Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Mkongwe wa ujiji akina Mzee Mbano akina sheikh kakolwa sheikh kiumbe Mzee kiburwa sheikh Karita Mzee manju msambya na wakongwe wengine
Wasemeje ikiwa nawe ni mkongwe
Kigoma Ujiji wenyewe kina Marehemu Mzee Jabu alikuwa ana nyumba pia Ilala Shariff Shamba. ila sio mbaya wapo vijana leo hii wenye ujiji yao waje kutusaidia hapa kina Dennis Ntaita Rashid Mzee wa posta Simba na Sele wa Saratoga...
 
Uliyesema amerithi kazi Njemba anafanya kazi zipi sasa kama bado mnasema "Njemba angekuwepo.....!!!?"
Aliumwa saratani, na alikuwa mtu mzima sana, alizidiwa maradhi yake akiwa kitandani kwake. Mwaka 2006/2007 na 2008 Kigoma Ujiji ilifiwa na wazee mashuhuri wakiheshimiwa kwa elimu zao. 2006 alikufa gwiji Akiitwa Selemani Apelee, mtu aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga kabla ya kutokea, (machale) kabla ya hatari alijua, na hats majambazi walipokusudia kumuua walimpiga sana kwa mapanga na marungu, na Zaidi hawakuweza walau kumjeruhi, walipoteza nao maisha. Waliona heri wamchome moto jambo ambalo halikufanikiwa pia moto haukuwa na nguvu ya madhara kwake.

Aliwaeleza wamuache na akawauliza iwapo wanataka kumuua kweli. Walipomthibitishia alijizingua na kuwaambia wamuue. Hapo walimpiga akafa.

Kisha 2007 alikufa Mzee Juma kwa saratani, waliwaeleza familiar na majirani zake kuwa atakufa kwa matadhi Yale, aliwaita wanae watatu wa kiume na kuwapa kila mmoja vitabu na elimu zake. Hivyo alipokuwa akiumwa alikuwa tayari ana warithi wanaosimamia kumuuguza na kumtunza, huyu mzee aliwaambia wanae karibu na kifo chake kuwa siku ya kufa kwake itakuwa Alhamisi inayoisha. Na kweli alikufa Alhamisi saa tano na nusu usiku.

Mji ulikuwa na simanzi kubwa kuondokewa nae, walizika, hakukuwepo na mahangaiko yoyote au miujiza ya kutisha katika kifo chake.

Siku ya tatu alitangazwa msibani mrithi wa Kazi zake, anaechukua jina la baba yake.

Wasichokijua watu ni kuwa Juma Njemba alikuwa chief wa kabila lake hivyo pia yupo miongoni mwa wanae ni chifu. Hata Yule aliyegombea urais na Magufuli akiitwa Chief Luta Losa Yemba wa chama anachoongoza Hamad Rashid wa kule Zanzibar ni motto wa mdogo wake Juma Njemba.

Mtu wa tatu akiitwa Issa Sadick huyu nae alikuwa mzee mwenye elimu kubwa na uganga mzito sana, watu wote hawa waliwasumbua wachawi na kuwapa taabu sana, wote walipokufa ilikuwa ni faraja kwa wachawi.

Wazee hawa walikuwa ni sehemu ya kimbilio la wengi, waliwaathiri watu wenye kuiba ndoa za watu, waliwaathiri watawala wenye majivuno, na kiburi na hata sass Kigoma huwaza kuhusu Juma Njemba kwa ajili ya mtawala wetu alivyo.

Duuh unasema na hata sasa ,Kigoma uwaza kuhusu Juma Njemba juu ya kiongozi wetu wa sasa alivyo,wafanye yao tu maana hakuna namna.
 
Watoto wake hawakusoma shule mkuu..Kwake ilikuwa ni " boko haramu" ..Walisoma madrasa tu na yeye ndio.alowasomesha Quaran Tukufu
Watoto wake wamesoma shule za msingi mbili wapo waliosoma Kaluta Primary na wapo waliosoma Azimio Primary

Wapo waliosoma elimu ya Sekondari pale Dodoma Bihawana sec school km 32 toka Dodoma Mjini.

Wapo waliosoma Tabora girls na Buronge Sec iko Gungu Kigoma
 
Mkongwe wa ujiji akina Mzee Mbano akina sheikh kakolwa sheikh kiumbe Mzee kiburwa sheikh Karita Mzee manju msambya na wakongwe wengine
Wasemeje ikiwa nawe ni mkongwe
Wakongwe wa Ujiji ni Said Arobati, Saleh Ndauga, Kabeke, Kitama, Njemba, Omari Kakolwa, Sheikh Kitumba, Sheikh Khalfan, Yusuf Tosiri, Abdallah kitenge, Mussa Rehani, Abdallah Chakuwa, Ganja Smoking, Saadan Abdul Kandoro, Snow White, Mohammed Saddallah, King Seleman, Issa Maganya, Mzee Mnukwa, Abubakar Mwilima, Jumapili Kasongo, Mzee Kocho, Issa Sadiki, Mzee Saliboko, Nk
 
Watoto wake wamesoma shule za msingi mbili wapo waliosoma Kaluta Primary na wapo waliosoma Azimio Primary

Wapo waliosoma elimu ya Sekondari pale Dodoma Bihawana sec school km 32 toka Dodoma Mjini.

Wapo waliosoma Tabora girls na Buronge Sec iko Gungu Kigoma
Acha uongo
 
Wewe muongo aseeee

Halafu huyu Abu fiiyza Hakuna aliyemuambia amfuate PM kwanin umpe tuhuma za utapeli?

Unasema watoto wake hawajasoma wakati moja ya watoto ni mwandishi wa habari nenda ujiji kaulize namtaka Mwinyi mbegu njemba yeye atakupa ukweli
Usiwape watu tuhuma kulazimisha uongo

Njemba humfahamu sema umesikia kwa watu
Ukiambiwa moja ya wake zake yuko hai utaamini

Nenda ujiji waulize wakwambie ni nani hasa chief Jumaa Njemba achana na soga za kusikia Mtt wake Mwinyimbegu ni rahimu na maarufu mno Mji ule mtafute akueleze kuhusu babake
Ndio maana nikamueleza hakutafiti, Mwinyi Mbegu jamaa mi Rahim nazumgumzaji mzuri sana, pia mwanae mmoja amewahi kufanya Kazi Mwananchi Newspaper miaka 2002 pamoja na kina Absolum Kibanda, Deodatus Mkuchu, Huyu mwanahabari kafa juzi anaitwa Shadrack Sagati nk

Huyu muandishi ni mpevu wa masala ya historia, jamaa kama Mohammed Said. Sasa Likud angeuliza sisi tunaoifaham ile familia toka zamani
 
Anajuaje kama ataenda mbinguni au peponi??? But anyway jamaa alifanya mambo mengi sana yasiyompendeza Mungu kwa kweli.........

Na jamaa naskia kweny kazi yake alikua hapokei hela yako mpka uone matokeo....sasa ww akufanikishie mchongo afu usimlipe....weeeeeeeee anasomba nusu ya ukoo wako
hahahahah
 
mi kazi yangu kutoa ushahidi niliouona kikweli bwana likud yuko sahihi kuwa hakuna mwenye uwezo ule tena na hilo nimesikia kwa nduguze wenyewe narudia niliishi kigoma 2 years ,ila wajukuu zake pia waganga ila tukirank top 20 ya waganga noma kigoma hao wajukuu hamna kitu hii aliniambia rafiki yangu marehemu kassim said tajiri wa mabot miaka hiyo so msimfate yoyote inbox hata mm mtaliwa sana

Dah huyu mzee kasim alifariki!! Alikuwa na mabot yakutosha pale kibirizi!!
 
Likud uzi wako umekuumbua yaani hujui kitu kabisa. Bila shaka una macho mekundu na maimani ya kishirikina
Anaishia kuwaambia watu matapeli utadhani kuna mtu kaambiwa achangie senti yake

Ni ngumu kuunyamazia kimya uongo na nilimwambia hakufanya tafiti vyema Kama Wale waliodai Abdul nondo aweza asiwe raia

Tukimwambia Abdul Nondo ni ktk jamaa wa Mzee njemba atakataaa pia

Abuu fiiyza komea hapo hana hajualo kuhusu Huyo Mzee itakuwa amesikia kijiweni kaleta thread apate credibility anapingwa kwa rejea za uzani anakomea Kuwaita watu matapeli mvutuwe huyu
 
Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.

Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.

Sifa za Juma Njemba zilienea katika mji wa kigoma na nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda.

Mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifurika kilingeni kwa Juma Njemba kwa ajili ya kazi moja tu ambayo ni kuwaua adui zao kwa kutumia uchawi wa Juma Njemba.

Kazi hii ya kuua watu kwa uchawi ilimtajirisha sana bwana huyu.

Kwa zaidi ya miaka ishirini aliyo Fanya kazi hii, Juma Njemba anakadiriwa kuwa amewauwa kichawi takribani watu elfu mbili na ushee ambao ni sawa na wastani wa karibu watu mia kwa mwaka

Juma Njemba alioa wanawake wengi sana .Anakadiriwa kuwa alioa zaidi ya wanawake 200 huku wengi kati yao akiwa anawaoa na kuwaacha na aliwaacha kwa sababu ndogo sana.

Kwa mfano akiwa anakula chakula halafu kikawa kimezidi chumv, au chai ikapungua au Kuzidi sukari au akatafuna jiwe kwenye wali basi mwanamke aliyepika chakula hicho atapewa talaka tatu papo hapo na wataliki wake wote walikuwa wanaishia kufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya muda mfupi na walio bahatika kuishi basi waliishia kuwa vichaa au kuugua maradhi mazito kama vile kiharusi nakadhalika.

KATIKA HILO SABABABU YAKE ILIKUWA " WAKE ZANGU KWA MAISHA NINAYO ISHI MIMI SIWEZI KWENDA PEPONI..PEPO YANGU NI HAPA HAPA DUNIANI ..PEPONI HAKUNA WALI WENYE MCHANGA WALA ULIOZIDI CHUMVI..SITAKI KUPATA TABU YA AINA YOYOTE ILE HAPA DUNIANI NA YEYOTE ATAKAE NISABABISHIA TABU YA AINA YOYOTE ILE BASI NITAMFUTILIA MBALI..."

Ukiachilia mbali mke wake wa kwanza na wa pili ambao aliwaoa wakati wa ujana wake kabla hajapata hiyo ilmu ya kuua watu kwa uchawi wake zake wote alikuwa anawaoa wakiwa bikira na alikuwa akiamini.wakeze hao walikuwa ni ma hurulain wake wa hapa DUNIANI.

Akimpenda binti yako basi anatuma tu ujumbe kuwa siku fulani atakuwa mgeni wako ambapo atakuja kumposa binti yako na hakuna mzazi ambae alikataa kumuozesha bintiye kwa Juma Njemba.Walio thubutu kufanya hivyo walikufa wao au binti zao au wote kwa pamoja..

MTU huyu aliogopwa kama Mungu..Wageni walio Tembelea katika kata aliyo ishi kwa sababu mbalimbali walikuwa wanaenda kuripoti na zawadi kwa Juma Njemba na wakati wa kuondoka walienda kumuaga kwa heshima zote.

Siku moja moja.alikuwa anapenda kuhemea soko kuu la pale Ujiji Kigoma.

Wafanyabiashara wa sokoni hapo walikuwa wakimuona walikuwa wakijipendekeza kwa kumuomba wampe bidhaa zao bure.

"Baba pitia hapa dukani kwangu uchukue walau kilo kumi za nyama baba ..Hii ni swadaka yangu kwako "

" Baba ukitoka buchani upitie hapa kilo 20 za mchele bill itakuwa kwangu" .Hayo ni maneno ya baadhi ya wafanya biashara wakijipendekeza kwa Juma Njemba.

Hata hivyo Juma Njemba alikuwa akikataa ofa hizo za nidhamu ya uwoga kwa kuwaambia kwamba yeye ana uwezo kuliko wao.

Ilikuwa ukimdhulumu MTU basi ataenda kulalamika kwa Juma Njemba halafu Juma Njemba atatuma ujumbe wa kukuita na ukifika atakwambia ulimpe deni lake.

Juma Njemba alifariki mwaka 2001. Waliokuwa NAE karibu wakati wa kifo chake wanasema kilikuwa ni kifo cha mateso makubwa sana..

Watu wa Kigoma waliposikia Juma Njemba amefariki walifanya sherehe kubwa sana.

Juma Njemba alifanya vituko na matukio Mengi sana ya kichawi ..Nikipata nafasi nitakuwa natupia kimoja baada ya Kingine ili watu waweze kujua
Hapo kwenye mwaka Wa kifo chake nadhani umekosea mkuu...ila sina uhakika....nakumbuka alikuwa anakaa mitaa kama unaelekea solo LA kagera..tulikuwa tukipita pale tunaambiwa tusipige kelele...siku moja nilimkuta ameket pale barabaran kwake chini ya mti nilitetemeka.
 
Dah huyu mzee kasim alifariki!! Alikuwa na mabot yakutosha pale kibirizi!!
Juma Njemba hakuacha wajukuu wenye uwezo wa kuwa waganga kwa umri wao, wote wapo mashuleni wakisoma.

Pili hata walio na ujuzi ule wamewekewa viwango maalum vya kutumia ufundi wao kwa kadiri ya makuzi yao.

Baba yao alipokuwa na miaka Kama yao hakuwahi kuonesha uwezo wake aliokuwa akiuonesha kwenye uzee wake
 
Back
Top Bottom