Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Swali zuri sana!
Huyu kwenye labial lake alikuwa ni chief, na alikuwa ni mkuu wa ngoma za makabila yake pia, acha Kigoma alikuwa ni chief wao kwa Tanzania hii, toka ikiitwa Tanganyika. 1963 Kama sikukosea nchi yetu ilifuta utaratibu wa kuwatawalisha machifu.

Lakini baadhi ya Jamii ziliendelea kuheshimu. Kama Chief Fundikira wa Nyanyembe, au Mtwa Adam Sapi, Chifu Burito wa Zanaki nk.

Yeye alikuwa chifu wao. Hivyo kwa kadiri jamii ya labial lake walivyomuheshimu, kwa kadiri ya tabia zake kwa watu wake ndivyo pia jamii kwa upana walimchukulia hivyo.

Katika tabia ninazozijua alikuwa mtu mkali sana, mwenye sauti Nene. Hivyo akikemea kwa sauti ya ukali unajua tu hapa mziki mnene.

Jina la Njemba alipewa akiwa katika umri wa Kati kwenye miaka baina ya 1947 na sitini mwanzoni, huyu alikua msanii miaka hiyo wa ngoma za kirua, aliigiza walivyokuwa wakicheza.

Pia alikuwa msanii wa vichekesho kwenye stage, na aliwahi kuwa kamanda wa TANU YOUTH LEAGUE miaka ya TANU.

Ushahidi wa haya muulizeni Meya wa Zamani wa Mji wa Kigoma Ujiji Mzee Abdallah Shaabani Tofiki. Anajua Zaidi kwa ni shuhuda wa hayo. Au mzee Ramadhani Anzuruni (KIBOKO) mzee aliyesalia kwa umri mkubwa katika eneo alilokuwa akiishi Juma Njemba.
Lakini hao wote walikuwa hawaogopeki kasoro yeye.
Machief wengi tunajua walikuwa warozi.
 
Sasa kwanini unadhani unafaa tukuamini?
1.Umefail kwny tarehe yake ya kufa na kuzikwa
2. Ulichioweza ni kuleta majina na idadi ya familia ya huyo Juma, ambayo ni ngumu kwa yyte humu ku verify kama usemacho ni kweli.
3. Umejikita only kuongea positive side bila ya angalau kijihusisha na anacho kiongea mleta mada na member wengine humu waliofika kilingeni kwake na kukubaliana na Likud
4. unakanusha tu anachosema Likud basi, yaani kama kuna kitu au jambo hutaki lisimwe
hahaha nimekupenda bure
 
Hivi we jamaa una akili kweli?kuna mtu anaweza kusema baba yake alikua muuaji au mshirikina?
Kwani wewe unazo ziko sehem Gani?

Unawezaje kumwita mtu muuaji na mshirikina kwa vimaneno vya kuokoteza??

Jumaa Njemba ni muungwana ktk ujiji aliyeiishi ujiji kwa heshima kubwa
 
ukikubali afe haraka mzee alikua na kisu kikali sana unachukua unachoma kichwani wewe mwenyewe basi mbaya wako kule muda huohuo anaaga dunia na ukisema afe taratibu achukue hata siku tatu walau wapeleke hospital wauguze kidogo ulikua unapewa sindano na kitambaa kwahiyo kile kitambaa kinalowana na kinalazwa kifuani kwenye kio kwenye ile sura ya mbaya wako unakua unachoma moyo taratibu huko mbaya wako anazidiwa kesho unachoma tena huko unasikia fulani hali mbaya ukija kumalizia sindano ikigonga kioo na mtu kwaheri.
Kwa msingi huo aliyekuwa anaua ni Juma Njemba au hao waliokwenda kutimiza azma za kuua wenzao?
 
Back
Top Bottom