Juma Nyosso amekamatwa na Polisi baada ya kumpiga shabiki hadi kuzimia

Mkuu rudia kusoma. Aliyepigwa ni shabiki wa kagera suger na siyo shabiki wa simba. Acha kukurupuka
wewe ndo uache kuwa kama bendera. Huoni huyo shabiki kavaa jezi nyekundu tena ya simba
 
Ngumi moja mtu chali ? Maisha haya sasa hivi ni kukaa mbali na watu wachokozi unaweza ukapata murder case bure
 
Dah ilikua ngumi jiwe hiyo hadi mtu kuzima!Ila Nyosso bana anazingua mno..si angevumilia tu ona anavyojiharibia.Chonde wasije wakampa adhabu ya kutokucheza maisha.
 
Uyo ni shabiki wa simba tena wa Dar
Nyosso wasikuzoee hao mikia
 
Kupiga mshabiki inawezekana ila hiyo picha ya pili mbona kama haioani na tukio.

Mpira umekwisha hawa watu hapo chini mbona wamekaa kama vile mechi inaendelea nilidhani ningaliwaona wakiwa wimawima kwenye harakati za kuondoka uwanjani!!
 
Kupiga mshabiki inawezekana ila hiyo picha ya pili mbona kama haioani na tukio.

Mpira umekwisha hawa watu hapo chini mbona wamekaa kama vile mechi inaendelea nilidhani ningaliwaona wakiwa wimawima kwenye harakati za kuondoka uwanjani!!
Kuna utata kidogo. Ila wasema shabiki aliingia uwanjani punde tu mpira kwisha.
 
Mashabiki wa Simba wanaushabiki wa kishamba sana, kwa nini wamzomee Nyoso!.
 
Mashabiki wa simba ni mambumbumbu ..

Hongera nyosso umemkosa Bocco umempata shabiki wa simba ,nilitaka kushangaa nyosso awaache simba salama?
Usisome "heading" tu bali soma habari yote
 
Huyu jamaa sasa akatafute kazi nyingine tu, kipaji bila nidhamu ni bure.

Unaacha kazi inayokuletea ugali mezani unahangaika na shabiki anayepiga mayowe yake akichoka anaenda kulala kwake huko.
 
Ila washabiki wanaboa, inasemekana huyo shabiki ni wa Simba na alienda akampulizia vuvuzela Nyosso tena usoni, ebu imajini mmefungwa alafu jamaa anakuja kukupigia makelele usoni na vuvuzela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…