Jusa amvulia kofia Tundu Lissu

Jusa amvulia kofia Tundu Lissu

Mughwira

Senior Member
Joined
Jun 10, 2008
Posts
109
Reaction score
34
Jusa ambaye alipewa nafasi ya kipekee na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Pandu Kificho kutoa mchango wake kuunga mkono hoja ya Rasmi ya Kanuni alisema; Kwa namna ya pekee tunamshukuru mjumbe mwenzetu kwa mchango mkubwa na uelewa na utundu wake katika kusoma mambo mbalimbali yahusuyo sheria, kanuni na kuziweka kwenye matendo, kwa kweli ametoa mchango mkubwa sana wa ubunifu na utayarisha bora wa hii kanuni...

Hongera Lissu na wajumbe wenzio kwa mchango wenu kwa Taifa hili. Mungu awabariki.
 
Kikwete mwenyewe anamwelewa vizuri sana.

Lisu peke yake ni sawa na wabunge mia mbili wa ccm.!
 
Ni kweli Mh. Jusa ni Gentleman hana unafiki na zaidi kukiri kuwa Mh. Lissu ameisaidia kamati ya Prof. Costa Mahalu.
 
Ukweli husimama hata kama utaudhuia bali ipo siku ndiyo itakuwa ndiyo, anastahili pongezi T. Lisu.
 
Ccm hawaupendi huu ukweli! Lkn ilikua Ni jambo zuri kwa taifa kujivunia Kua Na watu Km Hawa bila kujali itikadi za kisiasa!

Mfano tuko na Mh Lipumba, Huyu mtu amefanya kz mpk nje ktk taaluma yake ya uchumi! Ni vzr sn kwa taifa kuwatumia watu Km Hawa ktk kujenga taifa sio kuwaterekeza!

Binafsi nathamini sn watu wote wenye nia njema Na wanaotumia ujuzi wao mkubwa kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla!
 
hongeras Jussa. penye ukweli sema tu
 
Hmm...siku hizi huyo Lissu mnamsifia utadhani ni bonge la genius wakati majuzi tu hapa mlikuwa mnadhihaki.

Unaweza tuu ukatoa dhihaka kwa habari ambayo huna uhakika nayo nafikiri Mh. Jusa amejiridhisha ndio maana ameamua kuwa mkweli.
 
Lissu ni jembe na Kikwete ana siri kubwa kuhusu Lissu kuliko wana-ccm wafuata upepo. Aliwahi kutoa kauli pale singida mwaka 2010 kuwa, ni heri Slaa awe rais kuliko TL kuwa mbunge.
Ila lissu awe makini na sifa anazopewa.
 
Pia kuna Dr Akson na Mh Costa Mahalu na kwa ujumla ile kamati yote wamefanya sehemu kubwa!

Tuwashukuru kwa Hilo!
 
Jusa hataki unafiki wa kusubiri mtu afe eti ndo utoe mijisifa kwa marehemu
Taratibu CUF wanatakuwa na wakati mgumu sana wa kuchagua upande..Jussa na wengize si walidhani Lissue haipendi Zenj, sasa watahitaji reconcialte ktk akili zao watakapokuja jua kuwa kupitia kwa Lissu ndipo watafikia malengo ambayo walikuwa wakiyaota.Yaani ufafanuzi makini na sheria zilizoonyooka bila kinyongo ili wazenj wapewe serikali inayoeleweka na bara pia na ya kitaifa km Federal government.
 
Naona Leo mnamsifia JUSSA kwa sababu kamsifia Lissu, vijana wa CHADEMA mnabadilika kutokana na mazingira.
yes, watu makini wanasemaga 'we have neither a permanent friend nor permanent enemy, but a permanent interest'
mtu aweza kuwa adui yako au rafiki yako irimradi atimize matakwa yako.

sio kwamba vijana wa chadema wanabadilika kutokana na mazingira, ila wanafuata kanuni hiyo hao juu.
 
Naona Leo mnamsifia JUSSA kwa sababu kamsifia Lissu, vijana wa CHADEMA mnabadilika kutokana na mazingira.

Jussa alikuwa anamsikia Lissu kwenye magazeti kama walivyo wengine; mara hii amepata nafasi ya kufanya naye kazi kwa siku 21 ndio maana amenena hayo. Inatufunza kutokuwa waropokaji kwa jambo/ au mtu usiyemjua kiundani.
 
Ccm hawaupendi huu ukweli! Lkn ilikua Ni jambo zuri kwa taifa kujivunia Kua Na watu Km Hawa bila kujali itikadi za kisiasa!

Mfano tuko na Mh Lipumba, Huyu mtu amefanya kz mpk nje ktk taaluma yake ya uchumi! Ni vzr sn kwa taifa kuwatumia watu Km Hawa ktk kujenga taifa sio kuwaterekeza!

Hapo kwenye Bold ulitaka kusema nini!?

Issue ya Lipumba, kuna watanzania zaidi ya 20,000 wapo nje ya nchi wanafanya kazi za kitaluuma! Wala usifikiri kuwa Prof. Lipumba ni exceptional sana..wapo watu wanafanya kazi huko nje miaka nenda rudi, tatizo kwa vile Lipumba yupo kwenye siasa na hazimsaidii!
 
Back
Top Bottom