John Gregory
JF-Expert Member
- Jul 14, 2019
- 1,137
- 2,147
Huu utaratibu wa waumini wa kanisa katoliki kukutana kila Jumamosi kwa ajili ya taratibu zao za Jumuiya nadhani linapaswa kuigwa na liwe jambo la kila Mtanzania.Jumuiya hizi hujengwa na familia kadhaa zisizopungua tano hadi kumi na tano zilizo jirani.Familia hizi hushirikiana katika mambo yote ikiwa ni pamoja na kusali pamoja,kusoma na kushirikishana katika kutafakari Neno la Mungu, kufarijiana,kulea watoto,kusaidia wenye shida,kupanga maendeleo yao,nk.
Mbali na faida za kiimani wanazopata waumini hao kwa kusali pale wanapokutana, Hilo nisingependa kulizungumzia sana, Lakini pia kuna manufaa mengine ya kijamii.
1- Ni chachu ya ushirikiano na umoja kwa wanajamii.
2- Ni sehemu ya kufarijiana na kusaidiana katika changamoto mbalimbali kama za kiafya nk.
3- Husaidia kulea vijana na watoto katika miito na maadili sahihi ili kuwa watumishi bora kwa jamii na taifa.
4- Sehemu rahisi ambayo kila mwanajamii anaweza kutoa maoni, ushauri na mapendekezo yanayohusu masuala mbalimbali.
5- Hutumika kutatua migogoro mbalimbali kama ya wanandoa kwa utaratibu sahihi.
6- Inakuza imani na maadili kwa familia (kaya); hasa baba, mama, watoto na ndugu wanaoishi pamoja wakishiriki kikamilifu.
7- Jumuiya hutoa misaada mbalimbali kwa jamii inayoizunguka.
8- Pia, jumuiya hutumika kujengana kiroho kwa kurekebishana pale mmoja anapoyumba kimaadili.
Kwa hayo machache, nadhani kukutana mara kwa mara, hususan kwa majirani au wanajamii kwa ujumla, Kuzungumza mambo kadhaa, mfano changamoto kadhaa zilizopo katika jamii, kutambulisha wageni, kujuliana hali, kusaidiana katika changamoto na shida mbalimbali kama maradhi, magonjwa nk. ni jambo jema, Ikishindikana kukutana mara moja kwa wiki, basi angalau kila mwezi au kila baada ya muda fulani kwa utaratibu maalum ambao jamii itajiwekea.