Jua linaua kila mmea, halafu TMA wanasema kuna El Nino

Jua linaua kila mmea, halafu TMA wanasema kuna El Nino

Umeishia darasa la Ngapi?
Ukoo wenu wote mkijikusanya mkileta vyeti vyenu vya form iv mkijumlisha alama za masomo yenu mliyofaulu hampati hata Div III ,nimepiga A hadi masomo ambayo ni Optional ,siongelea kwa upande wa 6 na chuo maana huko ni mbali sana mtapoteana.

Ukiona jitu linashabikia SISIEMU basi tambua ni Zero brain.
 
Lakini Leo 22/10/2026 majira ya saa Nne; TMA wameweza kurudia Tahadhari yao na kusema: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesisitiza mvua kubwa za El Nino zipo na zitakuwa kubwa kuliko zilizotangulia.............. Soma uzi wa carbohydates uliopandishwa 10:04 am.
Unafikiri nimekataa? hoja ni hizo hela nusu trioni ilitengwa na zimeshaanza kutumika na si ajabu sehemu kubwa umeenda kwenye uhamasishaji badala ya kurekebisha mitalo na kununua vifaa vya uokozi
 
Unafikiri nimekataa? hoja ni hizo hela nusu trioni ilitengwa na zimeshaanza kutumika na si ajabu sehemu kubwa umeenda kwenye uhamasishaji badala ya kurekebisha mitalo na kununua vifaa vya uokozi
Kimbembe kitakuwa kwenye Utoaji wa TAARIFA ya Matumizi na Taarifa ya Mdhibiti wa Manunuzi(Procurement report). Wataoneshaje Physical manunuzi ya Urekebishaji wa mitaro? Hela itakuwa imepigwa sana.
 
Kwanza hao TMA Hawajui hata neno el nino maana yake nini

pimbi hawa waseme tu kutakuwa na mvua za hapa na pale!
 
Kuleni hizo 700+ billion na maisha yaendelee
Mkuu uwezekano wa mvua kutokana na joto ni kubwa sana.
1792744723623.png
 
Wanasema kesho ( tarehe 24)mvua itanyesha Mkoa wa Pwani.
Labda napaswa kwenda kutembea kidogo kabla ya house bound kesho.
 
SOUTH AFRICA WANASEMA KUTAJUWA NA UKAME USIO ELEZEKA.YANI ELININO YA JUA KALI SANA.

1. Mvua kuwa chini ya kiwango cha kawaida
Maeneo mengi ya Afrika Kusini yanatarajiwa kupata mvua chache kuliko kawaida.
Hali hii inatarajiwa kuonekana kuanzia Oktoba hadi Desemba 2026.
Hali ya ukavu inaweza kuendelea katika baadhi ya maeneo hadi mwanzoni mwa mwaka 2027.
South African Government +1

2. Joto kali kuliko kawaida
Joto linatarajiwa kuwa juu ya wastani katika maeneo mengi.
Mawimbi ya joto
(heatwaves) yanaweza kutokea mara nyingi zaidi.
Hali hii inaweza kuongeza mahitaji ya maji na umeme.
SAnews

3. Hatari ya ukame Mvua zikipungua kwa muda mrefu, nchi inaweza kukabiliwa na:
Upungufu wa maji katika baadhi ya maeneo.
Kupungua kwa unyevunyevu wa udongo.
Kupungua kwa uzalishaji wa mazao.
Changamoto kwa wafugaji kutokana na upungufu wa malisho na maji.
Hiyo hali ya ukame ambayo imetabiriwa na Mamlaka za South Africa iliwahi kutokea mwaka 2016 kama sikosei. Mji wa Cape Town ulikumbwa na uhaba mkubwa wa maji kiasi kwama ilibidi itungwe Sera ya Maji kuhusiana na mji huo tu. Yaani ulikuwa ukionekana unamwagilia maua shughuli unayo.
 
Huyo mwamba mTMA alitokea wapi na ilikuwa ni majira ya saa ngapi? Usikute aliyekuwa anamhoji alisahau kumwuliza: jua kali na tahadhari ya kuhama mabondeni kuna uhusiano gani?
au labda alitokea kule Kitambaa cheupe?

Yeah. Zile 780 B zitawatesa sana.
Usikute zishaliwa wanatafuta pakutokea TU,
 
Nakumbuka El Nino ya mwanzo 1998 mamlaka ya hali ya hewa ilitoa utabiri na angalizo kua mvua zitakua kubwa sana na watu wachukue tahadhari ikiwa ni pamoja na kuhama mabondeni

Watanzania kama kawaida yao wakapuuza, sababu tu kulitokea mabadiliko kidogo kwenye utabiri. Mvua zikachelewa na vipindi vya jua kali vikawa virefu kidogo kuliko ilivyo tabiriwa

Miongoni mwa waliopuuza utabiri ni pamoja na watumishi waandamizi wa serikali. Aliyekua Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakati huo alizungumzia kwa kejeli kuhusiana na kukosekana kwa mvua

Kina cha maji katika mabwawa ya Mtera na Kidato ambavyo vilikua ndio vyanzo vikuu vya kuzalisha umeme nchini kilikua kimepungua kwa kiasi ambacho hakikuwahi kushuhudiwa katika historia ya mabwawa hayo na kukawa na tishio la kukauka kabisa

Ndipo Kiongozi huyo mwanadamizi wa Wizara(kama kumbukumbu zangu ziko sahihi alikua Ekiakimu Maswi) akatoa kauli kua mgao wa umeme utaendelea maana mabwawa yanaelekea kukauka na hata mvua inyeshe miaka kumi mfululizo haziwezi tena kujaza mabwawa hayo

Bwana eeh, hazikupita hata siku kumi mvua zikaitika! Zilikua mvua kubwa sana za kupita kiasi, mvua za uharibufu na madhara, mvua za shari zilizogharimu maisha ya watu, mali zao kama mazao shambani na majumba na miundombinu mbalimbali ya serikali kama barabara, njia za umeme na simu nk. Zilikua Mvua za El Nino

Ndani ya siku chache mabwawa yote ya Kidatu na Mtera yakawa yanatapika! Kingo zake zikasalimu amri kwa maji na sasa yakaenea katika makazi ya watu na kuzidi kuleta maafa badala ya heri

Tusipuuze tahadhari za wataalamu. Ingawa kuna wakati mwingine kunaweza kua na mabadiliko kiasi fulani kwenye utabiri wa hali ya hewa
Kwani kuna mtu amebisha kwamba kutakuwa na mvua kubwa? , swali ni je, bilioni 700 zimefanya nini?
 
Back
Top Bottom