Juma Nyosso amekamatwa na Polisi baada ya kumpiga shabiki hadi kuzimia

Juma Nyosso amekamatwa na Polisi baada ya kumpiga shabiki hadi kuzimia

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso amekamatwa na Polisi baada ya kumpiga shabiki hadi kuzimia baada ya mchezo wa Kagera Sugar vs Simba uliyomalizika kwa Simba kupata ushindi wa magoli 2-0 mjini Kagera

========

Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso amejikuta akitiwa mbaroni na polisi mjini Bukoba kwa madai ya kumtwanga shabiki ngumi mara baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Kagera Sugar kupigwa 2-0 na Simba SC kwenye dimba la Kaitaba.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya mpira kumalizika wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo (dressing-room) ambapo inadaiwa kuwa baadhi ya mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Kagera Sugar wakawa wanawarushia maneno makali (matusi) wachezaji hao.

Kufuatia maneno hayo, Nyosso alionekana kukosa uvumilivu na kuamua kumtwanga ngumi mmoja wa mashabiki hao ambaye alizimia papo hapo.

Gari ya wagonjwa (ambulance) ilifika na kumchukua majeruhi na kumkimbiza hospitali na dakika chache baadaye polisi walikwenda kumchukua Nyosso na kwenda naye kituo cha polisi.

Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitafuata baadaye

Chanzo: Azam Tv

Nyoso2.jpg


Nyoso1.jpg
 
de5ea211b02c336d47b134de09572bc8.jpg
Mchezaji wa Kagera Sugar Juma Nyosso ashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kutuhumiwa kumpiga Shabiki mmoja uwanjani mpaka kupoteza fahamu.

Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara VPL kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba Sports Club.
 
Kwani hajaacha mchezo wake mpaka leo shauri yake[emoji13]
 
Huyu jamaa akili yake siyo nzuri. Nadhani mpira si sehemu yake
 
Machungu ya kufungwa

Huyo aende tu akanyee debe gerezani mpira hauwezi..alianza kushika wanaume wenzie kwenye makalio sasa anapiga watu
 
Machungu ya kufungwa

Huyo aende tu akanyee debe gerezani mpira hauwezi..alianza kushika wanaume wenzie kwenye makalio sasa anapiga watu
Kwann atukanwe na kukashifiwa na huyo shabiki bwege ww ungekubali?
 
Huyu jamaa anamajanga mara ashike watu makalio mara azimishe watu
 
Alafu eti Tanzania ipige hatua kisoka, wachezaji kama hawa ndo wapeleke mpira mbele?? Tff piga ban maisha huyu
 
Huyo shabiki aliyetikiswa chuma kimoja akazimia hope atakuwa mdada in case akawa mwanaume basi wanaBukoba itabidi mkae kama kamati mumchunguze kweli ni wa huko?asijekuwa mwanaume wa Dar Nyosso alimchukulia demu akaona ampandie bus kwenda kumtukana kwenye hadhira ya watu ili kikiwaka apate watetezi
 
Huyo shabiki amepigwa alikuwa wapi,tuache kukurupuka hivi shabiki mjinga je amemfuata jukuani au shabiki aliingia uwanjani?
 
Mashabiki wa simba ni mambumbumbu ..

Hongera nyosso umemkosa nyosso umempata shabiki wa simba ,nilitaka kushangaa nyosso awaache simba salama?
Mkuu rudia kusoma. Aliyepigwa ni shabiki wa kagera suger na siyo shabiki wa simba. Acha kukurupuka
 
Back
Top Bottom