Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

huyu mdau katutajia hizi haki ili wewe au mimi leo au kesho ukikamatwa na polisi jua namna ya kwenda nao sawa
 
asante kwa kutujuza ila sio kwa polisi wa Tanzania hawakuelewi wakikukamata wanakuoshea tu hata kama huna kosa.
 
Kuna exceptional...ndio maana kuna makosa ambayo hayahitaj search warrant....kama inaaminika mtuhumiwa hawez kukamatwa mchana...au n jambaz LA maana atakamatwa ucku

pia kosa la jambazi ni la moja kwa moja hapa mdau anazungumzia kwa watu ambao inawezekana wamefanya au hawajafanya kosa sasa polisi ndo wamekuja kukukamata ,usikikmbie wala usihofu ila jua haki zako kisheria juu ya kuwakabili
 
haki ipo kwa ajli ya kila mtu kwa sababu ni kitu cha asili tulichozaliwa nacho lakini wengi wetu uanumia kwa sababu hatuziju haki zetu,, ahsante sana mdau wa somo darasa lako zuriiiiii,,,"ukitaka uifurahie sheria ijue sheria"
 
Kwa hiyo asipekuliwe wala kukamatwa katika muda huo mpaka pale kutakapokuwa na ushahidi kwamba kutakuwa na madhara, tunatafuta madhara kwa nguvu, nani kaandika utumbo huu?[/QUOTE]

Soma CPA (Criminal Procedure Act) utamuelewa aliyeandika maana sheria ya nchi ndo isemavyo mwandish aliquote tuu
 
Kwa hiyo jizi likivamia usiku wa manane inabidi kisheria tusubiri kuche ndio tiulikimbize kulikamata na kulisachi?

Hapana hapa alichemka kidogo,dhumuni hasa sio kukamatwa baada ya 12:30 jioni bali ni kupekuliwa majumbani sio kukamatwa,hawaruhusu kupekuwa majumba muda tajwa hapo juu ila kukamatwa anakamatwa wakati wowote.
 
Hili la kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24, ni kwa siku zote za juma? mfano umekamatwa Ijumaa, saa 24 zitaangukia siku ya jumamosi...ambapo ofisi na mahakama huwa zimefungwa...na jumapili yake.

utajikuta umekaa mahabusu bila kufikishwa mahakamani kwa saa mpaka 48 au zaidi...je hapo haki itakuwa imetendeka? na ufanye nini ili haki itendeke?

NAULIZA
 
Haki zako za Kisheria unapokamatwa na Polisi

Raia unayo haki ya:-

*Kumwomba Askari ajitambulishe kwako.
-Muulize Jina lake.
-Muulize namba yake ya
Uaskari.

*Kujulishwa ni kwa nini unatiliwa mashaka au kukamatwa.

*Kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki ama sehemu unakofanyia kazi kwamba ama umekamatwa na Polisi au TAKUKURU.

*Kuomba na Kupewa dhamana wakati ukiwa Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.

*Hutakiwi kutoa Fedha kama Dhamana uwapo Kituo cha Polisi ama TAKUKURU, isipokuwa maelezo utakayoyatoa na kuandikwa Kituoni hapo.

*Kuwaeleza Polisi ama Maafisa wa TAKUKURU kwamba lolote utakalolisema linaweza kutumika kama ushahidi mahakamani na usiburuzwe wakati wa kuyatoa maelezo hayo.

*Kuomba wakili wako au mtu wa karibu yako utakayemchagua ili awepo Kituo cha Polisi ama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati unatoa maelezo yako.

*Haki ya kuyasoma maelezo yako kabla ya kutia sahihi katika maelezo hayo.

*Kudai risiti ya Orodha ya vitu vyako/fedha zako ulizotoa ama kukabidhi Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.

*Haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi Saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa Kituoni.

Haki za Raia Kupekuliwa

*Mtuhumiwa anayo haki ya kumpekua Polisi kabla ya yeye kupekuliwa na Polisi huyo.

*Raia kama ni Mwanamke, anayo haki ya kupekuliwa na Askari wa Kike, na iwapo Askari wa Kike hayupo, basi Mwanamke yeyote anaweza kumfanyia upekuzi, vile vile kwa Mwanaume.

*Askari hawana haki ya kuingia kwenye Gari, Nyumba au Ofisi ya Mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni y kufanya upekuzi bila kuwa na:
(a) Hati ya Upekuzi ambayo hutolewa Mahakamani.
(b) Mashahidi wanaotambulika rasmi Kisheria, kama vile Mwenyekiti/Mjumbe wa Serikali ya Mtaa au Kijiji husika.
(c) Jirani wa Mtu anayetuhumiwa.

Aidha, Mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na Askari Polisi baada ya Saa 12:30 Jioni au kabla ya Saa 12:30 Alfajiri, kwa mujibu wa makosa ya Jinai (Penal Code Act).

Isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua Mtuhumiwa kabla ya Saa 12:30 Alfajiri au baada ya Saa 12:30 Jioni kunaweza kuleta madhara kwa Askari Polisi, Mashahidi au Watu wengine wowote wale.

Share na marafiki zako!!!
 
Mkuu kabla hilo la kwanza halijafanyika utakuwa umepigwa kibao umepoteza fahamu. Halafu unaandikiwa ulitaka kuwapiga askari na kutoroka chini ya ulinzi! Si unajua utendaji wa vyombo vyetu?
 
Mkuu kabla hilo la kwanza halijafanyika utakuwa umepigwa kibao umepoteza fahamu. Halafu unaandikiwa ulitaka kuwapiga askari na kutoroka chini ya ulinzi! Si unajua utendaji wa vyombo vyetu?

Hivyo vyote hapo kwa tanzania ni ndoto ukitaka wakukimbie washushie english ya ukweli uone watakavyokanyagana.
 
Asante japokuwa kwenye nchi inayoendeshwa kwa amri za ''wapigwe tuu'' sidhani kama inasaidia badala ya kuchochea madhila zaidi!
 
Vipi huyu aliomba hivyo unavyodai awaulize kwanza Askari??

Polisi-piga.jpg
 
  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

Hapa kwenye picha huo usemi unaendana kweli na kwenye hapo kwenye RED???
3.JPG
 
tena ukujifanya unajua ndo unachezea kichapo hadi basi ivi askari mnawajua wanavo penda sifa kama yule alie leta uzi wa fast jet
 
Back
Top Bottom