Hata Nyerere hakujua kuwa iko siku Tanzania itakuja kumpata Rais ambaye ataliua Azimio lake la Arusha, atauza mashirika yote, viwanda vyote na nyumba zote za umma. Hakujua kwamba Tanzania itakujakumpata Rais ambaye atauza tembo wote, faru wote, twiga wote, tanzanite zote, dhahabu zote kwa bei cheee kabisa. Huyu Nkamia ni hatari kabisa, hajui kuwa iko siku Tanzania inaweza kumpata Rais ambae anaweza kuiuza au kuigawa Kigoma kwenda Burundi, Ngara kwenda Rwanda, Mtwara kwenda Msumbiji, Ruvuma kwenda....Kagera kwenda.... ili apate pesa za kustarehe?