Uchaguzi 2020 Jumuiya ya Madola yatoa taarifa rasmi kusikitishwa na yaliyotokea Tanzania kipindi cha uchaguzi mkuu ikiwemo udanganyifu na mauaji

Uchaguzi 2020 Jumuiya ya Madola yatoa taarifa rasmi kusikitishwa na yaliyotokea Tanzania kipindi cha uchaguzi mkuu ikiwemo udanganyifu na mauaji

Zile plate namba za un na sabaya plus kauli ya ocd we ushindi za nn sasa.
 
Kwa ajili hiyo mnamlipa huyo Muzungu Mamilioni ya US Dollars? kupata tu hayo matamko? Mnafikiri mtamtisha mtu na matamko? Hizo fedha mngewekeza kwenye uchaguzi angalau hata mngekaribia kura alizopata Lowasa.

Low IQ !
Bora hata wangefikiria kupanga ofisi yenye hadhi kubwa kidogo kuliko ufipa kwa baba mkwe wa mwenyekiti maana wazo la kujenga hawana.
 
Mkuu, unakijua kiingereza kweli? Au unadhani Commonwealth ni jina la mtu?
Wewe ndo huelewi kiswahili, kasema mnamlipa huyo mzungu kwa sababu aliyeyotoa tamko ni mzungu anaitwa Patricia Scotland, tatizo mnaweweseka na kipigo.
 
Haya sasa kumekucha...saivi kila info ni tamko kuhusu uchaguzi uliofanyika Tanzania.

Hii ni Taasisi kubwa sana duniani imeripoti hili.

Nina uhakika kwenye haya matamko, Magufuli hataachwa salama na ushindi wake wa kidhalimu.
Bado unategemea mabeberu
 
2/3 ya wapiga kura hawakujitokeza kwenye huo ushenzi uitwao uchaguzi. Na bado kwenye hiyo 1/3 hamkupata kura zote. Sina tatizo la Lisu kushindwa iwapo angeshindwa kwa uhalali. Sio kwa hizo kura zilizokuwa zinasambazwa na vyombo vya dola. Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Yaani hata kama mh. Magufuli angepata kura moja wengine wakapata sifuri bado ndiye mshindi kwa mujibu wa sheria za nchi.



MAGUFULI4LIFE.
 
“However, I am deeply concerned by reports alleging serious incidents of violence and electoral malpractice. I urge the relevant authorities to transparently and expeditiously conduct the necessary investigations and ensure the rule of law, justice and accountability prevails, in order to maintain the people of Tanzania’s confidence in democracy.
Hivi hizo relevant authorities wanazozisii ni zipi kiasi kwamba sio ndio hizo hizo zilizochafua uchaguzi kwa mujibu wa taarifa yao?
 
Hivi hizo relevant authorities wanazozisii ni zipi kiasi kwamba sio ndio hizo hizo zilizochafua uchaguzi kwa mujibu wa taarifa yao?
Those guys are clearly playing their own pre-planned game. Ila ngoma yao imebuma alfajiri-alfajiri tu. Hawakutegemea surprise kubwa kiasi hicho kutoka kwa wananchi wazalendo. They underestimated the level of awareness of our people kuhusu ghiliba yao ya kumtumia mamluki wao ili aturudishe kulekule kwenye mikono yao ya unyonyaji wa rasilimali zetu. Huyu Mzungu wao hajaanza juzi kuimba ngonjera zake za "Tutashtakiwa! Tutashtakiwa!" Sasa angoje kesi zake tu, maana mpango wake wa kuivuruga nchi umekatishwa na kufika mwisho.
 
The peace loving people of Tanzania greatly appreciate your concern and that of the people of the Commonwealth. We thank you for your concern and also support your call for concerned parties in the just ended GE in Tanzania to be as impartial as possibly when reporting on General Election matters and avoiding accusing and pointing fingers on one or any participating parties in the just ended General Election in Tanzania.
 
Haki gani unataka wewe? Uchaguzi umefanyika kwa uhuru na haki hakuna mtz yoyote aliyekatazwa kupiga kura na kura zote zimehesabiwa kwenye kituo mbele ya mawakala wa vyama vilivyoweka wakala na mshindi akaonyeshwa hapo hapo kwenye kituo. Sasa wewe unayesema uchaguzi haukuwa huru na haki leta ushahidi siyo kulialia tu kama mtoto mdogo!
Uchaguzi huu kwa kweli hatukuiba kama chaguzi zilizopita, tumefanya ujambazi tukamaliza kabisa. Waliofanya hili akili zao ndogo kama za mende na wanatuhalibia chama chetu kikongwe
 
Uchaguzi huu kwa kweli hatukuiba kama chaguzi zilizopita, tumefanya ujambazi tukamaliza kabisa. Waliofanya hili akili zao ndogo kama za mende na wanatuhalibia chama chetu kikongwe
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana.
 
Hai Mbowe ameshindwa ndiyo maana anahangaika na Dar kama wananchi wangekuwa wamemchagua Mbowe wangekuwa wako barabarani mkuu!

Tuseme tu ukweli Wapinzani wameshindwa vibaya sana na sababu kubwa ni Lissu kuside na beberu Robert Amsterdam. Watz huwa hawapendi sana mabeberu ambayo yako kwa ajili ya Rasilimali zetu.
Walioshinda hawana sababu ya kutumia nguvu kubwa kuzuia habari.
 
View attachment 1618126View attachment 1618125

My Take
Pamoja na ukweli wa mambo yasiyo ya kawaida,ila ndugu zetu wa damu jumuia za Afrika zinasema mambo yalikuwa shwari.
Waswahili walisema "Waarabu wa Pemba, hujuana kwa vilemba".

Waafrika wenzetu wanajua ikifika zamu yao kuiba viongozi wa Tanzania watawatetea pia.

Wewe mtu kama Uhuru Kenyatta kawaambia wapinzani wake, kama yeye anaiba kura, na wao si waibe tu.

Sasa unategemea mtu kama huyo ataukemea wizi wa kura Tanzania?
 
Back
Top Bottom