Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

mimi ni mtu wa mikoa nyanda za juu kusini, shughuli zangu ni za kusafiri hapa na pale.

kuna wakati nilibahatika kwenda machame,nilichokiona huko kuhusu maendeleo ya mtu mmoja mmoja kilinifanya niwe nawa admire sana watu wa mkoa wa kilimanjaro na bidii yao ya kutafuta pesa

mwenyeji wangu alinitembeza ili nijionee majumba ya kifahari ya wamachame yaliyojificha kwenye vichaka vya migomba ya ndizi na kunitajia majina ya watu wa koo maarufu za machame zinazomiliki majumba hayo.

kwa siku nilizokaa machame sikusikia kabisa kuhusu hekaya za uchawi,ushirikina au mtu kalogwa.
Uchawi wa kimachame ni kuwatoa kafara waume zao ili wapate utajiri.Familia nyingi za kimachame wamama ndo matajir tena ni wajane baada ya kuua waume zao.
Hawana time na watu wa pembeni bali ndani ya familia baba na mama hujishughulisha kwa bidii na pale wanapofika ktk utajiri basi mama wakimachame humtanguliza mumewe mbinguni, hubakia wajane na kuanza kwenda kununua wanaume uko nchini Kenya.
 
pamoja na hivyo, bado watu wa mkoa wa kilimanjaro wana unafuu sana na masuala ya imani za kishirikina ukilinganisha na watz wa mikoa mengine.

mikoa ya huku kwetu imani ya ushirikana ipo juu sana.

kuna mwaka fulani baba yangu alitaka kuwajengea wazazi wake nyumba ya kisasa huko kijijini kwao songea.

bibi alimkataza kwa kuhofia kwamba kama baba angefanya hivyo, baadhi ya wazee wa kile kijiji wasingefurahi.

baba yangu angeuliwa kichawi kwa kosa la kuwajengea wazazi wake nyumba ya kisasa.

baba hakujari, akawajengea wazazi wake nyumba ya kisasa pale kijijini na mpaka leo ipo na wala hakupatwa na jambo lolote.

visa kama hivi huwezi kuvisikia uchagani, ndio maana ukitembelea vijiji vya mkoa wa kilimanjaro unakutana na majumba makubwa ya kisasa ambayo watoto wamewajengea wazazi wao.
 
aisee jamaa umefikiria sana
Simple logic, mwana familia hakuna mahali kazungumzia kwamba karithi hata tunguri moja.

Sasa LIKUD kakomaa na utapeli, watu kumfata jamaa PM, utapeli mwisho insta etc, kiasi mpaka nahisi ndo yalikuwa malengo yake kuanzisha thread.

Na kuna part amesema ataendelea, nina uhakika hataendelea nayo kwa sababu wana ukoo wameingilia kumlinda mdingi.
 
Bila kuroga duniani utapata pesa ya kula tu ndogo ndogo na kila biashara utakayofanya utaishia kupata hasara hata kama hiyo biashara uliifanyia utafiti wa kina na tathmin miaka 1000 bado utaishia hasara. Mshana jr njoo uwarlekeze pesa nyeusi ikoje.
Dah sitaki kurejea huko ndugu yangu.. Hakuna amani kabisa
 
Teh teh teh! watoto huwa wanabishana watu wazima huwa wanaelewana. League zinaendeshwa vilabuni.
 
Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.

Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.

Sifa za Juma Njemba zilienea katika mji wa kigoma na nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda.

Mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifurika kilingeni kwa Juma Njemba kwa ajili ya kazi moja tu ambayo ni kuwaua adui zao kwa kutumia uchawi wa Juma Njemba.

Kazi hii ya kuua watu kwa uchawi ilimtajirisha sana bwana huyu.

Kwa zaidi ya miaka ishirini aliyo Fanya kazi hii, Juma Njemba anakadiriwa kuwa amewauwa kichawi takribani watu elfu mbili na ushee ambao ni sawa na wastani wa karibu watu mia kwa mwaka

Juma Njemba alioa wanawake wengi sana .Anakadiriwa kuwa alioa zaidi ya wanawake 200 huku wengi kati yao akiwa anawaoa na kuwaacha na aliwaacha kwa sababu ndogo sana.

Kwa mfano akiwa anakula chakula halafu kikawa kimezidi chumv, au chai ikapungua au Kuzidi sukari au akatafuna jiwe kwenye wali basi mwanamke aliyepika chakula hicho atapewa talaka tatu papo hapo na wataliki wake wote walikuwa wanaishia kufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya muda mfupi na walio bahatika kuishi basi waliishia kuwa vichaa au kuugua maradhi mazito kama vile kiharusi nakadhalika.

KATIKA HILO SABABABU YAKE ILIKUWA " WAKE ZANGU KWA MAISHA NINAYO ISHI MIMI SIWEZI KWENDA PEPONI..PEPO YANGU NI HAPA HAPA DUNIANI ..PEPONI HAKUNA WALI WENYE MCHANGA WALA ULIOZIDI CHUMVI..SITAKI KUPATA TABU YA AINA YOYOTE ILE HAPA DUNIANI NA YEYOTE ATAKAE NISABABISHIA TABU YA AINA YOYOTE ILE BASI NITAMFUTILIA MBALI..."

Ukiachilia mbali mke wake wa kwanza na wa pili ambao aliwaoa wakati wa ujana wake kabla hajapata hiyo ilmu ya kuua watu kwa uchawi wake zake wote alikuwa anawaoa wakiwa bikira na alikuwa akiamini.wakeze hao walikuwa ni ma hurulain wake wa hapa DUNIANI.

Akimpenda binti yako basi anatuma tu ujumbe kuwa siku fulani atakuwa mgeni wako ambapo atakuja kumposa binti yako na hakuna mzazi ambae alikataa kumuozesha bintiye kwa Juma Njemba.Walio thubutu kufanya hivyo walikufa wao au binti zao au wote kwa pamoja..

MTU huyu aliogopwa kama Mungu..Wageni walio Tembelea katika kata aliyo ishi kwa sababu mbalimbali walikuwa wanaenda kuripoti na zawadi kwa Juma Njemba na wakati wa kuondoka walienda kumuaga kwa heshima zote.

Siku moja moja.alikuwa anapenda kuhemea soko kuu la pale Ujiji Kigoma.

Wafanyabiashara wa sokoni hapo walikuwa wakimuona walikuwa wakijipendekeza kwa kumuomba wampe bidhaa zao bure.

"Baba pitia hapa dukani kwangu uchukue walau kilo kumi za nyama baba ..Hii ni swadaka yangu kwako "

" Baba ukitoka buchani upitie hapa kilo 20 za mchele bill itakuwa kwangu" .Hayo ni maneno ya baadhi ya wafanya biashara wakijipendekeza kwa Juma Njemba.

Hata hivyo Juma Njemba alikuwa akikataa ofa hizo za nidhamu ya uwoga kwa kuwaambia kwamba yeye ana uwezo kuliko wao.

Ilikuwa ukimdhulumu MTU basi ataenda kulalamika kwa Juma Njemba halafu Juma Njemba atatuma ujumbe wa kukuita na ukifika atakwambia ulimpe deni lake.

Juma Njemba alifariki mwaka 2001. Waliokuwa NAE karibu wakati wa kifo chake wanasema kilikuwa ni kifo cha mateso makubwa sana..

Watu wa Kigoma waliposikia Juma Njemba amefariki walifanya sherehe kubwa sana.

Juma Njemba alifanya vituko na matukio Mengi sana ya kichawi ..Nikipata nafasi nitakuwa natupia kimoja baada ya Kingine ili watu waweze kujua
Nashauri hii stori Ndalichako angeifanya ndyo mbadala wa ile ya Sadiki na Chitemo maana Stori Ya Sadiki na chitemo isha xpire
 
Haya ndio mambo tunayo yataka mkuu ..shusha nondo na Mimi badae nitashusha zangu..

Kuhusu kukwepa ajali inasemekana ndio zindiko lililo msaidia Zitto mwaka 2008 kwenye ajali ya Salome Mbatia..
Nawaoneni watani zangu watu wa KG
 
walikuuwa wewe?
peleka hekaya zako huko kwenu bisheke
na bado utatokwa povu vibaya Kilimanjaro ndio role modal ya maendeleo tz
ninyi mpo maskini kwasababu mnapigana mAjungu na kuoneana wivu wa kipuuz kwa hali hiyo ni sahihi KBS kagera kuwa ya tatu kwa umaskini
ishozi ni pa kAwaida
wewe ushafika marangu,himo,mwika,sanya,machame,bomangombe?
Wachagga kila siku nawaona huku Ludewa wanafuata uganga...Wachagaa sasa hivi ndio wanaongoza kutoa kafara ndugu zao ili wapate mali
 
u
pamoja na hivyo, bado watu wa mkoa wa kilimanjaro wana unafuu sana na masuala ya imani za kishirikina ukilinganisha na watz wa mikoa mengine.

mikoa ya huku kwetu imani ya ushirikana ipo juu sana.

kuna mwaka fulani baba yangu alitaka kuwajengea wazazi wake nyumba ya kisasa huko kijijini kwao songea.

bibi alimkataza kwa kuhofia kwamba kama baba angefanya hivyo, baadhi ya wazee wa kile kijiji wasingefurahi.

baba yangu angeuliwa kichawi kwa kosa la kuwajengea wazazi wake nyumba ya kisasa.

baba hakujari, akawajengea wazazi wake nyumba ya kisasa pale kijijini na mpaka leo ipo na wala hakupatwa na jambo lolote.

visa kama hivi huwezi kuvisikia uchagani, ndio maana ukitembelea vijiji vya mkoa wa kilimanjaro unakutana na majumba makubwa ya kisasa ambayo watoto wamewajengea wazazi wao.
Wachagga walipata bahati ya wakoloni kuweka makazi yao kilimanjaro kwa sababu ya hal ya hewa iliwavutia ukichanganya na mlima kilimanjaro...wakoloni wakajenga shule wachaga wakabahatika kupata elimu na wachaga hawakuwapa wakoloni upinzani waliwakaribisha na kuwanyenyekea.sehemu nyingine wakoloni walipata upinzani hawakuweza kukaa muda mref, mfano songea vita vya maji maji.....wachaga kuwa na maendeleo ni kutokana na usaliti wao wa kuwakaribisha wakoloni nao wakawajengea shule wakabahatika kupata elimu na kazi serikali na sekta binafsi...sio kama wachaga wana akili sana hakuna kukosa kwao uzalendo na muwakaribisha wakoloni kumewasaidia
 
basi sawa.
 
Back
Top Bottom