Juma Mgunda afungiwe kufundisha mpira ligi kuu Tanzania

Juma Mgunda afungiwe kufundisha mpira ligi kuu Tanzania

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kufundisha timu mbili za ligi moja kwa wakati mmoja wa ligi haikubaliki na sio weledi. Madhara yake ni pamoja na:

1. Juma mgunda ana mapenzi/maslahi na timu mbili za ligi kuu kwa wakati mmoja.

2. Juma mgunda anaweza kupanga matokeo ndani ya ligi kuisaidia Coastal au Simba katika mazingira fulani kwenye mwenendo wa ligi kwa kuitumia Coastal au Simba.

3. Mgunda anaweza kuidhoofisha Coastal Union kwa kupenda au kutokupenda.

4. TFF imeanzisha chaka jipya kwenye mpira wa TZ (Presidency).
 
Tulia wewe, tunaenda kuwakilisha taifa na sio ligi za mchangani za tiefuefu
Hii inasikitisha sana. Ndio maana sio ajabu kumbe kukuta coastal union chini ya mgunda ikifungwa kirahisi magoli mengi na simba, kitendawili kimeteguliwa. Karia ana shida kubwa sana.
 
Mkuu kama Mr.Mgunda hajavunja sheria yeyote hapa, relax na tafuta pesa acha gubu
Kwani timu inaweza kumtumia kocha bila mkataba? Kama mgunda hakuwa na mkataba na mgunda je inaruhusiwa timu kufanya hivyo?
 
Kosto wanasema hawana mkataba naye isipokuwa wapo kwenye mazungumzo naye ya kuongeza mkataba mpya
 
Tulia wewe mwaka 98 tuliwaazima Yanga wachezaji watatu wa kucheza michuano ya klabu bingwa Africa
Ao wachezaji hawakuazimwa, walisajiliwa. Monja liseki, Alfonce Modest na Jumanne Ramadhani. Caf hawana iyo michezo ya kuidhininisha wachezaji wa kuazima.
Walisajiliwa kutoka Simba kwenda Yanga. Nimasufuria ya shughuli ndio Yana azimwa.
 
Hii inasikitisha sana. Ndio maana sio ajabu kumbe kukuta coastal union chini ya mgunda ikifungwa kirahisi magoli mengi na simba, kitendawili kimeteguliwa. Karia ana shida kubwa sana.
Mara hii kichefu chefu?
Kula ndimu itakusaidia bado una safari ya miezi 9
 
Kosto wanasema hawana mkataba naye isipokuwa wapo kwenye mazungumzo naye ya kuongeza mkataba mpya
Huo ni uongo waliofundishwa kuusema, kama hakuwa na mkata nao kwanini simba iliwaponheza costo kukubali kumtoa mgunda, kwanini costo walikuwa wanalalamika kutoshirikishwa kwenye dili? Mkataba wa mgunda na costo ulikwisha toka lini?
 
Back
Top Bottom