Juventus Special Thread

Tangu Juan Laporta aondoke image ya Barca imeharibika sana (Barca is longer Mes en que) ukiangalia jinsi walivyowatreat kina Abidal,Valdez,Sanchez,Alacantara plus scandal ya Neymar,usajili wa watoto na udhamini wa Qatar.I hope huyu jamaa atarudi kurudisha image ya Barca.Fitina za Spain mchezaji akisajiliwa na Barca watasema Real Madrid walikuwa wanamtaka ,akisajiliwa na Madrid nao watasema Barca walikuwa wanamtaka
 
Ndio hivyo, kuna watu hawana zali tu. Mtu kama Pjanic fundi hatari, Daniele De Rossi mpaka atastaafu ila hapati heshima anayostahili, kina Kondogbia mpaka wanawafundisha mpira waingereza ndio wanaonekana, kuna watu hapo La Liga wanaupiga hatari, kuna dogo anaitwa Beñat alikuwa Betis msimu ulioisha, piga sana mpira, kaishia kuchukuliwa na Athletic club, kina Koke na Arda balaa tupu, watu kama Banega wamekamua hadí wamekuwa bored, yule Brahimi mpaka sasa watu hawajajua uwezo wake vizuri. Hizi timu kubwa zina scouts wanashinda bar tu nadhani, halafu wakiamka wanabeba mwenye jina.
 
Ni balaa tupu, hao kina Rosell walikuwa vichwa mkuki. Hizi za kuchukuliana matonge mdomoni zimeanza zamani sana, nakiri Madrid ndio ilianza kwa Di Stefano, na ndio maana Barca wana machungu mpaka leo, ingawa Madrid wamejitahidi mara kibao kusawazisha hiyo mambo. Cruyff mwenyewe ashakiri hadharani kwamba Barca walichemka kuwaacha watu kama Kroos, James na Isco kwenda Madrid, badala yake wameishia na kina Rakitic ambao walitakiwa kuja Madrid.
 

Anayeing'arisha image ya Barcelona kwa sasa ni Lionel Messi, wangerogwa kumuuza huyu kipindi kile ana msuguano na Enrique basi wangerudi enzi zile za Barca ya 1990's ya kina Overmars, Cocu, captain mkorofi Enrique nk
Laporta pia alikua na uhusiano mzuri sana na Uefa, kipindi cha Guardiola, Barca ilikua inabebwa sana na waamuzi kwenye UCL, nakumbuka ile match ya 1/2 final Vs Chelsea ya Guus Hiddink pale darajani jamaa walivyobebwa ( Ntuzu, Manumbu, Mentor, kalou ) na pia 1/2 yao pale Nou Camp Vs Inter ya Mourinho kuanzia hotelini walikolala Inter mpaka red card ya uongo ya Thiago Motta, so wamrudishe Laporta maana mchango wake huko Barca ni heavy
 
Last edited by a moderator:
Hahaha uliyoongea hapo, wajina wako yule mreno angeyaona angekuwa proud sana. Mpaka kesho nadhani akiskia Barca anaona conspiracies tu.
 
Last edited by a moderator:

Aisee umetaja watu hapo ambao huwa nawafikiria sana, hasa Banega na Brahimi (how old is this guy?) Brahimi machine asee, natamani nimwambie Allegri amchukue huyu jembe
Koke ni kwere man, yaani huwa nashangaa kwanini Pogba anasifiwa hivi na si Koke, maana Pogba kwa Koke ni kama Okocha kwa Zizzou
Pjanic fundi balaa, ukienda Napoli utamkuta dogo Mertens, jembe letu Marchisio huwa hapewi credit kama wale wanyoa viduku, Southampton kuna jembe linaitwa Jose Fonte, mreno huyu hata sijui kama kashawahi vaa jezi ya team ya Taifa, EPL nzima wa kulingana na Fonte ni JT tu, halafu 1 Jose Fonte = 10 Pepes
 
Brahimi 25 tu, still a lot to come from him.

Yule Allegri bana ni mtambo tu(with all due respect), alichemka sana Milan. Na huyo boya ndio alisema Pirlo zilipendwa, akamuachia kimandazi. Juve mpaka walipo sasa wamefika kwa auto-pilot aliyoi-set Conte.
 
Morinho breaking news kutoka kwa trend setters ninaowaamini, zinasema Paris Saint-Germain and Juventus agree €80 million fee for Pogba mchana huu.
 

-Usiseme watu wa Barca huwa wanajiona saints sana ila ni Guardiola.
-Guardiola ni mpuuzi sana, katuharibia mamb mengi sana, katuondolea Toure, eto'o, Helb n.k
-Ndani ya Kipindi chake alifanya ubaguzi mkubwa kwa wasio Wakatalunya.
-Hii timu ingekuwa chini ya Tito Vilanova(RIP) au ingekuwa hata chini Enrique usingetokea upuuzi ule.
 

-Song tumempeleka ili afanye mazoezi kisha arudi.
-Umri kwake sio mbaya.
 
Last edited by a moderator:

Aiseee, huyu James sijui tulikuwa wapi kwa kweli.
 
Angalia msije makarudia kasajili kama ilivyokuwa kwa Tiago,Diego,Felipe Melo na Milos Krasic (new Nedved)

Sijawahi kuamini mpaka leo hii kwamba Diego aligeuka kuwa flop, kajamaa kalikua kanajua sana soccer
Teh teh teh Krasic kama Mateja Kezman tu, lol
 
-Song tumempeleka ili afanye mazoezi kisha arudi.
-Umri kwake sio mbaya.

Acha siasa wewe, arudi kucheza namba ya nani? Buesqest au Rakitic? Naona Gang Chomba anasema miamba ya Milan inamtaka huyo dogo
 
Last edited by a moderator:
Acha siasa wewe, arudi kucheza namba ya nani? Buesqest au Rakitic? Naona Gang Chomba anasema miamba ya Milan inamtaka huyo dogo

Sasa AC Milan si ndo itamfanya hata supersport ya South Africa imsajili. Hawezi kwenda timu ya kishamba yule.
 
Last edited by a moderator:

Hakuna siku nilikasirika kama walivyotuletea Allegri ila kwa sasa niko poa tu, naona jamaa kajirekebisha lakini tutajua vizuri msimu ujao, ana record nzuri sana on his debut seasons halafu huwa yanafuta madudu
Brahimi basi ana future mzuri sana, asibweteke tu hapo Porto, atafute uhamisho kwenda EPL au Spain, akija Italy ni club moja tu ndio itamfaa
Kuna jembe jingine linaitwa Juao Moutinho, huyu ndio proper replacement kama tutamuuza Pogba. Kikwazo ni pesa ya kumpata huyu bwana
 
Sasa AC Milan si ndo itamfanya hata supersport ya South Africa imsajili. Hawezi kwenda timu ya kishamba yule.

Milan wana kibopa mpya mvimba macho mmoja Mr.Nyuki, atawapa mchuzi wa kujenga uwanja na kikosi kipya
 
Sasa AC Milan si ndo itamfanya hata supersport ya South Africa imsajili. Hawezi kwenda timu ya kishamba yule.

Acha dharau,AC Milan itarudi upya.Usije shangaa kusikia Galliani anakuja kumchukua Inniesta au Messi
 
Acha dharau,AC Milan itarudi upya.Usije shangaa kusikia Galliani anakuja kumchukua Inniesta au Messi

Nadhani Galliani apumzike na yeye pamoja na swahiba wake Berlusconi, nafasi yake apewe mtu kama Maldini na kina Seedorf warudishwe kusimamia academy na utafutaji na ukuzaji wa vipaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…