Deo Corleone
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 17,006
- 13,281
Hili jamaa ni disgrace kwa mpira hapa duniani, Msimu uliopita alifungiwa mechi 10 kwa kosa hilo hilo.
Leo karudia tena.
=============================
=============================
Leo karudia tena.
=============================
=============================
Chanzo; BoiPlus Blog
BEKI kisiki wa Mbeya City Juma Nyoso aliwahi kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumfanyia vitendo vya udhalilishaji aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Elius Maguri.
Baada ya adhabu hiyo jamii ya wanamichezo iliamini kuwa Nyoso amejifunza kitu na kwavile alijitokeza kumtaka radhi Maguri basi ilitarajiwa asingerudia tena kutenda kosa hilo.
Jioni ya leo katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom kati ya Azam na Mbeya City Nyoso amethibitisha utukutu wake na kwamba ile ya kwanza haikuwa kwa bahati mbaya. Kwa mara nyingine amerudia kufanya kitendo kile cha udhalilishaji na safari hii akimfanyia mshambuliaji wa Azam John Bocco.
Kitendo hicho kimenaswa na kamera zilizokuwepo uwanjani hapo na ni matumaini ya wapenda soka kuwa TFF itachukua hatua kali zaidi za kisheria kwa Nyoso ili iwe fundisho kwake na kwa wachezaji wengine ambao wanafanya vitendo hivi.