Mr. Somebody
Member
- Sep 12, 2013
- 76
- 24
huyu mdau katutajia hizi haki ili wewe au mimi leo au kesho ukikamatwa na polisi jua namna ya kwenda nao sawa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna exceptional...ndio maana kuna makosa ambayo hayahitaj search warrant....kama inaaminika mtuhumiwa hawez kukamatwa mchana...au n jambaz LA maana atakamatwa ucku
Kwa hiyo jizi likivamia usiku wa manane inabidi kisheria tusubiri kuche ndio tiulikimbize kulikamata na kulisachi?
Mkuu kabla hilo la kwanza halijafanyika utakuwa umepigwa kibao umepoteza fahamu. Halafu unaandikiwa ulitaka kuwapiga askari na kutoroka chini ya ulinzi! Si unajua utendaji wa vyombo vyetu?
- Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
- Mwulize jina lake
- Mwulize namba yake ya uaskari
- Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
- Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
- Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
- Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
- Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
- Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
- Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
- Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.