Juventus Special Thread

Juventus Special Thread

BTW Ntuzu naomba umtakie heri Mourinho kazaliwa leo ndo maana ana raha zote za dunia ukizingatia na Juve wamempa furaha kwanini asicheke, daddy Aleyn uwe unaona tag basi kuna kazi jana nimekupa umetekeleza?

Happy birthday Mkuu Mourinho nakutakia maisha marefu Na yenye furaha Na amani.

Mungu akubariki Kiongozi.
 
Last edited by a moderator:
Ona oyaoya mwingine huyu hata unachokiandika hujui halafu unataka battle na mabudula, huyo kilikuu kazaliwa Brazil ikichukua kombe la dunia kule America, Juventus ya yule nguli aliyeenda kufundisha team ya kina Ntuzu ilichukua kombe lini?
Haya njoo ufute hizi kamasi kabla watu hawajaziona

Mara ya mwisho ilikuwa '96 almost 19yrs ago. Sema sasa
 
Last edited by a moderator:
Hoja yangu mamito ni kwamba second leg bado haijachzwa. Ikichezwa Na tukapata matokeo Yake hapo tutaweza kusema.

Dalili ya mvua ni mawingu atacheza vizuri sana game ijayo we unafikiri na wao hawamtaki mwali? Tena wakichukua itakuwa ni bonge la mafanikio kwao mwaka huu wamedhamiria kuvunja rekodi, wacha wairudishe wairudishe Italy kwenye ulimwengu wa soka, #ForzaJuve
 
Ni kweli Italy km imepotea vile. J2 niliona game ya ac Milan nilibaki nasikitika tu. Milan hii sio ile ya buruda Ancelloti. Yani imekufa kabisa.
 
Teh teh teh, naona kijana bado ana mawenge ya shughuli ya jana mpaka kasahau nyakati.
Leo media yote inamponda mchezaji ghali duniani kwa kuvurunda jana, wamemuandama kijana wa watu bure bila kuelewa ya kuwa hakuwa na cha kufanya mbele ya Chiellini
Niliwauliza juzi hawa kina Salamander kwa nini Khedira hapati namba wakanijibu kisiaasa, sasa jana wakatuletea yule kichwa maji Ramos kwenye Midfield ya Arturo, Marchisio na St.Pirlo, akaishia kurukaruka tu kama kabanwa na mkojo, Vidal katawala dimba kama anacheza na mji mpwapwa vile
Sebuleni kwa Madrid huwa tuna historia ya kupeleka dhahma pale, Del Pierro alishasujudiwa kwa makofi na vigelegele siku tunamtwaa mwali pale, wiki ijayo itakua zamu ya Andrea

ancelloti amekiri kama pirlo aliwavuruga sana pale kati kwani jinsi alivyokuwa akicheza alisababisha viungo wake waache sana nafasi hivyo juve kuwa huru kushambulia.....halafu uzuri pale olympic stadion tuna upepeo napo (tushaingia fainali mechi ya marudiano ni kukamiisha ratiba) kwani mwaka 2006 mafundi wetu watatu wakiwa na Italy ndo walipobebea ndoo ya dunia....
 
Na Pirlo mwenyewe hakuwa na match fitness na bado kawagalagaza mbayaa
Ile fainali ilikua na mafundi wetu wengi sana kwa pande zote mbili, safari hii tutakua na kibarua cha kuwapiga gwara Messi and co
 
morata mwenyewe kaongea, two goals for real madrid is nothing, naona wakatalunia wamefulahii, bt namnukuu kaka angu salamander "game bado ipo half time na juve anaongoza 2-1" lets stay tune anything can hapen
#halaa_madrid
 
Back
Top Bottom