Huyu mbunge anafahamu kuwa kuna watu wengi sana wataudhika kwa kubadilisha Katiba ili kuwaongezea watu akiwemo yeye muda wa kubaki madarakani. Huu ni uchochezi sawa na uchochezi mwingine.
Hivi kama siku Tanzania tutapata Rais na bunge linalohusudu ufisadi, rushwa, kuuza twiga, faru, ndovu na kushabikia biashara ya dawa za kulevya kwa miaka 14 mfururizo kama Nkamia anavyotaka iwe itakuwaje? Tumkemee Nkamia kwakuwa hakuna utafiti unaoonyesha kuwa umaskini wetu ulisababishwa na uchaguzi wa kila miaka 5 na namna kuchaguana kila baada ya miaka 7 kutakavyopandisha uchumi wetu.