Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

Si mnayo TBS? Inafanya nini kama juisi zenu mbovu?

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
😀
Mtamkumbuka JPM
 
Kenya wana cement ya kutosha sana mkuu tena watakuletea na utainunua kwa bei ya tzs elfu 8 mpaka kumi. Kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa watakuwa wanufaika sana wa hili manake huko cement ya tz ni zaidi ya elfu 25, ili hali ya Kenya ukienda tu hapo Isibania unaipata kwa elfu 10, Imesababisha vita isiyoisha kati ya polisi na bodaboda wanaobeba hiyo cement toka Kenya kuja Sirari. Kwa TANZANIA hii acha iwe hivo manake maajabu hayaishi Mtwara cement ya Dangote inauzwa bei ghali kuliko DAR, Pwani, Morogoro na pengine hata Dodoma.
 
acha woga we ni mtoto wa kiume,na hizi point zako za history form 3,unajichoresha tu kwenye profile yako miwani mikuubwa lakini roho ya kike.
Maoni yangu, hiyo miwani Wala haina tatizo, nijibu kwa hoja hata Kama una akili kuliko Mimi.
 
JPM mwondoe. Hakuna mchango wake wa maana kwenye sekta ya viwanda.
Kwahio alipopandisha bei ya maziwa yanayotoka nje ili Tanga Fresh na wenzake wasukume gurudumu la maendeleo...kwako ilimaanisha nini
 
Tuongeze ubora katika bidhaa zetu la sivyo tutaachwa kwenye mataa. Mf. Wembe ni sh 200 na wa Kenya bei sawa pesa ya Tz, wa Tz ni butu wa Kenya una makali ya kutosha, sasa nichukuwe wa Tz au Kenya? Pamoja na uzalendo wangu nachukua wa Kenya.
 
Ajabu moja ya materials za kutengeneza cement hiyo(Coal) zinatokea Tanzania

Makaa yatoke mbinga yaende kisumu (Rai Cement ) kutengeneza cement , halafu cement hiyo inakuwa nafuu kuliko ya dangote ambayo makaa yanatoka km 700tu
Hehehehe hawa watunga sera wetu bana
 
Wataweza tu, utaogopa mpaka lini?
 
You have clue !
Hiyo vita isiyoisha kwa bodaboda na askari , nimeishuhudia pale sirari, !!
 
Nimeona mnasifia sana ubora wa bidhaa za Kenya na unafuu wake katika upande wa bei....vipi kuhusu KONYAGI? je wako vizuri pia katika ubora? na bei zao ni nzuri?View attachment 1805644
Ni moja ya products zinazotoka kwetu kwenda kenya na kubamba sana zikiwa huko
Japo kuna wakati ziliwahi kurudishwa na kebs pale namanga kwa kuwa quality ilikuwa mbaya. Kwa baadhi ya batches.
 
Suala la sukari nimecheka mpaka mbavu zimeuma, wenye mitaji zao akina nani sasa? We mwenye afya nzuri ya akili huna mtaji si ungefungua kiwanda cha sukari hapo kijijini kwenu. Hahahaha
 
Sikuwahi kulijua hili
Kuna kipind makaa ya mawe yalileta shida , wale wamiliki walikua wakitoa hoja zao na hasara wanayopata kwa kutozalisha, moja wapo ya hoja zao ni hiyo , watashindwa timiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…