Jumuiya kama za Kikatoliki zinapaswa kuigwa na jamii zote na taifa kiujumla

Jumuiya kama za Kikatoliki zinapaswa kuigwa na jamii zote na taifa kiujumla

Sasa inakuaje tena madhehebu mengi yameiga huo utaratibu kutoka kwa Wakatoliki manake huku mtaani sikuhz tunaona Anglican,KKKT,TAG,Walokole n.k na wenyewe wanafanya jumuiya hasa siku ya Jumamosi asubuhi.
Utaratibu wa jumuiya haujaletwa na wakatoliki ulikuwepo tangu muda. Kuna channel ya wale Marabi wa kiebrania sijui kiyunani aliulizwa tena na mtanzania wakati wapo Israel akaifafanua. Labda hoja iwe kuifanya jumamosi asubuhi.😂😂 Shotocan ameiweka kiprotestant tu
 
Tunazungumzia kwa context ya hapa Tanzania lipo wazi kwamba Wakatoliki ndio walianzisha huu utaratibu wa kusali Jumuiya hasa siku ya Jumamosi asubuhi na makanisa mengi yalikua yanawadhihaki Wakatoliki kuhusu huu utaratibu sasa cha kushangaza sikuhz na yenyewe yameiga huu utaratibu wa Jumuiya huku mtaani.
 
Rudia kusoma kule juu mvutano wao umebase wapi? Sahwah eeh
 
Soma Biblia wewe hayo ya sala ya nyumba kwa nyumba za jumuiya yalianza kipindi cha mitume uwe unasoma Biblia sio tu kushindia misale ya waaumini na kusikiliza padre tu au unacholishwa matango pori seminary

Tatizo wakatoliki hamsomi Biblia ndio masna huwa mnaamini kanisa la Kikristo lilianzia Roma Italia mnasahau kuwa Kristo mwanzillishi wa Ukristo alizaliwa Israel sio Roma Italia mnalishwa ujinga

Ukiristo ulianzishwa uyahudi na Kristo mwenyewe anayeitwa Kristo sio Petro au yeyote

Ukristo ulianza uyahudi na Kristo ndio maana tunaitwa wakristo wafuasi qa Kristo myahudi wa uyahudi sio wa Petro wafuasi wa Petro papa wa kwanza wa wa Roman Catholic wabaojitia kanisa la kwanza lilianzia Roma kwa Petro

Sisi hatuhiji Roma na hatuna mpango tunatambua kanisa la kwanza lilianzishwa Uyahudi na Kristo mwenyewe alipozaiwa,kuhubiri kuteswa ,kufa na kufufuka

Hilo kanisa lenu mnaita la kwanza aliloanzisha Petro bakini nalo wenyewe na utapeli wenu

Kanisa la kwanza mwanzilshi Kristo hakuna cha Petro ,wakoritntho wala nani

Ni Yesu Kristo tu
Mkuu utaenda Mashariki,Magharibi,Kusini na Kaskazini kutaka kuwabeza Wakatoliki hautaweza kamwe.Hiyo imani uliyinayo chanzo chake ni Biblia iliyokusanywa na kuundwa na Wakatoliki.Vyovyote vile utakavyoamini na kujifanya mjuaji lkn kama unajiita Mkristo basi kuna athari ya Ukatoliki ndani yako.
 
Sasa inakuaje tena madhehebu mengi yameiga huo utaratibu kutoka kwa Wakatoliki manake huku mtaani sikuhz tunaona Anglican,KKKT,TAG,Walokole n.k na wenyewe wanafanya jumuiya hasa siku ya Jumamosi asubuhi.
Nao sababu ni hiyo hiyo. Watu wanapoanzisha dini wanabuni na mikakati ya kupata waumini endelevu na wakiwapata kuna mbinu za kuwakoleza zaidi ili iwe ngumu kutoroka
 
View attachment 3129561
Huu utaratibu wa waumini wa kanisa katoliki kukutana kila Jumamosi kwa ajili ya taratibu zao za Jumuiya nadhani linapaswa kuigwa na liwe jambo la kila Mtanzania.Jumuiya hizi hujengwa na familia kadhaa zisizopungua tano hadi kumi na tano zilizo jirani.Familia hizi hushirikiana katika mambo yote ikiwa ni pamoja na kusali pamoja,kusoma na kushirikishana katika kutafakari Neno la Mungu, kufarijiana,kulea watoto,kusaidia wenye shida,kupanga maendeleo yao,nk.

Mbali na faida za kiimani wanazopata waumini hao kwa kusali pale wanapokutana, Hilo nisingependa kulizungumzia sana, Lakini pia kuna manufaa mengine ya kijamii.

1- Ni chachu ya ushirikiano na umoja kwa wanajamii.

2- Ni sehemu ya kufarijiana na kusaidiana katika changamoto mbalimbali kama za kiafya nk.

3- Husaidia kulea vijana na watoto katika miito na maadili sahihi ili kuwa watumishi bora kwa jamii na taifa.

4- Sehemu rahisi ambayo kila mwanajamii anaweza kutoa maoni, ushauri na mapendekezo yanayohusu masuala mbalimbali.

5- Hutumika kutatua migogoro mbalimbali kama ya wanandoa kwa utaratibu sahihi.

6- Inakuza imani na maadili kwa familia (kaya); hasa baba, mama, watoto na ndugu wanaoishi pamoja wakishiriki kikamilifu.

7- Jumuiya hutoa misaada mbalimbali kwa jamii inayoizunguka.

8- Pia, jumuiya hutumika kujengana kiroho kwa kurekebishana pale mmoja anapoyumba kimaadili.

Kwa hayo machache, nadhani kukutana mara kwa mara, hususan kwa majirani au wanajamii kwa ujumla, Kuzungumza mambo kadhaa, mfano changamoto kadhaa zilizopo katika jamii, kutambulisha wageni, kujuliana hali, kusaidiana katika changamoto na shida mbalimbali kama maradhi, magonjwa nk. ni jambo jema, Ikishindikana kukutana mara moja kwa wiki, basi angalau kila mwezi au kila baada ya muda fulani kwa utaratibu maalum ambao jamii itajiwekea.
Kamwambie Kagame.
 
Back
Top Bottom