wameongeza Sudan, Congo, Burundi, Rwanda wakati ya awali ilikuwa haijawa integrated vizuri
Jumuiya za maana kama EU hawaongezi wanachama hovyo hovyo tu
Wamekwenda kukutana na kula pesa za wavuja jasho tu.Leo na kesho kutakuwa na mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki huko Arusha. Kwa mtazamo wangu mkutano huo ni wa upotevu wa muda, fedha za wananchi kwani hakuna lolote la maana linajadiliwa na kufikia hatua ya utekelezaji.
Mengi ya makubaliano ya jumuiya hii huishia kwenye makabati, huku kila nchi ikifanya kwa ubinafsi. Jumuiya hii ya Afrika Mashariki ilikuwa na ufanisi wakati wa utawala wa mzungu, lakini sisi waafrika kwenye hili tumekwama.
Ushauri wangu kwa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki, acheni kupoteza muda na fedha za wananchi kwa mikutano isiyo na tija.
Majumuia yote ya afrika hakuna hata moja lenye nguvu. Wako kwa ajiri ya kutengeneza ajira za watoto wao na wajomba zao kwenye hizo ofisi. Au na SADEC hadi leo wameshindwa kutoa msaada japo kidogo tu kule Cabo Delgado Msumbiji ambapo Magaidi wanasumbua karubu mwaka wa tano sasa.Naunga mkono hoja!
Kati ya jumuiya za hovyo duniani hii inaongoza!
Toka mdogo naskia tu mara sarafu ya pamoja, mara shirikisho la kisiasa, mara umoja wa forodha.. mara kiswahili nininini sjui lakn hadi leo haieleweki utekelezaji zaidi ya kula pesa tu
🤣🤣🤣Somalia on the way to join
Dah!Leo na kesho kutakuwa na mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki huko Arusha. Kwa mtazamo wangu mkutano huo ni wa upotevu wa muda, fedha za wananchi kwani hakuna lolote la maana linajadiliwa na kufikia hatua ya utekelezaji.
Mengi ya makubaliano ya jumuiya hii huishia kwenye makabati, huku kila nchi ikifanya kwa ubinafsi. Jumuiya hii ya Afrika Mashariki ilikuwa na ufanisi wakati wa utawala wa mzungu, lakini sisi waafrika kwenye hili tumekwama.
Ushauri wangu kwa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki, acheni kupoteza muda na fedha za wananchi kwa mikutano isiyo na tija.
Dah!
Hii ni mada nzito kweli, lakini nimebaki tu nikitoa kicheko; hasa kuhusu huyo "mzungu"!
Tukiondoa hilo la mzungu, ninakubaliana nawe moja kwa moja. Angalia viongozi waliopo kwenye kundi hilo, akina M7, Kagame, Samia...
Hawa ni viongozi wa kutegemewa kuleta mabadiliko ya maana katika jumuia kama hii? Kenyatta, anaondoka, lakini hakuwa na faida yoyote katika malengo ya kuleta maendeleo, mbali ya kuiona Kenya kuwa ndiye baba na mama wa ukanda mzima; kwa hiyo walitarajia manufaa zaidi ya wengine wote katika jumuia.
Sasa watamkaribisha Somalia!
Kazi yao kwisha.
Wanaungana ukubwa wa kieneo, lakini tabia zinabaki za kinchi binafsi. Ukipita mipakani maofisa wa nchi hizo hawajui hata umoja ni nini, na unafanyaje kazi! Umebaki ni umoja wa viongozi, nao uko midomoni na kwenye mikutano zaidi.
Kuna hiyo porojo ya sarafu ya pamoja ni muda sasa, lakini haianzi wala dalili! Kuna ushuru wa forodha ni porojo kama porojo nyingine. Kwa sasa ni rahisi kufanya biashara na nchi za ulaya, Amerika na Asia kuliko baina ya Afrika mashariki. Ili jumuiya hiyo iwe na tija ni lazima isimamiwe na mzungu na sio zaidi ya hapo.

Ngoja nikufahamishe kwa nini ipo hivyo kama hujalifikiria hili.Wanapanuka kwa ukubwa wa kijiografia, lakini makubaliano ya msingi hayatekelezwi. Na upanukaji mkubwa ni wa nchi zilizo desparate na vita.