July 7,2005

July 7,2005

Kuua mtu asiye na hatia ni kosa!! Kwahiyo mwenye hatia ni sawa kuuwawa? Na huyu mtu mwenye hatia ni mtu wa aina gani?
Vizuri, mfano, mtu aliye kuja kuiba nyumbani kwako Tena na silaha akiwa anataka kukudhuru, ruksa kumuua, mtu anataka kuanza kukudhuru(kukuua) ruksa kumaliza.

Vibaya kuanza wewe, mtu kajikalia zake, hana hili wala lile na wewe unapiga bisu, au kujilipua kufa nae ni kosa. Mmebishana, ama mmetofautiana mitazamo, ubishi wa vitu tofauti ndio umuue, ni kosa
 
2


Ukiachana na huyu Mohammed atta ambaye alikuwa na connection na Jiji la London ,list bado ni ndefu. Mfano mwingine Kuna Rashid al-Ghannushi ambaye alikuwa ni kiongozi wa Muslim brotherhood huko Tunisia alikuwa akiishi huko London kwa karibu miaka 15 baada ya kukimbia nchi yake kwa kushtakiwa katika kulipua uwanja wa ndege nchini mwake. Pia Kuna aliyekuwa akiitwa Abu Doha raia wa Algeria ambaye inasemekana alikuwa mtu wa karibu kabisa na Osama bin laden aliyekuwa akiishi London na alikuwa kwenye jopo kazi la magaidi waliopanga kulipua uwanja wa ndege wa Los Angeles huko marekani. Na pia raia mwingine wa misri aliyeitwa Yasser al-Siri aliyekuwa pia akiishi London alikuwa na connection na mtandao wa magaidi jijini hapo, na alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi , ikiwemo kupanga mauaji ya wazir mkuu msaidizi wa misri wakati huo na baada ya kufeli kutekeleza huu mpango aliamua kuua mtoto mdogo.
Lakini kwa majibu wa ripoti za wachambuzi , inasemekana harakati za Hawa watu wakiwa jijini London zilikuwa hazijawahi mulikwa na vyombo vya usalama kwa namna yoyote ile ,Hali iliyopelekea haya makundi ya kigaidi kumea .Hii ilipelekea wasomi na wachambuzi kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Ikumbukwe kwamba mwaka mmoja baada ya shambulio la kigaidi la September 11 huko marekani, kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba lile tukio lilifurahiwa sana na baadhi ya viongozi na wanazuoni wa kiislamu waliokuwa huko London. Hili lilidhihirika baada ya kipeperushi kilichokuwa kina picha ya majengo pacha yaliyolipuliwa kusambazwa mtaaani na kundi la waislamu la Al muhajiroun kama kuunga mkono na kulifurahia tukio Hilo likiwa Lina maandishi yanayosomeka "September 2001, a Towering Day in World History," . Lakini hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa na serikali ya uingereza.

Kwa mfano baada ya Iraqi kuivamia Kuwait kijeshi mwaka 1991, Nchi nyingi za magharibi ziliamua kupambana na uvamizi huu wa Iraqi kwenye nchi hii ya Kuwait . Hali hii ikapelekea chuki kwa baadhi ya viongozi wa kiislamu waliokuwa wakiishi uingereza . Aliyekuwa kiongozi wa kundi la Hizb ut-Tahrir bwana Omar bakri Mohammed raia wa syria alitamka hadharani waziwazi kwamba endapo ingepatikana nafasi ya kuuawa kwa waziri mkuu wa uingereza kipindi hicho John major ,basi asingesita kufanya hivyo. Kwa kauli yake hii hakuchukuliwa hatua zozote kwa kuhamasisha mauaji .
Gazeti la times la uingereza likaamua kufanya uchunguzi wa kimya kimya dhidi ya huyu bwana bakri, inakuwaje anahamasisha mauaji kama njia ya kuulinda uislamu . Uchunguzi ulibainisha kwamba huyu bwana alikuwa akipokea Hela za serikali ya uingereza za social welfare benefits kama euro 300 kwa ajili ya kujikimu yeye pamoja na mke na watoto kama 7 hivi. Aliulizwa inakuwaje Sasa anapokea fedha za serikali ambayo kwake yeye alikuwa akiamini ni ya kikafiri ,haifuati sheria za kiislamu. Jamaa alijibu kwamba yeye hawezi kupata kazi na viongozi wa kiislamu ambao wapo kwenye harakati za kuutetea uislamu Allah huwawezesha kuishi kwa neema zake [emoji848]. Huyu bakri aliwekwa kwenye mabano Ili waweze kuchunguza harakati zake pamoja na mafundisho aliyokuwa akiwapa wafuasi wake .
Tukiachana na harakati za Hawa jamaa waliotajwa kujihusisha na harakati za kigaidi , Kuna sehemu pia kulianza kumulikwa kimya kimya na ma undercover .
Sehemu hii ni msikiti mkuu wa kiislamu ulioko kaskazini mwa Jiji la London uliokuwa maeneo ya Finsbury Park, ikisemekana msikiti huu ndio ulikuwa kama kambi ya mafunzo ya jihad. Historia ya msikiti huu kuwepo ilitokana na mwanamfalme wa Wales aliyemshawishi mfalme Fahd wa Saudi Arabia wakati huo kujenga msikiti huo kwa ajili ya jamii ya kiislamu ya watu wa Bangladesh waliokuwa kwa wingi maeneo ya London kaskazini. Na kweli huyu mfalme wa Saudi Arabia alichangia kiasi Cha euro milioni Moja na laki Tatu msikiti huu ujengwe . Lakini huu mradi ulikuja kuingiliwa na viongozi wa makundi ya kiislamu ya itikadi Kali .Japo kulitokea vurugu lakini mwisho wa siku msikiti ukaangukia mikononi mwa makundi haya ya itikadi Kali. Na katika msikiti huu, bwana Abu hamza alipewa nafasi ya kuhubiri. Huyu bwana hamza alikuwa ni mhandisi aliyewahi pigana vita ya Afghanistan akapoteza jicho Moja na mkono. Na vilevile aliwahi kuwa baunsa kwenye klabu za usiku.
Mwaka 2002 ripoti za maswala ya ugaidi za marekani zilimworodhesha kwenye kundi la magaidi akihisiwa kuwa ni mwanamama wa kundi la Islamic army of Aden ambalo lilihusika katika katika kulipua manowari ya jeshi la marekani USS Cole kwenye fukwe za Yemen. Na pia huyu Abu hamza alikuwa akihisiwa kuwa anaushirika na serikali ya Taliban wakati huo. Huyu bwana aliwahi kunukuliwa na gazeti la Italia la la republica akikiri kwamba alitamani rais bush na viongozi wengine wa G8 wauliwe kwa njia ambayo ingehusisha kulipua ndege ambazo wangekuwa wamepanda. Kutokana na kauli yake hii ,ripoti za kwenye gazeti Hilo lilihitimisha kwamba huenda makundi mengi ya kiislamu ya itikadi Kali yalikuwa yamepania kwa 100%katika kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya nchi za magharibi.
Mwaka 1998 Yalifanyika majaribio kadhaa ya kumuondoa huyu bwana kwenye msikiti huo ikiwemo kumuwekea zuio la mahakama la yeye kutohubiri kwenye msikiti huo ila ikashindikana. Hili zuio lilikuja baada ya Baadhi ya waumini walianza kushtushwa na kupata wasiwasi baada ya kuanza kuona makundi ya vijana wakibaki msikitini hapo Hadi usiku wa maanane walifundishwa vitu visivyoeleweka. Miongoni mwao walikuwa ni Richard reid ambaye baadaye ndiye aliyekutwa na bomu la kujitoa mhanga kwenye kiatu akipanga kulipua ndege. Mwingine alikuwa ni raia wa Tunisia ,nizar trebelsi na Zacarias Moussaoui. Mwingine aliyekuwa akihusishwa kubaki Hadi usiku mrefu msikitini hapo ni Anas al-Liby ambaye alikuwa kwenye list ya FBI ya most wanted baada ya upekuzi kufanyika kwenye nyumba yake jijini Manchester na ikakutwa manual book ya Al Qaeda 1998.
Mwaka 2003 , mamlaka za uingereza zilianza kufanya uchunguzi wa kina kwenye msikiti huo pamoja na mhubiri wake Abu hamza. Zaidi ya askari 150 walivamia msikiti huo kwa ajili ya kupekua huku wakiepuka kukanyaga sehemu ya Ibada. Mamlaka za uingereza zilikuwa zimefikia hatua za kumnyang'anya uraia wake na vilevile kumpiga ban kuhubiri msikitini hapo. Kutokana na uchunguzi wa tuhuma dhidi yake kuendelea, huyu bwana aliendelea kuswalisha nje ya msikiti huo. Kutokana na shinikizo la marekani Baada ya miaka Saba alifunguliwa mashtaka ya ugaidi. Siku ya kushtakiwa, wafuasi wake walikuwa wamejazana kusikiliza kesi yake.... Lakini hili swala la Abu hamza likatengeneza tatizo jingine. Uingereza iliamua kupitia Baraza la wadhamini la kiislamu kuchagua uongozi mpya wa msikiti huo. Miongoni mwa waliokuwa kwenye Baraza hili alikuwepo Mohammed Kassem Sawalha. Huyu alikuwa ni rais wa Muslim association of Britain. Bwana huyu alikuwa anatuhumiwa kujihusisha na harakati za itikadi Kali za kundi la Hamas. Yote haya yalileta mgawanyiko miongoni mwa jamii za watu nchini uingereza huku mamlaka za nchi hiyo zikiwa zinajivuta kupambana na makundi ya kigaidi.
Mbaya zaidi ni kutokana na mfumo wa uhamiaji wa uingereza ndio kwa kiasi kikubwa ilichangia kwa makundi haya kujipenyeza Hadi nchini humo. Kwa mfano wahamiaji Hawa walikuwa hawakutani na masharti mengi ya uhamiaji kama vile kuulizwa visa ,au karatasi za uhamiaji pamoja na taratibu zingine. Hivyo newcomers wakapata mwanya huku wakikaribishwa na social welfare benefits. Ni wachache sana waliokuwa na legal documents za kuweza kubaki uingereza lakini wengine wengi walijichanganya katikati ya Raia wa uingereza pasipo kufuatiliwa. Kwa mfano mtaalamu na mchambuzi wa maswala ya kigaidi aliyejulikana kama Robert leiken aliwahi kusema kwamba Al Qaeda walikuwa wanatumia njia ya uhamiaji katika kujipanga na kupanga harakati zao. Na wengi wao walikuwa wakiishi kwenye slums baada ya kujipenyeza nchi za magharibi.Lakini haya yote ya kuzembea kwenye uangalizi wa uhamiaji kwenye nchi za commonwealth yaliwahi kuelezwa na mwanasiasa Enoch Powell 1968 kwamba Endapo wasipochukua hatua za kudhibiti wahamiaji ,basi italeta shida na mgogoro mkubwa wa kiusalama hapo Baadaye. Lakini wanasiasa wenzake wakampuuzia kwa kusema kwamba ni mbaguzi kwa misimamo yake ya kupinga uhamiaji.[emoji848]. Continued
 
3





Baada ya vita baridi kuisha mwanzoni mwa miaka ya 1990 ,. Nchi ya marekani na ulaya hawakuweka kipaumbele sana kwa maswala ya itikadi Kali kama kitisho kingine Cha ugaidi. Kwa mfano uingereza haikuipa kipaumbele mashariki ya kati kama sehemu ambayo sumu za ugaidi zilikuwa zinapikwa , badala yake serikali ya nchi hiyo ilijikita zaidi na maswala ya ugaidi huko Ireland kaskazini ambapo kulikuwa na kundi la kigaidi lililotaka kujitenga kwa Ireland kaskazini kutoka uingereza.
Mkurugenzi mkuu mstaafu wa shirika la kijasusi aliyefanya kazi kuanzia 1993 Hadi 1995 alisema kwamba mashirika ya kijasusi ya nchi za marekani na uingereza yalifanya makosa sawa katika kutochunguza athari za itikadi za madhehebu ya kiislamu ambayo yalikuwa yanahubiri itikadi Kali ambayo yangekuja kuzalisha ugaidi. Mashirika haya yalijikita katika kuangalia ukomunisti tu peke yake .
Na la zaidi ni kwamba uingereza ilidai Haina maslahi yoyote kwenye nchi za mashariki ya kati, hivyo isingeweza kuingilia maswala ya makundi ya kidini kwenye nchi hizo. Lakini nchi kama ufaransa wenyewe walikuwa tayari wameshaonja ladha ya ugaidi na walikuwa wanapigana vita hivyo vya ugaidi huko Algeria.
Kwa mfano shirika la kijasusi la uingereza la M15 mwaka 1994 waliamua kuvunja idara ndogo ya G7 iliyokuwa ikijikita zaidi kukusanya taarifa za Siri na ku monitor ugaidi wa kidini. Na hata baadaye idara hii iliporudishwa Tena mwaka 1996 , bado haikuwa na nguvu ya kukusanya taarifa hizo za hayo makundi ya itikadi Kali kutokana na kukosa base line ya kuanza kuchunguza mafundisho Yao na vilevile kukosa mashushushu watakaojipenyeza kwenye makundi haya kukusanya taarifa. Watu mbalimbali walianza kuionya uingereza na haya makundi yaliyokuwa yanashika Kasi nchini humo lakini kama kawaida wanasiasa hawakutaka kusikiliza.
Kwa mfano aliyekuwa mkuu wa kitengo Cha counter-intelligence ndani ya FBI kuanzia 1980 Hadi 1991 na baadaye akawa mkuu wa FBI huko Texas bwana Oliver revell , Alikiri wazi kwamba marekani walijua Kuna makundi ya kidini yenye msimamo mkali na yanakuwa kwa Kasi nchini uingereza , lakini wanasiasa kama kawaida hawakutaka kujishughulisha na hili . Hii ni kutokana na ukweli kwamba uingereza haikutaka kujiingiza kufanya upelelezi wa makundi haya ambayo yalikuwa yakisemekana Yana mfungamano na ugaidi labda kungekuwa na udhibitisho au ushahidi wa Moja kwa Moja.
Chanzo kingine pia kilisema kwamba inner circle za mashirika ya kijasusi nchini uingereza waligawanyika kutokana na hili swala. Wengine wakiamini kwamba kuingilia maswala ya kidini kungeleta athari kwa maslahi ya uingereza maeneo mbalimbali duniani na la zaidi uingereza ingeonekana siyo nchi inayoheshimu demokrasia na uhuru wa watu kuabudu.
Na hata aliyekuwa kiongozi wa kidini wa Anglican wa Canterbury lord Carey alilipa uzito hili swala la makundi ya kijihadi yaliyokuwa yanakuwa kwa Kasi sana kiasi kwamba akawatahadharisha wanasiasa wakubwa kama thatcher na pia John major kipindi wakiwa P.M lakini bado wakakaza na kusema Hilo haliwahusu Moja kwa Moja kutokana na ukweli kwamba wao wangeonekana kama wanaingilia uhuru wa dini za watu[emoji848].
Kwa mtu ambaye angekuwa ni mdadisi zaidi ni kwamba haya makundi ya kiislamu ya itikadi Kali yaliachwa yakuwe kwa kasi ,huku yakikingwa na wanasiasa wenyewe pasipo kujua wanafuga joka. Na hata Mohammed bakri wakati Fulani Alikiri waziwazi na kusema kwamba wao kama makundi ya itikadi Kali wasingeweza kuishambulia uingereza kigaidi kutokana na ukweli kwamba uingereza iliwapa hifadhi ya kisiasa/asylum na social benefits za hapa na pale . Lakini baada ya uingereza na mshirika wake marekani kuanza kujiingiza kwenye vita vya Afghanistan ,msimamo wa makundi haya ulibadilika Sasa uingereza ikawa ni next target ya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa Hawa wenye itikadi Kali, Makundi haya yakiamini kwamba uingereza ni adui wa imani ya kiislamu.
Hata serikali ya Algeria kupitia waziri wake wa mambo ya nje ,kwa wakati fulani walijaribu kuionya uingereza kwa kutopokea raia wa Algeria waliofukuzwa nchi hiyo kwa tuhuma za ugaidi, lakini kwa dharau uingereza ikajibu kwa kusema hao ni FREEDOM FIGHTERS . Hivyo watapewa hifadhi za kisiasa na benefits nyinginezo kama wakimbizi. What a mistake.Wachambuzi wanadai kwamba , uingereza na marekani kutokana na kuwa ni nchi za kidemokrasia na zenye ushawishi , lakini hazikuwa na mamlaka ya Moja kwa Moja kuchunguza vikundi vya dini za watu , labda tu kuwe kumetokea serious crime. Hii ndio ilikuwa chanzo kikubwa Cha kwanini nchi kama uingereza ilikuwa ikijivuta kufanya uchunguzi wa kina kwa Haya makundi ya kidini yenye itikadi Kali.
Na mzizi mkubwa wa kwanini hizi nchi hazikutaka kuingilia mambo ya kidini unaanzia mbali sana.
Wakati wa zamani ambapo nchi za ulaya zinaingia kwenye mgogoro wa kidini , vita vingi vilipiganwa na umwagaji mkubwa wa damu , ikapelekea mgawanyiko wa madhehebu enzi zile za vikings na Jesuits. Na ndio maana Hadi Sasa huko ulaya Kuna nchi ya Anglican church, Roman ,protestant na madhehebu mengine madogomadogo. Kutokana na hili uingereza ikaona si vyema kujiingiza kwenye migogoro ya kidini tena. Shida ndipo ilipoanzia hapa na uingereza ikashindwa kupambana na hizi religious fanaticism zilizokuwa zinakuwa upya kwa Kasi . Kwa sababu uingereza waliamini kupigana vita ya kidini ,ni Moja ya vita Moja ngumu sana kwakuwa unapigana na human beliefs ambazo zipo attached na nafsi Yake.. ni ngumu kuishinda vita ya namna hii. Na mbaya zaidi vyombo vya usalama hususan polisi hawakuwahi kufahamu jinsi haya makundi yanavyofanya kazi zao za kigaidi kisaikolojia. Kwa mfano wakati Fulani polisi walijichanganya wenyewe baada ya kumpiga risasi raia wa Brazili wakimdhania ni member wa kundi la kigaidi. Hali hii ilipelekea umma ku discuss competency ya polisi wa uingereza katika ku deal na ugaidi . Na ukiachana na hili ni kwamba tayari vyombo vya usalama vya nchi hiyo ikiwemo polisi ,tayari walikuwa wameathirika na kitu kinaitwa VICTIM CULTURE . Hii Ina maana kwamba makundi ya watu ambao ni minority kwenye jamii ya waingereza majority walikuwa mara nyingi wanaonewa na maaskari. Kwa mfano unakuta watu weusi mara nyingi kukamatwa na kuhusishwa na uhalifu. Hali hii ikapelekea mindset kwenye jamii kwamba polisi wanalenga makundi ya watu fulani Fulani tu peke Yake kwenye jamii na sio jamii ya wazungu. Hali hii ikawapa makundi ya kijihadi mwanya wa kufanya harakati zao. Na endapo polisi wanafuatilia harakati zao ,basi Moja kwa Moja wangepaza sauti zao kwamba wanaonewa na polisi kutokana na uchache wao ndani ya jamii.Hivyo polisi nchini uingereza wakawa wanasita katika kuchunguza au kufuatilia nyendo za makundi ya kijihadi.
Tatizo hili pia likatengeneza pia mgongano mwingine baina ya minority British Muslims na majority ya raia wengine. Ni kwamba mji wa Dewsbury ni miongoni mwa miji midogo ndani ya Yorkshire . Ni Moja kati ya miji ambayo ilikuwa Ina viwanda vingi vya nguo na wengi wa wakazi wake ni raia wa kigeni jamii ya Asia ambao wengi ni waislamu. Lakini mwaka 1987 ilitokea kisa kimoja kwenye mji huu ambapo wazazi wa wanafunzi kama 26 hawakutaka kuwapeleka watoto wao kwenye public school ambazo watoto wa kiislamu walikuwa wengi zaidi ya wakristo. Uchunguzi huu ilifanyika na ikabainikia kwamba wazazi Hawa walitaka watoto wao wakulie kwenye maadili ya kingereza Kwa maana walisema shule hizo zilikuwa Zina upendeleo kwa wanafunzi wa kiislamu ukilinganisha na wakikristo . Na wakaenda mbali na kusema shule hizi zilikuwa zinakiuka sera ya elimu ya uingereza ,ambayo ilitaka shule iwe ni multifaith na cultural diversity. Na hata maafisa wa serikali ya mtaa walipoulizwa kuhusiana na haya malalamiko ,wakakana . Ilikuja pia kubainika kwamba wanafunzi waliokuwa wa imani ya kikristo kwenye shule hizo walikuwa wakidhihakiwa na wenzao kutokana na mtindo wao wa ibada wa kusali. Lakini miaka 18 baadaye, ilikuja kubainika ndio mji aliokulia bwana Mohammed sidique Khan Ring leader ambaye alihusika na ulipuaji wa mabomu jijini London July 7 , 2005.Pia msikiti uliopo mji wa Dewsbury wa Jamaat tablighi ulikuwa ukihusishwa na mafunzo ya kidini yenye itikadi Kali. Pia ilbainika na waandishi wa habari kwamba Mufti Zubair Dudha wa msikiti huo ambaye alikuwa akifundisha vijana na watoto kwenye akademi ya Tarbiya madhara ya ugaidi na itikadi Kali , pia alihusishwa na ku support mashambulio dhidi ya nchi za magharibi kwa kile alichodai kwamba nchi za magharibi ni "the enemies of Allah". Tokea hapo jamii ya uingereza ilibadilisha mtazamo kuhusiana na Hawa wenzao katika maswala mazima ya kujamiiana. Ikawa imeonekana kwamba minority British Muslims wakawa wanapewa kipaumbele dhidi ya majority ya wenyeji. Hii ilitengeneza kitu wanakiita multicultural paralysis. Hii ni baada ya sera ya kudhibiti wahamiaji kufeli kwa kiasi kikubwa.
Kwa ripoti za kidemografia tokea mwaka 2001 za nchini uingereza zilikuwa zikibadilika kwa kiasi kikubwa. Ripoti hii ilionyesha kwamba raia wa uingereza ambao walikuwa wakihamia nchi nyingine ilibadilika kutoka idadi ya 50,000 Hadi 120,000 kwa Mwaka. Hii ilitokana wahamiaji wa nchi za Asia kuingia kwa wingi nchini humo pasipo udhibiti wa serikali. Na baada ya hapo ripoti ikaonyesha kwamba raia wa kigeni hususan wa jamii za Asia waliokuwa wakiingia uingereza ilifikia 200,000 kwa mwaka , mara nne zaidi ya idadi ilivyokuwa kati ya mwaka 1985 na 1995. Hali hii ilipelekea profile ya population structure ya uingereza kubadilika kwa kiasi kikubwa na kupelekea mgongano wa kiutamaduni baina ya wahamiaji na wenyeji na hali hii ikapelekea kukua kwa makundi ya itikadi Kali. Continued
 
4


Kiuhalisia baada ya tukio la July 7 2005 huko London kulifanya raia wengi wa uingereza kutetemeka kwa uoga usio na kifani. Baada ya mkanda wa video kuonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari hususan tv ,ukimuonesha Mohammed sadique khan akiongea kwa chuki dhidi ya uingereza na west , kulifanya sumu ya chuki kukolea kwa Kasi sana baina ya uingereza na Muslims community . Mkanda huo uliomuonesha huyu bwana akisisitiza kwamba uingereza itarajie zaidi umwagaji wa damu zaidi mpaka pale serikali hiyo itakapoacha kuonea na kuwanyanyasa jamii ya waislamu. Alitoa maneno makali yanayosema nanukuu " Our words are dead until we give them life with our blood,......" Akaendelea kusema kwamba".....Therefore, we are going to talk to you in a language you understand.... We are at war and I am a soldier. Your democratically elected governments continuously perpetuate atrocities against my people and your support of them makes you directly responsible, just as I am directly responsible for protecting and avenging my Muslim brothers and sisters. Until we feel security, you will be our target. Until you stop the bombing, gassing, imprisonment and torture of my people, we will not stop this fight"
Katika nukuu hii maneno ya kiwakilishi kama "you" alikuwa anawalenga uingereza , na "my people" na "we" alimaanisha jamii ya waislamu. Hapo ni kwamba alikuwa anachora mstari wa kiutengano kati ya ummah wa waislamu na jamii nyingine za west. Kwa kifupi Japo huyu bwana alizaliwa na kukulia uingereza , kusomea n kupata kazi huko ni kwamba hakuwa na huruma na uingereza hata kidogo.
Lakini wachambuzi wa hili swala wakatoa mawazo Yao wakisema hili tukio la bomu la kujitoa mhanga huenda sio kwamba ni sababu za kidini za kuifanya nchi za west kuwa civilized na Sheria za kiislamu , Bali ni kisasi tu kutokana na uingereza na mshirika wake marekani kuivamia Afghanistan na nchi zingine za mashariki ya kati. Wengine wakatofautiana wakidai mzizi wa hili tukio ni ubaguzi waliokuwa wakipitia waislamu nchini uingereza kwenye nyanja zote ikiwemo ajira , kwenye elimu n.k. kulikuwa na mgawanyiko katika hili Wengine wakadai kwamba Hawa wahusika hawakuwa waislamu barabara na vitendo walivyofanya magaidi Hawa havikubaliki hata kidogo na jamii za waislamu. Na pia mashambulizi haya yaliwalenga pia hata waislamu . Hivyo wengine wakasema wasihukumu jamii nzima ya waislamu kwa mabaya yaliyofanywa na wachache.
Na pia kwenye hili , aliyekuwa mwenyekiti wa msikiti mkuu kwenye mji Birmingham Mohammed Naseem Alikiri waziwazi na kusema hakuna ushahidi wa Moja kwa Moja wa kuonyesha waliotenda tukio hilo la shambulio la kigaidi ni waislamu na pia akamwita tony Blair P.M wa uingereza kuwa ni mwongo na anachafua dini za watu. Na pia akaenda mbali na kusema hakuna mwislamu popote duniani anayejua Wala kusikia kitu kinaitwa Al Qaeda.
Kwa kifupi viongozi wa dini ya kiislamu wengi walikuwa wanakwepa kuuhusisha ugaidi na uislamu moja kwa moja lakini in deep down behind the scenes mambo yalikuwa tofauti.
Kwa mfano wengi wa viongozi Hawa kidini walidai kwamba kwa mujibu wa mafundisho ya Quran ,haisupport kwa namna yoyote vitendo vyovyote vya itikadi Kali na za kuua wengine ambao WASIO NA HATIA kwa fatwa.Lakini wachambuzi wa historia na theolojia wakadai kwamba haya ambayo viongozi wa kiislamu wanasema kwamba uislamu hauruhusu kuua kunaacha maswali na loopholes kwa kile walichokuwa wanakiri.
Kwa mfano kwenye Aya za kwenye kurani ya surat Al maidah mstari wa 32 unasema kwamba "Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote...."
Wachambuzi wanasema ukiisoma Aya hii ya korani kwa haraka haraka ni wazi kabisa uislamu hauruhusu Wala ku glorify mauaji kwa Namna yoyote ile na kwamba anayeua ni adui wa watu wote. Lakini katika sura hii ya Al maidah kwenye korani Kuna mstari unaendelea mbele wa 33 unaosema "Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa". Wachambuzi na wataalamu wakadai kwamba kupitia Aya hizi mbili ni kwamba uislamu kwa namna nyingine walikuwa wanahamasisha kuuawa kwa wote ambao walikuwa against na imani ya kiislamu haijalishi kama alikuwa ni mwema kwa kusaidia wengine (uingereza kuwakaribisha waislamu wakimbizi katika nchi hiyo) lakini uingereza na marekani walikuwa wanapambana na ugaidi kwenye nchi za Afghanistan na Pakistani na jeshi la jihad wanaotaka kuwe na Islamic states. Aya hizi zilileta mkanganyiko kuhusiana na hili swala la ni Je uislamu ulikuwa unasupport ugaidi kwa Siri huku hadharani wakiukana?[emoji848]

Mwaka 2004 wizara ya mambo ya ndani ya uingereza ilifanya survey ambayo matokeo yake yalishtua wataalamu . Kwenye survey hii , ilibainika kwamba takribani 26% ya raia wa uingereza wa kiislamu walikuwa hawana loyalty na nchi ya uingereza. Pia 13% ulionyesha pia raia hao walitetea harakati za ugaidi na 1% walikuwa wanajihusisha moja kwa Moja na vitendo vya ugaidi ndani na nje ya uingereza. Wachambuzi wakadai kwamba hii asilimia Moja ya wanaojihusisha na ugaidi ni ndogo ikilinganishwa na mambo yalivyokuwa kwenye uhalisia. Kwa mfano ripoti za kijasusi na pia za idara za polisi zilionyesha raia wengi wa uingereza ambao ni waislamu wamewahi au walitarajiwa kupitia kwenye kambi za Al Qaeda kujifunza ugaidi. Hata kura za maoni kwenye shirika la bbc ,lilionyesha 15% ya waingereza waislamu walisapoti kushambuliwa kwa Marekani 9/11. Ripoti zingine zikaonyesha kwamba kati ya 8% na 26% ya raia wa uingereza ambao ni waislamu walikuwa wazalendo kwa nchi hiyo ila wengine wakiwa na msimamo wa kati. Ripoti zingine zikaonyesha kwamba asilimia 56 ya raia Hawa walikuwa wanapendekeza waislamu wengine waikubali nchi ya uingereza na kuwa loyal ila asilimia 32 ya raia wakapinga na kusema uingereza ni nchi ya kikafiri na haifuati sheria za kiislamu na mfumo wa maisha yake ni batili. Ripoti hizi zilionyesha kwa kiasi gani nchi ya uingereza ilikuwa katika steji gani ya kupambana na joka la ugaidi. Na ripoti hii ilionyesha ni jinsi gani katika dimbwi hili ugaidi unaelea kwa kasi dhidi ya nchi za kimagharibi.
Kwa mujibu wa ripoti hizi , swali likabaki Je kwanini chuki dhidi ya uingereza kutoka kwa jamii ya kiislamu ilikuwa inakuwa kwa Kasi? . Inadaiwa kutokana na mfumo wao maisha na tamaduni za kiislamu , wengi wao walikuwa wakitengwa na jamii ya wazawa wa uingereza ,na kwa kifupi ilikuwa ngumu kwa tamaduni za kiislamu za mashariki ya kati ku fit kwenye tamaduni za kimagharibi na mbaya zaidi mfumo wao wa kuishi walitaka uwe ndio mfumo rasmi nchini uingereza. Kutokana na mgongano huu ikaonekana kwamba wao ndio wanaonewa na nchi za magharibi katika ku empose sheria za kiislamu [emoji848]. Lakini haya yote yalitokana na mahubiri ya sayed Qutb na wanazuoni wenzake kama Sayed Abu'l Ala ambao mahubiri Yao yalijikita katika kuanzisha Islamic states na serikali nyingine za kidunia lazima zifutwe kupitia jihad . Na pia Qutb huyu alienda mbali na kusema nanukuu "destroying the kingdom of man to establish the kingdom of heaven on earth." Na hili ndilo lilikuwa msingi wa karibia mafundisho Yote ya kiislamu. Continued
 
Back
Top Bottom