Kitu pekee ninachokijua kwa elimu ya bongo upande wa afya ni ndoto nyingi za wanafunzi kuwa madaktari huzimwa na competence ya ufaulu kidato Cha sita Ili mtu afinikiwe kwenda chuo chenye gharama nafuu ambavyo vyote ni vya serikali kama MUHAS, UDOM, UDSM (tawi la medicine lipo mbeya nafikiri) Hawa ada zao at least zipo chin kwa sababu wanagharamikiwa na serikali sehemu kubwa ila kupata nafasi ya kusoma inabidi uwe na ufaulu mkubwa Sana, (kwa miaka ya hivi karibuni) ada za private ni kubwa kidogo ila baadhi ya vyuo kiukweli ni kubwa mno mfano Kampala na Kairuki japo kitaaluma sioni tofauti na sie wengine tena si ajabu tumewazidi, wengi wanapenda hivyo vyuo wanatoka familia zenye uwezo na wengine hawategemei mkopo ambao kwa serikali mkopo asilimia mia upande wa afya tuition fee ni 3100000, sijui kama wameshabadilisha gharama inayobaki unaongezea mwenyewe., Kwa sababu ya gharama hzo na wengine kukosa mkopo wanaachana na kozi ya udaktari na kutafuta kozi zingine ambazo siyo malengo yao, kupata hivyo vyuo vyenye gharama kubwa vigezo vyao siyo vikubwa ukilinganisha na vyuo kama MUHAS, UDOM, UDSM, ni pesa ndio Ina mater.