Juma Nkamia ampinga Rais Magufuli kuhusu miaka 7 ya Urais

Kamwe hakuna anayekataa muda wa uongozi kuongezwa
 
katumwa na yuleyule mzee wa jiuzulu ugombee tena eti kuonesha si yeye aliyemtuma..
nani anaweza kumpinga pombe akabaki mtaani salama..
yule mkurugenzi kule kagera aliambiwa wewe unanijibu mimi hivyo ?
yakamkuta..
nkamia asingekua ametumwa kesho ungesikia avuliwa uanachama kwa kumpinga mwenyekiti..
 
Nkamia ametoa maoni yake.
Mh Magufuli ameshatoa msimamo wake kuwa hapendelei mjadala huo ni vema tukaheshimu msimamo wa kiongozi wetu.
Hata hivyo najua watanzania wengi wangependa atawale muda mrefu zaidi ili adumishe yale mazuri anayoyafanya.
Ulizunguka Tanzania nzima kukusanya maoni? Au unawasemea tu watanzañia?
 
Huyu ana mawazo mgando!!!! Anadhani Tanzania ni yeye.
 
Hapo kuna mambo mawili yanayomsukuma mwanahabari Nkamia kutaka jambo hilo.
Mosi ni kujipendekeza kwa Rais ili nae aonwe kwenye teuzi. Alikwisha wahi kuonja tamu ya teuzi kama NW wa Habari, sasa anajaribu kujipendekeza ili awamu hii nayo imuone.
Pili, huenda hana hakika ya kupata tena Ubunge ktk uchaguzi ujao, na anaona miaka inakimbia faster, so anaona kama watacheza karata vizuri wataongeza miaka miwili mbele ya posho na mishahara ya kiutukufu.
Nafikiri cha kubadili kwenye uchaguzi kiwe ni kumzuia kiongozi wa kuchaguliwa atayejivua nafasi yake bila sababu za msingi kugombea tena nafasi hiyo kwa miaka hiyo saba anayosema yeye.
Nampongeza Rais Magufuli kwa kufunga mjadala huu.
 
Kwa kweli sikubaliani na Nkamia na hoja yake ya kuongeza muda kutoka miaka5 kwenda 7 lakini bado anayohaki ya hoja yake kusikilizwa na kukataliwa kidemocrasia si kwa amri ya raisi. Nkamia katika hoja yake hasemi kwamba magufuli aengezewe muda ila anataka katiba ibadilishwe ili kipindi cha uraisi kiwe miaka7.
 

Wewe mwite mchochezi, kwani nani amekukataza?
 
This issue is very well planned, tusubiri baba Jesca aingie kipindi cha pili 2020 ndipo mtaona nguvu ya hii hoja, kwa Sasa anaona watu watamtosa kwny uchaguzi mkuu ujao ila jamaa hana mpango wa kuachia madaraka kamwe!
 
Ndio pale yule anjiita King kimzahamzaha tu anakua raisi halafu anatawala 14 years
 
Tatizo lile jamaa la pale juu linapenda sana vitu vya aina hiyo pia liongoliongoo..Jamaa katumwa kimkakati na ndiyo maana hata NIPASHE wametumbuliwa kwa habari ya kijinga kabisa! Kimkakati zaidi.
 
Halafu wanamchukia Trump kwa maneno yake, nkamia is a good example na wale wanaomtuma
 
This issue is very well planned, tusubiri baba Jesca aingie kipindi cha pili 2020 ndipo mtaona nguvu ya hii hoja, kwa Sasa anaona watu watamtosa kwny uchaguzi mkuu ujao ila jamaa hana mpango wa kuachia madaraka kamwe!
Hakuna wa kuachia hapo,hii kitu planned, hadi jirani kaja,we subiri 25
 
Nkamia ametoa maoni yake.
Mh Magufuli ameshatoa msimamo wake kuwa hapendelei mjadala huo ni vema tukaheshimu msimamo wa kiongozi wetu.
Hata hivyo najua watanzania wengi wangependa atawale muda mrefu zaidi ili adumishe yale mazuri anayoyafanya.
We mzee mimi naomba unitoe katika hao watanzania wengi, Usinijumuishe kwenye vitu visivyo na maana!
 
Hakuna wa kuachia hapo,hii kitu planned, hadi jirani kaja,we subiri 25
Hahaha tena jm amekanusha siku moja kabla ya Kagame kutua nchini, what a coincidence??

Ila tusiombe iwe hivyo aisee, huyu mzee ataipeleka nchi kusikojulikana
 
Hiyo hoja jana alisema rais hupatikana kwa kupitia chekeche nyingi ikiwemo watu wa usalama, hivyo hakuna uwezekano wa kupata rais mbaya. Kama hivyo ndivyo huko mbele si watafuta ukomo kabisa?
 
Kuna kitu kimefichwa au kipo nyuma ya pazia, Mkamia mkienda ktk jimbo lake ni aibu tupu, badala ya kuja na muswada wa kusaidia maeneo ya vijijini yeye anakuja na issue ambayo haina maslahi hata chembe kwa Wa Tz. Poleni sana wananchi wa Chemba, 2020 fanyeni mabadiliko yenye tija kwenu.
 

Mbona kila siku wako busy kununua wapinzani na kufanya uchaguzi au hiyo siyo gharama??Upuuzi mwingine ni wa kuuchoma moto tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…