwa nini unatiliwa mashaka au kukamatwa.

*Kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki ama sehemu unakofanyia kazi kwamba ama umekamatwa na Polisi au TAKUKURU.

*Kuomba na Kupewa dhamana wakati ukiwa Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.

*Hutakiwi kutoa Fedha kama Dhamana uwapo Kituo cha Polisi ama TAKUKURU, isipokuwa maelezo utakayoyatoa na kuandikwa Kituoni hapo.

*Kuwaeleza Polisi ama Maafisa wa TAKUKURU kwamba lolote utakalolisema linaweza kutumika kama ushahidi mahakamani na usiburuzwe wakati wa kuyatoa maelezo hayo.

*Kuomba wakili wako au mtu wa karibu yako utakayemchagua ili awepo Kituo cha Polisi ama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati unatoa maelezo yako.

*Haki ya kuyasoma maelezo yako kabla ya kutia sahihi katika maelezo hayo.

*Kudai risiti ya Orodha ya vitu vyako/fedha zako ulizotoa ama kukabidhi Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.

*Haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi Saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa Kituoni.

Haki za Raia Kupekuliwa

*Mtuhumiwa anayo haki ya kumpekua Polisi kabla ya yeye kupekuliwa na Polisi huyo.

*Raia kama ni Mwanamke, anayo haki ya kupekuliwa na Askari wa Kike, na iwapo Askari wa Kike hayupo, basi Mwanamke yeyote anaweza kumfanyia upekuzi, vile vile kwa Mwanaume.

*Askari hawana haki ya kuingia kwenye Gari, Nyumba au Ofisi ya Mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni y kufanya upekuzi bila kuwa na:
(a) Hati ya Upekuzi ambayo hutolewa Mahakamani.
(b) Mashahidi wanaotambulika rasmi Kisheria, kama vile Mwenyekiti/Mjumbe wa Serikali ya Mtaa au Kijiji husika.
(c) Jirani wa Mtu anayetuhumiwa.

Aidha, Mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na Askari Polisi baada ya Saa 12:30 Jioni au kabla ya Saa 12:30 Alfajiri, kwa mujibu wa makosa ya Jinai (Penal Code Act).

Isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua Mtuhumiwa kabla ya Saa 12:30 Alfajiri au baada ya Saa 12:30 Jioni kunaweza kuleta madhara kwa Askari Polisi, Mashahidi au Watu wengine wowote wale.
 
samahani mkuu hapa unaongelea polisi ya Chicago, New york, California, london uk, European union au unawaongelea kina kova?
 
vipi kuhusu upekuzi wa dharula.vipi kumkamata jambazi mwenye silaha .inakuaje kama utapata taarifa kuna vitu vya hatari ktk nyumba au gari kama mabomu ,bunduki nk
 
samahani mkuu hapa unaongelea polisi ya Chicago, New york, California, london uk, European union au unawaongelea kina kova?

Ha aha aa nadhani mwandishi anatamani jeshi letu liwe na sura hiyo..(future impossible tense)
 
Eti nini? Askari hana haki ya kuingia ktk gari? Lengo lako ni kuwachongea wananchi kwa polisi si bure.
 
ungefafanua mazingira ya ukamataji na upekuzi kutokana na mazingira mfano ya hatari na wahalifu sugu hata kama ni usiku.tambua kuna ambush inakuaje
 
Maaskari wengi wa cku hizi wanavuta sana bangi hata mabosi wao wanajua..kwa hiyo ukijifanya sana kujua hizo sheria utaishia kutwangwa hata risasi
 
kazi za polisi zinafuata sheria na kanuni vile vile mazingira ndio yanaongoza ukamataji na upekuzi.tambua kuna waizi wa kuku na waizi wenye kutumia bunduki na makosa madogo kama lugha ya matusi .huo ni mfano tu yapo mazingira mengi hatarishi na rafiki
 
mmmmmh uanze kumpekua polisi kabla hajakupekua kibongo bongo ukijaribu utajibeba
 
Mh hawa askari wa kibongo ngumu wanaweza hata kukusingizia case waonevu hata ukiwashtaki hawachukuliwi hatua na ukiwa mkorofi kujidai mjanja inakula kwako
 
Nanwanaoombwa mapenzi Mbona uwasaidii Nimeona live kawe darajani police anamkamata dadangu anajshia kuomba namba

Msg zilizofwata tu.samehe Ana familia kama zetu akijua niko nyuma ya tinted namchora tu
 
Labda takukuru wanaweza kukuelewa lakini vijana was Magu utaambulia kupigwa
 
polisi wa kibongo wakikudaka kwanza ni mkongongoto kifuatacho ndy unachukuliea maelezo...
 
Polisi watakufanyia hayo endapo hufahamu sheria, hujui nini wafanya, wakikutisha usitishike. Ukianza waambia kuhusu sheria wataogopa na kukutisha ila wao hawajui hizo sheria
 
Inawezekana sana,sema watu wengi huwa hawajiamini...
 
Polisi watakufanyia hayo endapo hufahamu sheria, hujui nini wafanya, wakikutisha usitishike. Ukianza waambia kuhusu sheria wataogopa na kukutisha ila wao hawajui hizo sheria

Hamna kitu ambacho Askari Polisi au TAKUKURU hajui katika hayo sema wanajitoa akili ila ndio kama unavyosema ukijiamini hata wao pia wanakuwa wapole wanaitaga "ma-bush lawyer"...
 
samahani mkuu hapa unaongelea polisi ya Chicago, New york, California, london uk, European union au unawaongelea kina kova?

mkuu Matola hii polisi wetu wasipoifata ukifika mahakamani inakuwa silaha yako tena...
 
Last edited by a moderator:
Hapo ukimuuliza jina tu na namba ya uaskari lazima akubambikie kosa....raia rinajifanya rijuaji

Hapo kwenye kusoma marlezo yako kabla ya kutia sahihi inaweza kuambatana na kipondo


Sheeeeeeda sana
 
Back
Top Bottom