Julius adakwa akijifanya Afisa Muuguzi Mloganzila, atuhumiwa kwa wizi wa mali za wagonjwa na kukiri kuiba Simu Tatu

Julius adakwa akijifanya Afisa Muuguzi Mloganzila, atuhumiwa kwa wizi wa mali za wagonjwa na kukiri kuiba Simu Tatu

Wamchunguze vizuri kwasababu huwezi kuharibu kazi kwasababu ya wizi huko alikofukuzwa awali ni aibu tupu nursing iharibike kwasababu ya wizi wa simu??? Haiingii akilini
Kama mavazi anayo pia na vitambulisho 🤔 hii inatia ukakasi sana
 
nilikuwepo hapo usiku wa jana...saa 6 usiku jamaa katiwa nguvuni naamka naskia ndugu wa wagonjwa pale bandani wanapolalaga waachiwe walau kwa dkk 5 hivi wamtie adabu ndipo walinzi walipoenda kumuhifadhi chumba chao pale getini
Aisee tungempatia haki yake ya kikatiba 😃
 
Ni maajabu haya. Nimezoea kusikia Polisi bado wanafanya uchunguzi, na utakapokamilika umma utajulishwa.

Hapa uchunguzi au hitajiki?
 
Ccm ni wapumbavu sana

Siwapendi CCm ila kwenye hili hawahusiki, Watazingua mno kama jamaa hatalipa hizo simu za wagonjwa na atafikishwa mahakamani, Hapo CCm itakuwa inalea hao watu.
 
Siwapendi CCm ila kwenye hili hawahusiki, Watazingua mno kama jamaa hatalipa hizo simu za wagonjwa na atafikishwa mahakamani, Hapo CCm itakuwa inalea hao watu.
Ccm ni wapumbava sana ndiyo wamesababisha hata wewe usijue wanausika vipi ...hivyo hata wewe kutokujua kuhusika kwa ccm ni matokeo ya upumbavu wa ccm pia
 
Jamaa apelekwe jela.moja kwa moja kufungwa bila kupelekwa mahakamani
 
Aidha uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili inapenda kuihakikishia jamii kuwa inayo mifumo imara ya kiusalama ya kuweza kubaini watu wote wanaoingia na kutoka hospitalini na ndio maana imeweza kumfuatilia mtuhumiwa huyu na kumkamata.
Politics!!
Aliwezaje kufanya kazi humo msimjue muda wote huo? Bora mngenyamaza kuficha aibu
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imemkamata Bw. Steven K. Julius kwa tuhuma za wizi wa mali za wa wagonjwa ikiwemo simu za wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kwa kujifanya ni mwajiriwa wa Muhimbili Mloganzila kwa cheo cha Afisa Muuguzi.
View attachment 3187027
Baada ya mahojiano Bw. Julius amekiri kuiba simu tatu ambapo mbili aliziuza kwa mkazi wa Kibamba na moja ameiuza kwa mtu anyeishi nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Bw. Julius baada ya kumaliza mafunzo kwa vitendo ya uuguzi (nursing internship) amefanya kazi katika hospitali kadhaa za mkoa wa Dar es Salaam ambapo alifukuzwa kutokana na vitendo vya kukiuka maadili ikiwemo wizi.

Mtuhumiwa amefikishwa Kituo cha Polisi Gogoni kilichopo Kibamba kwa taratibu za kisheria.

Aidha uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili inapenda kuihakikishia jamii kuwa inayo mifumo imara ya kiusalama ya kuweza kubaini watu wote wanaoingia na kutoka hospitalini na ndio maana imeweza kumfuatilia mtuhumiwa huyu na kumkamata.
Wakristo ni wezi sana
 
Politics!!
Aliwezaje kufanya kazi humo msimjue muda wote huo? Bora mngenyamaza kuficha aibu
20241229_085615.jpg
 
Back
Top Bottom