Tatizo labda ni uchama, eidha yeye amelitoa Wazo kichama ama wanaompinga nao wako kichama ama amewajibu kichama. Siasa za vyama vingi Tz ni sumu ya kufikiri.
Lakini hii hoja ina mantiki sana, kwa taifa changa kiuchumi kama letu, na kwa yaliyo tukia 2015 kwa mfano kiuchumi, kuna mantiki kubwa kwa vipindi vya uchaguzi kuongezwa, tena si saba bali kumi kabisa kwa awamu moja na iwe kwa awamu mbili.
Bendera, magari, mizunguko, matangazo, vipeperushi, muda nknk vyote ni mali tena in cash, makampuni, watu, wanalipwa. Fedha ambazo zingekidhi baadhi ya majukumu ya msingi ya kitaifa, Mfano elimu, afya, maji, kilimo nknk.
Dar ilifurika mabendera, vipeperushi na maujinga kibao, yote ni kwa kipindi kifupi tu cha mpito wa uchaguzi, kwanza zile ni hela, lakini pia sisi si matajiri wa kutumia fedha kijinga vile. Leo tunalia uchumi na huduma ni mbovu, hatuwazi ni kiasi cha shilingi ngapi chaguzi zetu, kwa ujumla wake ugharimu.
Fikiria hali ilivyo kwa sasa, nchi inapigania kujikwamua ktk hili wimbi, majukumu ni mengi, muda ni mchache, fedha ama vipato ni vichache, urasimu ni mwingi, ila miaka miwili ijayo, taifa liache yote, lijikite tena kwenye uchaguzi. Kama 2015 ama zaidi ya pale, hela itumike tena kivile, ni ujinga. Hata ni kama familia yako binafsi, usingependa ipitiwe na ujinga huu, mzee au wewe kila baada ya miaka mitano, unapoteza mamilioni kugombea udiwani ama ubunge,kihasara: kila baada ya miaka mitano tu! Duh! Nadhani hata mke na watoto wangekushauri vinginevyo, taifa ni zaidi ya familia.
Inawezekana, amelitoa kisiasa, au amezijibu hoja kisiasa, au ameulizwa maswali kisiasa, ama amejibiwa kisiasa, ila hoja ina MASHIKO SANA.