Mtu mwenye uwezo atafanya patent hata 40, anaweza kukosa 39, akapata moja tu, na hiyo moja ikazibeba zote hizo 49.
Halafu hizo hela si lazima utie wewe, wewe unakuja na the right idea tu, kuna watu wanakuwa nanhela zao wanatafuta idea nzuri ya ku invest. Ndivyo watu smart wanavyofanya dunia hii, hao matajiri wite kina Google kina Elon Musk ndivyo waliavyonza hivyo. Sisi hatujachangamkia fursa katika kutambua vipaji na kuvipa support, kwa njia ya investment. Watu wana hela kibao, halafu wote wanagezana kwenye biashara. Wakati tuna matatizo kibao yanahitaji ufumbuzi, tuna watu kibao wanaweza kuja na ufumbuzi hawana funding tu.
Ndiyo watu smart wanavyofanya ma billionaire wote ma venture capitalists wanaoanzisha startups za dunia huwa wanafanya hivyo.
Jamaa aliyeanzisha Uber alipewa dola milioni 100, akawa kama anazimaliza bila results, akamuendea venture capitalist aliyempa hela akifadhaika sana kwamba kapoteza hizo dola milioni 100. Akitegemea atakaripiwa. Yule venture capitalists akamwambia kuwa ni kawaida sana kwa wazo zuri la biashara kushindwa mara ya kwanza, ila kama bado anaamini ni wazo zuri, ajipange kimkakati upya tu, fedha zitakuwepo tu.
Baadaye akafanikiwa Uber ikashika chati dunia nzima.
Tatizo kwetu tuna umasikini mkubwa, umasikini si wa hela tu, bali hata wa fikra.
Na umasikini huu unakuja na a very low tolerance for initial failure. Yani tuna woga mkubwa sana wa risk. Na hii ni moja ya sababu hatuendelei. Kwa sababu maendeleo yanataka kukubali risk, yanataka uweze kufanya patents 39 zifeli zote na uwe na uwezo wa kufanya ya 40 ambayo itakutoa.
Kwetu hatuna mentality hiyo, hatuna uthubutu huo, na si kwamba nawalaumu sana. Naelezea tu mambo yalivyo. Naelewa kwa nini mambo yako hivyo.
Ni vigumu sana kuwa na high tolerance ya initial failure katika jamii ambayo ina umasikini mkubwa na margin of error yake ni ndogo sana.
Yani huko kwetu ukikosea kidogo tu unabwengwa unatukanwa unatupwa.
Angalia hata watoto wanavyocheza ni hivyo hivyo. Mtoto akicheza kwenye matope akichafua nguo kidogo tu anatukanwa, anapigawa, anakatazwa.
Wenzetu mtoto akijichafua kwenye matope mzazi anamwambia "Oooh, Johnny, why are you so naughty?. Look, you are bringing mud into the house. Are you exploring your creative skills? What did you make today, a castle?". Mzazi anaweka nguo kwenye washing mashine maisha yanaendelea.
Sisi mtoto atachapwa hapo mpaka akome, na hatujui pengine mtoto alikuwa anajifunza na kujenga interest ya kuwa architect udongoni, na tunapomchapa ndiyo tunamuondolea interest yake hiyo.
Na hata huko kwenye patents ni hivyo hivyo, one mistake, you are out.
Sasa uvumbuzi hautaki hiyo approach.
Ndiyo maana kila siku tunalalamika, kwa nini Waafrika hawavumbui kitu?