Juma Nature andaa Shoo yako kuonesha wewe ni mkubwa

Juma Nature andaa Shoo yako kuonesha wewe ni mkubwa

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
4,664
Reaction score
9,929
Kiroboto sihitaji andika sana, hebu kaa na wadau mjini usisubirie upepo wa sugu na lile tamasha lake kaa na wadau itisha tamasha HESHIMA YA JUMA NATURE siku moja tu usiku mmoja tu.

Hiyo siku tuje turuke goma zako
Tupakue ugali
Tumuimbie radhia
Tulianzishe kigheto gheto
Tumtulize mtoto iddy
Tucheze hili game
Tuwatafute migambo
Tusifie muungano wa ccm na cuf

Wanakudharau wanasahau umewalea TMK
 
Kuna fundi wangu hata kama hana kazi na ikatokea labda dayworker ya 25k wala hawezi kwenda.

Kumtoa nyumbani kwa day walau 30k anaweza kuja, tena muwe mnajuana.

So simshangai kiroboto kukataa 500k.
 
Hajapata shida huyo
Kwa hiyo walioenda pale kumbe wote wana shida?

Na amejuaje kuwa shida ya jamaa kui-solve ni laki 5?

Kwa hiyo tamasha la Diamond ni mahususi kutumbuizwa na wasanii waliokuwa na shida?

Kumbe hili Festival ni foundation ya kuwasaidia wasanii wenye shida?

Kama ndio hivyo anatoa hela ili kuwasaidia si angewapa hizo hela wakiwa makwao bila kuwasumbua mpaka majukwaani?
 
Ila kiukweli kama alipewa offer ya 500k ni ndogo wadau.

Laki 5 anafanyia nini cha maana? Hata akisema akale bata na wana inaisha dk 30 tu.
 
Kiroboto sitaji andika sana ebu kaa na wadau mjini usisubilie upepo wa sugu na lile tamasha lake kaa na wadau iitisha tamasha HESHIMA YA JUMA NATURE siku moja tu usiku mmoja tu

Hiyo siku tuje turuke goma zako
Tupakue ugali
Tumuimbie radhia
Tulianzishe kigheto gheto
Tumtulize mtoto iddy
Tucheze hili game
Tuwatafute migambo
Tusifie muungano wa ccm na cuf

Wanakudharau wanasahau umewalea TMK
Hiyo unayoita dharau ni kuwa wameshindwana kwenye malipo. Na ni kiki nzuri sana kwake, hata hivyo yeye pamoja na waandaaji wa matamasha hawatochukua fursa hii.

Itapita kama upepo, mtasubiri aondoke duniani ndio muanze kusema "alikuwepo", "unamjua Nature wewe"
 
wasanii wazamani hawataki kuendana na wakati wakati wa sasa ni mwendo wa kiki tuu. kiroboto aendeleze chokochoko maana watanzania wanapenda ujinga ujinga,

atoe tena dongo lingine kwa wasafi watu waendelee kuwa mdomoni.

aongee na diamond kabisaa kuusu huu mkakati.

tena hili awatumie clouds itamake sense atafuta na malegendary wengine wakumuunga mkono, kwa kifupi ajitoe ufahamu,

amtumie pia yule mtangazaji tumbo tumbo sijui anaitwa mujaki.
 
Back
Top Bottom