Juma Nkamia ampinga Rais Magufuli kuhusu miaka 7 ya Urais

Nkamia ametoa maoni yake.
Mh Magufuli ameshatoa msimamo wake kuwa hapendelei mjadala huo ni vema tukaheshimu msimamo wa kiongozi wetu.
Hata hivyo najua watanzania wengi wangependa atawale muda mrefu zaidi ili adumishe yale mazuri anayoyafanya.
Shithole
 
ushauri mzuri sana
 
Mkiwa na viongozi wa aina ya Nkamia apa Africa ni bora mkatawaliwa tena na wazungu!
Jamani Watanzania wenzangu!! Kuliko kupoteza muda kumjadili nkamia, niheri tupoteze muda kumjadiri dr shika, maana unaibu waziri ulimuadhiri kisaikolojia ndg yetu nkamia na ndo maana amekuwa mlopokaji.
 
Trump ajakosea kuwaita watu weusi shimo la choo sasa kama mawazo ya Nkamia unaweza kumlaumu Trump
 
Najaribu kuwaza je kingekua kinyume chake kwamba Rais apunguziwe miaka ya kubaki madarakani iwe angalau nane si angeitwa mchochezi sasa hivi kuongeza miaka sio uchochezi
 
Mheshimiwa Nkamia ni mwanasiasa Mchanga sana hivyo hana uwezo wa kuchanganua mambo kwa mapana na marefu. Hoja anayoishabikia ni hoja nzito inayohitaji mjadara mpana wa kitaifa na siyo ushabiki wa kisiasa ambayo ndiyo nguvu kubwa anayoitegemea huyu mheshimiwa. Namshauri a withdraw hii hoja kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.
 
Hata akitaka awe wa maisha kama majirani zake ni poa tu! Kama kweli alimaanisha kile alichokisema basi amwite waziri wa katiba na sheria na yule wa bunge na katibu wa bunge na spika waizuie hoja hiyo isifike bungeni na huyo mbunge aonywe na chama chake! Tofauti na hapo basi naamini wanacheza na akili zetu na hisia zetu jambo ambalo ni hatari kwa demokrasia yetu. Mwl. Nyerere alilitabiri hili kabla ya kufariki!
 
Tatizo la nchi hii ni moja, wachochezi wanaachwa huru, wasiowachochezi wanasingiziwa kuchochea.
Nkamia anachokifanya ni uchochezi
 
Hajampinga, ni mipango. Hatukubali katiba iheshimiwe, miaka 5 mitano kama katiba inavyoagiza.
 
Tukisema katumwa tunapigwa ban. Hivi lile dudu ni la kulibishia lilivyo na roho mbaya?
 
Nkamia Kama anataka iwe hivyo,ahamie Rwanda.
 
Mzalendo2015, Hoja ya Mh. Nkamia haimuhusu JPM hata kidogo wala CCM ni maoni na mtazamo wa MH. NKAMIA MWENYEWE- Katiba yetu na haki ya asili (natural rights) inampa Mh. Nkamia fursa hiyo- sasa WEWE NI NANI wa kumzuia mtu kutumia fursa aliyopewa na Mungu wake kuitumia?
 
Nkamia Kama anataka iwe hivyo,ahamie Rwanda.
Rwanda mbali -CHADEMA PANATOSHA MAANA MH. MBOWE YUPO JUZI, JANA, LEO, KESHO, NA MILELE SEMA AMENNNNNNNNNNNNNNNNN
 
Wapendwa hakuna haja ya kutoa lugha chafu.
Wapo watanzania wengi wanaovutiwa na utendaji kazi wa Mh Magufuli hususani utetezi wa Rasilimali zetu na kupambana na ufisadi. Naamini hayo ndiyo yanayowasukuma watu wengi hata kufikiria kumuongezea muda wa kukaa madarakani.
 
Tafadhali
 
Akija mbaya apunguziwe muda.......saafi saana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…