Juma Nyoso amdhalilisha John Bocco

Juma Nyoso amdhalilisha John Bocco

Status
Not open for further replies.

Deo Corleone

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2011
Posts
17,006
Reaction score
13,281
Hili jamaa ni disgrace kwa mpira hapa duniani, Msimu uliopita alifungiwa mechi 10 kwa kosa hilo hilo.

Leo karudia tena.

=============================
=============================

attachment.php


BEKI kisiki wa Mbeya City Juma Nyoso aliwahi kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumfanyia vitendo vya udhalilishaji aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Elius Maguri.

Baada ya adhabu hiyo jamii ya wanamichezo iliamini kuwa Nyoso amejifunza kitu na kwavile alijitokeza kumtaka radhi Maguri basi ilitarajiwa asingerudia tena kutenda kosa hilo.

Jioni ya leo katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom kati ya Azam na Mbeya City Nyoso amethibitisha utukutu wake na kwamba ile ya kwanza haikuwa kwa bahati mbaya. Kwa mara nyingine amerudia kufanya kitendo kile cha udhalilishaji na safari hii akimfanyia mshambuliaji wa Azam John Bocco.

Kitendo hicho kimenaswa na kamera zilizokuwepo uwanjani hapo na ni matumaini ya wapenda soka kuwa TFF itachukua hatua kali zaidi za kisheria kwa Nyoso ili iwe fundisho kwake na kwa wachezaji wengine ambao wanafanya vitendo hivi.
Chanzo; BoiPlus Blog
 

Attachments

  • IMG-20150927-WA0001.jpg
    IMG-20150927-WA0001.jpg
    101.3 KB · Views: 6,552
huyu jamaa kufungiwa maisha ni haki yake.. Hafai kabisa kucheza Ligi Kuu.. arudi tu kucheza ndondo.
 
Naskia nimeitwa ...ati nyoso kafanyaje...adhabu yake afungiwe mechi 50 au arudishwe kwa wauni wenzake msimbazi
 
Hivi huyu jamaa huwa anajifikiriaje! kiukweli ni jambo la kukera na kuudhi, huko nikumdhalilisha mwenzie, hakianani kama ndo mie uwanjani patachimbika, naomba tukemee na kuisambaza sehemu nyingi picha hii kukemea upuzi huu
 
Hakika si tabia njema michezoni na mahali pengine popote kwani ni kitendo kidhalilishacho uanaume wa mtu...

Lakini kuna jambo moja huwa lanitatiza, hao wanaume wanaodhalilishwa mbona huwa wapo kimya tu hata hatujawahi kuona wakianzisha hata zogo?

Hivi kweli mwanaume rijali uguswe kalio halafu upotezee tu hivi hivi....mmmh!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom