KERO Julius Nyerere International Airport (JNIA) kukosa air condition ni aibu kubwa kwa nchi hii

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni zaidi ya wiki sasa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport air condition hazifanyi kazi, hasa kipindi hiki cha joto kali Dar es Salaam, hivi wahusika wanafikiria nini? Je, ni hujuma?

Mama Kizimkazi anajua? Na kama anajua amechukua hatua gani? Na kama hajui kwa nini hajui? Alafu tuna ndoto za kupata watalii zaidi, utawapata wapi wakati wakija tu Dar hali ni mbaya kila eneo mpaka airport, ule uwanja kwa sasa umekuwa ni jehanam, kuna baadhi ya watalii walipoingia tu Dar kesho yake wakageuza kurudi, mana walipofika hali ni mbaya, joto kali airport mpaka mtaani.

Nauliza swali, je, hii hali itaisha lini mana hakuna anayejali kabisa, na watanzania kama kawaida yao wamekaa kimya.
Ukichilia mbali ukosefu wa AC, mvua zikinyesha pale termina 2 huwa panavuja sana.
 
Kutokuwa na air condition uwanja huo haujaanza leo yaani kila kitu ni hovyo tu
1995 nilishuka hapo kulikuwa na joto balaa na a/c hakuna kabisa ingawa unaona makasha tu tena mapya
Lakini nchi za kiafrika ndio tulivyo uhujumu mwingi kila sekta
Nenda Nigeria unapishana na mende na panya airport na hawajali mnasalimiana tu
 
Nipe majina yako matatu kama yanavyoonekana kwenye kitambulisho cha NIDA ili tufuatilie
majina yake matatu yanahusiana nini na kufuatilia uzembe na ukiazi unaoendelea airport pale..... au unajifariji ki ndezi hapo sebule i mwa shemeji yako?
 
TANESCO wanachezea KOKI mwi mwa mara wamezima mara wamewasha mara wamezima wamewasha wamezima tena wamewasha, sasa najiuliza jamaa anasikia raha au kitu gani?
 
Ni zaidi ya wiki sasa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport air condition hazifanyi kazi, hasa kipindi hiki cha joto kali Dar es Salaam, hivi wahusika wanafikiria nini? Je, ni hujuma?

Mama Kizimkazi anajua? Na kama anajua amechukua hatua gani? Na kama hajui kwa nini hajui? Alafu tuna ndoto za kupata watalii zaidi, utawapata wapi wakati wakija tu Dar hali ni mbaya kila eneo mpaka airport, ule uwanja kwa sasa umekuwa ni jehanam, kuna baadhi ya watalii walipoingia tu Dar kesho yake wakageuza kurudi, mana walipofika hali ni mbaya, joto kali airport mpaka mtaani.

Nauliza swali, je, hii hali itaisha lini mana hakuna anayejali kabisa, na watanzania kama kawaida yao wamekaa kimya.
Ulipita terminal ipi ndugu? Mie nimepita terminal 2 mwezi huu naona zilikuwa zinafanya kazi kama kawaida. Hata wakati naondoka zilikuwa zinaofanya kazi kama kawaida!
 
Back
Top Bottom