Kuna jamaa kijijini kwetu enzi za ujana wake alicheza rafu sana kwa wasichana. Alikuwa ananiambia "nakwenda hadi mara 11". Wakati huo mimi nilikuwa haya mambo siyajui, ila nilikuwa nikimwambia "kama unafanya hivyo utaathirika baadaye, utakuwa utakuwa huwezi tena haya mambo." Sijaonana naye tangu wakati huo, lakini wanaokutana naye wanasema nywele zimebakia tu kwenye maskio, na hamjui mke tena. Amekuwa tu mtu wa mwaloni: mvuvi anayevua, piga maji ile mbaya na kulala huko huko na hana mpango na mke wala familia yake. Kwa maneno mengine, amekwisha!