Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Leo na kesho kutakuwa na mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki huko Arusha. Kwa mtazamo wangu mkutano huo ni wa upotevu wa muda, fedha za wananchi kwani hakuna lolote la maana linajadiliwa na kufikia hatua ya utekelezaji.
Mengi ya makubaliano ya jumuiya hii huishia kwenye makabati, huku kila nchi ikifanya kwa ubinafsi. Jumuiya hii ya Afrika Mashariki ilikuwa na ufanisi wakati wa utawala wa mzungu, lakini sisi waafrika kwenye hili tumekwama.
Ushauri wangu kwa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki, acheni kupoteza muda na fedha za wananchi kwa mikutano isiyo na tija.