Jumla ya ada ya kusoma degree ya udaktari katika chuo kikuu cha Kairuki kwa miaka yote mitano ni milioni 32, swali langu is it worth it ?

Vipi umeyawaza maisha/uhai ambao unaokolewa na hao madaktari?, umewaza thamani ya uhai wa mtu?. Thamani ya hiyo taaluma haipo kwa mtaaluma pekee bali jamii na taifa.

Dhumuni la elimu ni kuikomboa jamii sio kuwa tajiri mbinafsi. Haina maana kuwa tajiri na afya mbovu au kuwa tajiri na jamii yako ni hohehahe.
 
Serikali ingelipia 100% ya gharama za masomo kwa watu wa afya . Serikali ndiyo inapaswa kuonyesha kujali.
Ukilipa ada na gharama zingine mwenyewe hapo maana yake unawekeza Ili uvune zaidi ya ulichowekeza.
Utumie mamilioni uje kuambulia mshahara wa laki 6 private au milioni 1 serikalini.
Binafsi siwezi huo ujinga
 
wakati hiyo ni ada ya mwaka mmmoja vyuo vya maana US na Canada

u cant quantify elimu mkuu
 
Madaktari mje kutupa muongozo DR Mambo Jambo
Sijajua Worth it anamaanisha Nini?
Kwamba Elimu atakayopata Ni nzuri au Elimu ni mbovu hapo kairuki..

Kwa Uelewa wangu Mdogo chuo.cha Kairuki ni chuo Cha private Tanzania Chenye Ada Ndogo kuliko vyote katika maswala.ya Udaktari..

Udaktari Ni wito kutoka Ndani..
Investiment ya Udaktari kwa daktari mmoja Ni kubwa kuliko Mshahra wake..

Daktari sio Mshahara daktari ni Moyo wa Huruma Compassion within...

Hata kama Una knowledge kubwa ya Udaktari lakini ukawa una ukatiri Bado utakuwa ni Muuaji uliyejivika Vazi la Proffesionalism..

Kwa mfano Mwingine ili kumaliza Udaktari lazma uwe na Si chini ya 40Milion
Na bado kwa wale watakaoamua kwenda residents (Kusomea ubingwa) ni zaidi ya hizo tuseme uwe na 60Milion..

Ila mshahara wa Dakatri bingwa Ni hauzidi 2.5mil kwa mwezi basic salary..

Na bado mambo yakienda vibaya Atapata Lawama na laana kwa panxe zote mbili serkali na Jamii..

Udaktari ni wito..
Ukiona mtu anaulizia Benefit kwenye kusoma Udaktri Hafai kuwa Daktari hata kwa kunusa tu
 
duh kumbe mshahara wa daktari bingwa ndo mdogo hivyo??? Mi nlkuwa naskia wanalipwa 8M+
 
Hoja nzuri hii mkuu maana vijana wanaingia kusaka elimu chuoni kichwani wakiwaza mshahara na ndio maana wanaangalia ela iliyotumika vs manufaa yatakayopatikana in term of cash. Other benefit ambazo hazionekani Kwa macho kwao haiwahusu.

Anyway, endeleeni kuielewesha jamii ipo siku tutasogea
 
Wabongo kwa kulialia tu
Kuna jamaa yangu january hii kampeleka mwanae kidato cha kwanza pale hela school karibu nanabii. Ile ada inalipwa pale ni yakibabe ukilinganisha na hii ya huyu dr mtarajiwa hapa.
 
Ukisomea udaktari lenga eneo ambalo unajua kuna uhitaji. We unaenda somea udaktari wa kutoa dawa kitu ambacho kwa sasa hata watu wa pharmacy wanafanya?

Yaani ni ile mgonjwa kaja, anakuelezea anajisikiaje hali yake, then unamsikiliza na kurejea dalili za magonjwa hayo na kumuandalia karatasi ya kwenda nayo maabara kwaajiri ya vipimo kisha akuletee ripoti ya maabara ambayo itaamua utoe dawa ipi na ipi.

Sasa hiyo kazi na utitiri wa madaktari wa hivyo plus pharmacy, zilivyojaa hapa mjini ndio utegemee kulipwa milioni na zaidi?

Somea magonjwa ya watoto, wanawake wajawazito, magonjwa ya upasuaji mbali mbali, magonjwa ya uzeeni hapo sasa ndipo utaweza kupata mapato.
 
It is worth it elimu ni gharama mkuu
 
Si ndo maana mnapewa gredi za juu kuliko vyuo vingine vya taaluma yenu .. ilhali walimu wanatoka kwenye hivyo vyuo vingine...

Natamani takwimu za ufaulu wa mtihani wa mct ziwekwe hapa kwa vyuo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…