Unaambiwa mifumo ya ulinzi ya hiyo nyumba ya Bakresa imeunganishwa moja kwa moja na mifumo ya usalama ya CIA huko Langley, Virginia USA... Kukitokea hata mwanga anapita usiku kutaka kumloga Mzee Bakresa basi lazima alarm iite kwenye simu ya mkurugenzi mkuu wa CIA, ambapo yeye huziamrisha ndege za kivita zisizo na rubani (drones) kuwa tayari kwa lolote. Hizo ndege huwa zimepaki pwani ya Afrika Mashariki maalum kwa kumlinda Bakresa... kilichonishangaza ni ule mfumo wa ulinzi unaoweza kunusa hatari kupitia joto la mwili na mapigo ya moyo kwa yeyote mwenye nia mbaya ndani ya nyumba ya mzee. Mtaalamu wa ulinzi alisema waliweka huo mfumo kudhibiti udokozi