3
Baada ya vita baridi kuisha mwanzoni mwa miaka ya 1990 ,. Nchi ya marekani na ulaya hawakuweka kipaumbele sana kwa maswala ya itikadi Kali kama kitisho kingine Cha ugaidi. Kwa mfano uingereza haikuipa kipaumbele mashariki ya kati kama sehemu ambayo sumu za ugaidi zilikuwa zinapikwa , badala yake serikali ya nchi hiyo ilijikita zaidi na maswala ya ugaidi huko Ireland kaskazini ambapo kulikuwa na kundi la kigaidi lililotaka kujitenga kwa Ireland kaskazini kutoka uingereza.
Mkurugenzi mkuu mstaafu wa shirika la kijasusi aliyefanya kazi kuanzia 1993 Hadi 1995 alisema kwamba mashirika ya kijasusi ya nchi za marekani na uingereza yalifanya makosa sawa katika kutochunguza athari za itikadi za madhehebu ya kiislamu ambayo yalikuwa yanahubiri itikadi Kali ambayo yangekuja kuzalisha ugaidi. Mashirika haya yalijikita katika kuangalia ukomunisti tu peke yake .
Na la zaidi ni kwamba uingereza ilidai Haina maslahi yoyote kwenye nchi za mashariki ya kati, hivyo isingeweza kuingilia maswala ya makundi ya kidini kwenye nchi hizo. Lakini nchi kama ufaransa wenyewe walikuwa tayari wameshaonja ladha ya ugaidi na walikuwa wanapigana vita hivyo vya ugaidi huko Algeria.
Kwa mfano shirika la kijasusi la uingereza la M15 mwaka 1994 waliamua kuvunja idara ndogo ya G7 iliyokuwa ikijikita zaidi kukusanya taarifa za Siri na ku monitor ugaidi wa kidini. Na hata baadaye idara hii iliporudishwa Tena mwaka 1996 , bado haikuwa na nguvu ya kukusanya taarifa hizo za hayo makundi ya itikadi Kali kutokana na kukosa base line ya kuanza kuchunguza mafundisho Yao na vilevile kukosa mashushushu watakaojipenyeza kwenye makundi haya kukusanya taarifa. Watu mbalimbali walianza kuionya uingereza na haya makundi yaliyokuwa yanashika Kasi nchini humo lakini kama kawaida wanasiasa hawakutaka kusikiliza.
Kwa mfano aliyekuwa mkuu wa kitengo Cha counter-intelligence ndani ya FBI kuanzia 1980 Hadi 1991 na baadaye akawa mkuu wa FBI huko Texas bwana Oliver revell , Alikiri wazi kwamba marekani walijua Kuna makundi ya kidini yenye msimamo mkali na yanakuwa kwa Kasi nchini uingereza , lakini wanasiasa kama kawaida hawakutaka kujishughulisha na hili . Hii ni kutokana na ukweli kwamba uingereza haikutaka kujiingiza kufanya upelelezi wa makundi haya ambayo yalikuwa yakisemekana Yana mfungamano na ugaidi labda kungekuwa na udhibitisho au ushahidi wa Moja kwa Moja.
Chanzo kingine pia kilisema kwamba inner circle za mashirika ya kijasusi nchini uingereza waligawanyika kutokana na hili swala. Wengine wakiamini kwamba kuingilia maswala ya kidini kungeleta athari kwa maslahi ya uingereza maeneo mbalimbali duniani na la zaidi uingereza ingeonekana siyo nchi inayoheshimu demokrasia na uhuru wa watu kuabudu.
Na hata aliyekuwa kiongozi wa kidini wa Anglican wa Canterbury lord Carey alilipa uzito hili swala la makundi ya kijihadi yaliyokuwa yanakuwa kwa Kasi sana kiasi kwamba akawatahadharisha wanasiasa wakubwa kama thatcher na pia John major kipindi wakiwa P.M lakini bado wakakaza na kusema Hilo haliwahusu Moja kwa Moja kutokana na ukweli kwamba wao wangeonekana kama wanaingilia uhuru wa dini za watu[emoji848].
Kwa mtu ambaye angekuwa ni mdadisi zaidi ni kwamba haya makundi ya kiislamu ya itikadi Kali yaliachwa yakuwe kwa kasi ,huku yakikingwa na wanasiasa wenyewe pasipo kujua wanafuga joka. Na hata Mohammed bakri wakati Fulani Alikiri waziwazi na kusema kwamba wao kama makundi ya itikadi Kali wasingeweza kuishambulia uingereza kigaidi kutokana na ukweli kwamba uingereza iliwapa hifadhi ya kisiasa/asylum na social benefits za hapa na pale . Lakini baada ya uingereza na mshirika wake marekani kuanza kujiingiza kwenye vita vya Afghanistan ,msimamo wa makundi haya ulibadilika Sasa uingereza ikawa ni next target ya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa Hawa wenye itikadi Kali, Makundi haya yakiamini kwamba uingereza ni adui wa imani ya kiislamu.
Hata serikali ya Algeria kupitia waziri wake wa mambo ya nje ,kwa wakati fulani walijaribu kuionya uingereza kwa kutopokea raia wa Algeria waliofukuzwa nchi hiyo kwa tuhuma za ugaidi, lakini kwa dharau uingereza ikajibu kwa kusema hao ni FREEDOM FIGHTERS . Hivyo watapewa hifadhi za kisiasa na benefits nyinginezo kama wakimbizi. What a mistake.Wachambuzi wanadai kwamba , uingereza na marekani kutokana na kuwa ni nchi za kidemokrasia na zenye ushawishi , lakini hazikuwa na mamlaka ya Moja kwa Moja kuchunguza vikundi vya dini za watu , labda tu kuwe kumetokea serious crime. Hii ndio ilikuwa chanzo kikubwa Cha kwanini nchi kama uingereza ilikuwa ikijivuta kufanya uchunguzi wa kina kwa Haya makundi ya kidini yenye itikadi Kali.
Na mzizi mkubwa wa kwanini hizi nchi hazikutaka kuingilia mambo ya kidini unaanzia mbali sana.
Wakati wa zamani ambapo nchi za ulaya zinaingia kwenye mgogoro wa kidini , vita vingi vilipiganwa na umwagaji mkubwa wa damu , ikapelekea mgawanyiko wa madhehebu enzi zile za vikings na Jesuits. Na ndio maana Hadi Sasa huko ulaya Kuna nchi ya Anglican church, Roman ,protestant na madhehebu mengine madogomadogo. Kutokana na hili uingereza ikaona si vyema kujiingiza kwenye migogoro ya kidini tena. Shida ndipo ilipoanzia hapa na uingereza ikashindwa kupambana na hizi religious fanaticism zilizokuwa zinakuwa upya kwa Kasi . Kwa sababu uingereza waliamini kupigana vita ya kidini ,ni Moja ya vita Moja ngumu sana kwakuwa unapigana na human beliefs ambazo zipo attached na nafsi Yake.. ni ngumu kuishinda vita ya namna hii. Na mbaya zaidi vyombo vya usalama hususan polisi hawakuwahi kufahamu jinsi haya makundi yanavyofanya kazi zao za kigaidi kisaikolojia. Kwa mfano wakati Fulani polisi walijichanganya wenyewe baada ya kumpiga risasi raia wa Brazili wakimdhania ni member wa kundi la kigaidi. Hali hii ilipelekea umma ku discuss competency ya polisi wa uingereza katika ku deal na ugaidi . Na ukiachana na hili ni kwamba tayari vyombo vya usalama vya nchi hiyo ikiwemo polisi ,tayari walikuwa wameathirika na kitu kinaitwa VICTIM CULTURE . Hii Ina maana kwamba makundi ya watu ambao ni minority kwenye jamii ya waingereza majority walikuwa mara nyingi wanaonewa na maaskari. Kwa mfano unakuta watu weusi mara nyingi kukamatwa na kuhusishwa na uhalifu. Hali hii ikapelekea mindset kwenye jamii kwamba polisi wanalenga makundi ya watu fulani Fulani tu peke Yake kwenye jamii na sio jamii ya wazungu. Hali hii ikawapa makundi ya kijihadi mwanya wa kufanya harakati zao. Na endapo polisi wanafuatilia harakati zao ,basi Moja kwa Moja wangepaza sauti zao kwamba wanaonewa na polisi kutokana na uchache wao ndani ya jamii.Hivyo polisi nchini uingereza wakawa wanasita katika kuchunguza au kufuatilia nyendo za makundi ya kijihadi.
Tatizo hili pia likatengeneza pia mgongano mwingine baina ya minority British Muslims na majority ya raia wengine. Ni kwamba mji wa Dewsbury ni miongoni mwa miji midogo ndani ya Yorkshire . Ni Moja kati ya miji ambayo ilikuwa Ina viwanda vingi vya nguo na wengi wa wakazi wake ni raia wa kigeni jamii ya Asia ambao wengi ni waislamu. Lakini mwaka 1987 ilitokea kisa kimoja kwenye mji huu ambapo wazazi wa wanafunzi kama 26 hawakutaka kuwapeleka watoto wao kwenye public school ambazo watoto wa kiislamu walikuwa wengi zaidi ya wakristo. Uchunguzi huu ilifanyika na ikabainikia kwamba wazazi Hawa walitaka watoto wao wakulie kwenye maadili ya kingereza Kwa maana walisema shule hizo zilikuwa Zina upendeleo kwa wanafunzi wa kiislamu ukilinganisha na wakikristo . Na wakaenda mbali na kusema shule hizi zilikuwa zinakiuka sera ya elimu ya uingereza ,ambayo ilitaka shule iwe ni multifaith na cultural diversity. Na hata maafisa wa serikali ya mtaa walipoulizwa kuhusiana na haya malalamiko ,wakakana . Ilikuja pia kubainika kwamba wanafunzi waliokuwa wa imani ya kikristo kwenye shule hizo walikuwa wakidhihakiwa na wenzao kutokana na mtindo wao wa ibada wa kusali. Lakini miaka 18 baadaye, ilikuja kubainika ndio mji aliokulia bwana Mohammed sidique Khan Ring leader ambaye alihusika na ulipuaji wa mabomu jijini London July 7 , 2005.Pia msikiti uliopo mji wa Dewsbury wa Jamaat tablighi ulikuwa ukihusishwa na mafunzo ya kidini yenye itikadi Kali. Pia ilbainika na waandishi wa habari kwamba Mufti Zubair Dudha wa msikiti huo ambaye alikuwa akifundisha vijana na watoto kwenye akademi ya Tarbiya madhara ya ugaidi na itikadi Kali , pia alihusishwa na ku support mashambulio dhidi ya nchi za magharibi kwa kile alichodai kwamba nchi za magharibi ni "the enemies of Allah". Tokea hapo jamii ya uingereza ilibadilisha mtazamo kuhusiana na Hawa wenzao katika maswala mazima ya kujamiiana. Ikawa imeonekana kwamba minority British Muslims wakawa wanapewa kipaumbele dhidi ya majority ya wenyeji. Hii ilitengeneza kitu wanakiita multicultural paralysis. Hii ni baada ya sera ya kudhibiti wahamiaji kufeli kwa kiasi kikubwa.
Kwa ripoti za kidemografia tokea mwaka 2001 za nchini uingereza zilikuwa zikibadilika kwa kiasi kikubwa. Ripoti hii ilionyesha kwamba raia wa uingereza ambao walikuwa wakihamia nchi nyingine ilibadilika kutoka idadi ya 50,000 Hadi 120,000 kwa Mwaka. Hii ilitokana wahamiaji wa nchi za Asia kuingia kwa wingi nchini humo pasipo udhibiti wa serikali. Na baada ya hapo ripoti ikaonyesha kwamba raia wa kigeni hususan wa jamii za Asia waliokuwa wakiingia uingereza ilifikia 200,000 kwa mwaka , mara nne zaidi ya idadi ilivyokuwa kati ya mwaka 1985 na 1995. Hali hii ilipelekea profile ya population structure ya uingereza kubadilika kwa kiasi kikubwa na kupelekea mgongano wa kiutamaduni baina ya wahamiaji na wenyeji na hali hii ikapelekea kukua kwa makundi ya itikadi Kali. Continued