Juma Nkamia ampinga Rais Magufuli kuhusu miaka 7 ya Urais

Juma Nkamia ampinga Rais Magufuli kuhusu miaka 7 ya Urais

Nakuunga mkono.
Huyu mtu ni mchochezi kweli kweli.

Dunia nzima kuna vita na vurugu kwenye nchi ambazo viongozi wake wamejiongezea muda wa kukaa madarakani.

Na hili liko wazi sana.
Vurugu zote kwenye nchi maskini zinatokana na uroho wa viongozi au wapambe wao kutaka wakae muda mrefu madarakani.

Huyu Mbunge anataka kuliingiza taifa kwenye mjadala usio na tija.
Kuna mambo mengi sana ya kushughulikia sio muda wa kukaa madarakani.

Kama mtu anapenda kukaa muda mrefu madarakani basi atafute kazi nyingine lakini sio siasa.

Ni kweli siasa inatumia fedha nyingi sana lakini ndio msingi wa utawala bora unaofuata sheria tuliojiwekea na pia uwajibikaji unaongezeka.

Masuala mazima ya utawala ,bunge,ulinzi mahakama n.k. ni masuala yenye gharama kubwa sana katika nchi yoyote duniani.
Utawala na bunge tumeyawekea muda wa miaka 5 yawe yanafanyiwa uchaguzi ili wananchi wapime viongozi na wabunge wao kama wametekeleza yale waliyoahidi.

Kukwepa gharama kati haya masuala yanayogusa amani ya nchi ni sawa na kulea jipu.
Hatutaki kukaa na viongozi mpaka tuwachoke bali tunataka tuwape muda wa ama kuendelea au kukaa pembeni kwa sababu ya uwajibikaji wao.
Uchaguzi unasimamiwa na watanzania wenyewe ambao ndio walipa kodi kwa hiyo suala la uchaguzi pia linawanufaisha watanzania kupata fedha na mzunguko wa fedha kuongezeka kwa kutokana na ajira za muda ama za kudumu za wasimamizi wa uchaguzi.

Tumuunge mkono rais na kumpuuza Mkamia na walioko nyuma yake wanaotaka kuliingiza taifa kwenye migogoro ya kisiasa.
Kuna vijana wengi wa vyama vyote wanaosubiri 2020 ili wajaribu bahati yao ya kupata hiyo ajira ya ubunge na udiwani waboreshe maisha yao na hao wakina Mkamia wastaafu mana wamesha kule mpaka uwaziri. Kama hawajajipanga basi wasubiri kuona wale UVCCM na BAVICHA wakichukua majimbo 2020 na wazee waliochoka wakae pembeni.

Hili vijana walipinge kwa nguvu zote bila kujali vyama mana linawaumiza wao huku wale wanaolipigania wakiwa wameshashiba vya kutosha.

Kiongozi mwadilifu kabisa hawezi kung"ang"ania madarakani hata siku moja.
Anataka kuwagawa wananchi kwenye hili bila sababu za msingi ili kututoa kwenye ajenda yetu kuu ya ujenzi wa nchi ya viwanda. Ashindwe na alegee. Kama kuna kuna mtu anataka kukaa kwa muda mrefu asubiri wananchi wamrudishe kwa kura kama anafaa kurudishwa tena jimboni, wananchi hawajapewa nguvu ya kumuondosha madarakani kiongozi wakati wowote kama hawafai, hivyo wasilazimishwe kwa nguvu kuongozwa miaka 7 na kiongozi wasiempenda. Tusubiri kwanza katiba itamke namna wananchi watavyoweza kumtoa madarakani kiongozi. Wakati wowote kama hawafai
 
Nimependa hii comment ya jamaa huko FB
185fab011ea780ed1a923b07df3e0b87.jpg
 
nkamia ni kilaza tu...
Kuna kipindi alikua anasoma UDOM pale ndipo nilipo shuhudia upimbi wake.
Hawa machalii wa CCM niwakuwachukua makofi tu.
Kuwakumbusha kila wanapo jisahau.
 
Wadau najiuliza Kwanini CCM haijamkemea Mbunge Nkamia Kwa kuendeleza MJADALA WA Urais LICHA ya Rais ambaye ni Mwenyekiti Wa CCM kukataa?
 
HANA TAKWIMU. ATWAMBIE HIZO TAKWIMU KAZITOA WAPI? NA JE WAPIGA KURA WAKE ANEWAULIZA AU WAMENTUMA?, HAWA NDIO WANATUFANYA TUTUKANWE NA TRUMP.
ANGALIENI WENYEWE WANGAPI HUMU NDANI WANAUNGA MKONO HUU UPUUZI
 
Mpango ushasetiwa tayari hii ndio namna ya kuuleta nkamia katumika tu Hivi Kuna mwana CCM anaweza mpinga Dr wazi wazi namna hii
Mara sifurahishwi
Mara spika
Mara wazee wa ndiooo
Mara kura za maoni
Mara ushindi wa kishindo
Umesahau maandamano makubwa ya kumshinikiza Rais akubali ombi la wanyonge.
Huyu Nkamia sio wa kupuuza wala kuchukulia kijuujuu
 
Jamani nauliza hivi ile mahakama ya mafisadi ipo mkoa gani hapa Tanzania? Kuna mjomba wangu ni fisadi nataka nimpeleke uko
 
Jamani nauliza hivi ile mahakama ya mafisadi ipo mkoa gani hapa Tanzania? Kuna mjomba wangu ni fisadi nataka nimpeleke uko
 
Huyu mbunge anafahamu kuwa kuna watu wengi sana wataudhika kwa kubadilisha Katiba ili kuwaongezea watu akiwemo yeye muda wa kubaki madarakani. Huu ni uchochezi sawa na uchochezi mwingine.

Hivi kama siku Tanzania tutapata Rais na bunge linalohusudu ufisadi, rushwa, kuuza twiga, faru, ndovu na kushabikia biashara ya dawa za kulevya kwa miaka 14 mfururizo kama Nkamia anavyotaka iwe itakuwaje? Tumkemee Nkamia kwakuwa hakuna utafiti unaoonyesha kuwa umaskini wetu ulisababishwa na uchaguzi wa kila miaka 5 na namna kuchaguana kila baada ya miaka 7 kutakavyopandisha uchumi wetu.

Danganya toto
 
Katika taarifa ya habari ya BBC jioni hii amesikika Mhe.Juma Nkamia amempiinga waziwaazi Rais Magufuli kuhusiiana na hoja ya kutaka kuongezewa muda wa Urahisi toka miaka 5 mpaka miiaka 7!



Nkamia amesema atawasiliiana na Spika kuona namna atakavowasillisha hoja yake hiyo!

Pamoja na Rais Magufulii kuwatangazia Watz kupitia K/Mwenezi Bw. Polepole kuwa JPM hafurahishwi na mjadala huo wa kutaka aongezewe muda!!!!

Hoja ya Ngamia haina mashko anapodai ati Serkali inatummiia mabiilionii kwenye chaguzi kiila baada ya miaka 5!!! Ngamiia ni mnafiikii na hana adabu!!!Watz wangelimwelewa angelihoji kuhsu chaguzi ndogo za marudiio zinazokula mabiliionii kwa uzembe tu........!!!

Swali ni, Je, nani yuko nyuma ya huu upuuzi anaong'ang'ania Nkamia??Kama Mbunge wa CCM anapingana na Rais na Mwenyekiti wake wa Chama kwanini tusimwite MCHOCHEZI????



Ni lini alipata kuwa na akili timamu!!!?
 
Umesahau maandamano makubwa ya kumshinikiza Rais akubali ombi la wanyonge.
Huyu Nkamia sio wa kupuuza wala kuchukulia kijuujuu
Nionyeshe rafiki zako ili nami nikuambia wewe ni mtu wa aina gani
 
Back
Top Bottom