Juventus Special Thread

Bitter rivalry btn Bianconeri na Viola? Me naona ni Viola ndio wanatuchukia tena sana probably kuliko team yoyote, wao ndio viongozi wa kutuita majina mabaya, mara watuite wezi. Unakumbuka mwaka flani hivi Zoff aliitwa mwizi na beki wa Viola akiwa kwenye mahojiano na TV?
Na lile saga la Baggio labla nalo liliongezea chuki zao juu yetu, lakini Viola sio wapinzani wetu kamwe, ni vile tu wanatuchukia sana ndio maana majuventin hatupendi kufungwa na hivi vijamaa
Me team sizipendi ni Napoli na wale washenzi wa mjini, Roma na Lazio ila Napoli zaidi, upinzani na Inter ni kama umepoa imebaki historia tu, hawa Viola wana wivu wa kike tu na sisi dawa yao tunayo
 
Last edited by a moderator:
Mmeiona hii wakulungwa? juve2012, Gang Chomba Belo, gutierez, Ziroseventytwo #Majuventini na #Mabuluda
 
Dortmund 0 Juventus 3...Carlos Tevez dk ya 3 na dk ya 79,Alvaro Moratta dk ya 70. Aggregate 5-1!@mourinho did you expected this?
 
Dortmund 0 Juventus 3...Carlos Tevez dk ya 3 na dk ya 79,Alvaro Moratta dk ya 70. Aggregate 5-1!@mourinho did you expected this?

Nilitegemea ushindi ila c mkubwa kiasi hiki. Hii juve hii ina kila dalili za kuendelea kufanya vizuri.
 
Nilitegemea ushindi ila c mkubwa kiasi hiki. Hii juve hii ina kila dalili za kuendelea kufanya vizuri.

mie pia nimeshangazwa na jinsi walivyobadilika jana.Juve hawachezi mpira kasi,lakini jana walikuwa wanakimbia sana,goli 2 za counter,kombinenga ya Morata na Tevez ni hatari.
 
mie pia nimeshangazwa na jinsi walivyobadilika jana.Juve hawachezi mpira kasi,lakini jana walikuwa wanakimbia sana,goli 2 za counter,kombinenga ya Morata na Tevez ni hatari.

Draw ya kesho ingefaa sana tupewe timu kutoka ufaransa hasa Monaco. Hapo semi final lazima.
 
Draw ya kesho ingefaa sana tupewe timu kutoka ufaransa hasa Monaco. Hapo semi final lazima.

pweza umeanza mambo yako,kwa hiyo tukienda ligue 1 tunatoboa?haya ngoja tuone ila kumbuka wamemtoa mwingereza hao jamaa si wa kudharau.PSG ndio naiogopa kuliko hata Bayern.
 
Draw ya kesho ingefaa sana tupewe timu kutoka ufaransa hasa Monaco. Hapo semi final lazima.

na Juve akifika Semi tu basi yeyote atakaepangiwa atambaishia...
juve ni timu iliokamilika.
juve ukuta wake unacheza kwa nidhamu ya hali ya juu.
juve kiungo chake kinakaba bila kutegeana.
ukitoa ubishoo wa mtu mweusi Juve hakuna mtu mwenye kujiona yeye ndio yeye, so pasipo yeye hakuna ushindi
...

forza Juve
 
pweza umeanza mambo yako,kwa hiyo tukienda ligue 1 tunatoboa?haya ngoja tuone ila kumbuka wamemtoa mwingereza hao jamaa si wa kudharau.PSG ndio naiogopa kuliko hata Bayern.

teh teh umeitaja PSG umenikumbusha kauli ya Ibrahimovic eti juzi alivocheza ile rafu na kisha wachezaji wa Chelsea kumfuata eti anadai aliona kama kazongwa na vitoto (panya road) kumi na moko....kwi kwi kwi kwiiiiiii
 
juve2012, Ziroseventytwo na shifta, jana mwenzenu nimeshinda mlingotini, kule mapangoni kabisa alikokabidhiwa Mwalimu mwenge wa Uhuru kwa ajili ya zile bao 3 bila majibu.
Nimefurahi sana siku ya jana, hata sikuweza kuingia humu, ntawapa story siku mingine za huko mlingotini

FORZA BIANCONERO
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahahaaaa, Violla bana hawana adabu kabisa, juzi wamemshikisha adabu mtu mzima flan hivi, leo wamewashikisha ukuta wale washenzi wa Roma
 
Hawa Roma wamepatwa na nini? Kuna kitu hakipo sasa pale clubuni kwao. Hii club si imechukuliwa na mwekezaji? Afanye mabadiliko makubwa akichukuwa ushauri kwa watu kama Sacchi, Lippi na kina Cappello. Ovyo kabisa
 
teh teh umeitaja PSG umenikumbusha kauli ya Ibrahimovic eti juzi alivocheza ile rafu na kisha wachezaji wa Chelsea kumfuata eti anadai aliona kama kazongwa na vitoto (panya road) kumi na moko....kwi kwi kwi kwiiiiiii

ha ha ha haa!anaringia zile futi 6 na points kadhaa zake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…