Jukwaa la Wahariri ni sawa na Bunge au Mahakama?

Jukwaa la Wahariri ni sawa na Bunge au Mahakama?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kitendo cha Balile kulifananisha Jukwaa la Wahariri na Bunge au Mahakama linafikirisha sana. Yaani kweli Bunge tukufu ndio la kufananishwa na Jukwaa la Wahariri? Yaani kwa sababu bunge linapewa fedha na serikali za kujiendesha?

Kwamba kwa sababu bunge halina vyanzo vyake vya mapato basi nao Jukwaa la Wahariri wanaiomba Serikali iwabebe ili waweze kwenda Urusi na Marekani kujifunza?

Waandishi wa Habari ngachoka kabisa.

Nawasalimu kwa jina la JMT.
 
Kama Bunge lenyewe linajiendesha kwa namna ambayo wananchi wameona haikupaswa kuendeshwa kwa namna hiyo, si ajabu hata kidogo mwananchi au wananchi kuona vyama vya kitaaluma au vya kikazi vikiwa na uwezo wa kuchukua nafasi ya Bunge.

Bunge lijichunguze. Je mijadala yao na namna wanavyojiendesha linakidhi vigeo vya kuitwa mhimili wa serikali?

Nadhani Balile anahoja. Asikilizwe
 
Katiba yetu ndio inahitaji marekebisho.

Nchini Kenya mahakama inajitegemea kweli na walishatengua ushindi wa rais aliye madarakani kwamba sio wa haki.
Hapa Tanzania unategemea ingewezekana?

Bunge hili la ndugu-yai ungetegemea linge challenge serikali ya mwendazake?
 
Kwa Bunge la Ndugai bora hata kikao cha Viranja wa Kibasila sekondari kinaweza kujadili na kuamua la maana.
 
Tunachohitaji ni katiba mpya ambayo itamuweka kila mtu huru na si kutegemea hisani ya mtu fulani!
 
Back
Top Bottom