Juventus Special Thread

Juventus Special Thread

One mistake one goal....ukimuacha anafunga ukimuangusha penalt kazi kwako....fair kabisa
 
wengi mnaweka hii still picture kuhalalisha penati ile.je,huo mkono ulimsukuma?huo mkono una kilo ngapi kumuangusha ndani ya impact ambayo haikudumu hata sekunde mbili?mkuu weka moving picture(video) ujiumbue!

Mwalimu wa mabeki wakati anatufundisha japo mimi sikuwa nafasi ya ubeki alikuwa anafundisha ukiwa beki kama mpira upo juu unamfuata mshambuliaji wewe kama beki upo nyuma mshambuliaji yupo mbele,unatakiwa mikono yako uichanue uende kwa kifua yaani mikono iwe wazi kabisaa!kwa sababu kama mkono wako utamgusi mshambuliaji au mchezaji pinzani golini hata kama hutamsukuma kuna wale wanaojifanya kuanguka makusudi kwa kuguswa tu hata bila kusukumwa.kwa hali ile ya jana ni penati hata kama wangeitumia VAR (video assistance referee)pia kwa tukio la jana kwenye mechi ile wengine wanasema kwa dk zile penati haikupaswa.swali je, kwani penati uwanjani imepangwa muda maalum? Mimi nimefuatilia mitandao mbalimbali huko italia baadhi ya waandishi wenyewe wanasema ile ni penati.Tuseme tu ukweli kwa Juventus wao italia wanapendelewa ndivyo wanavyosema baadhi ya mashabiki wa timu pinzani toka lile suala la CalcioPoli.kwa upande wangu mimi Real Madrid kama wananunua marefa basi kwa champion wamezidisha dau.kama uliona sehemu moja kwenye ule ugomvi Giorgio Chiellin alikuwa anamuuliza kwa hasira mchezaji wa Real Madrid "Quanti pagate? Yaani nyinyi munanua kiasi gani" ni hasira tu za jana.Buffon naye alimwambia refa baada ya refa kuonyesha ni penati cha kwanza alimsukuma pili alisema"vai a cacare" yaani nenda kany...).timu za hispania ni matatizo ukianza ile mechi ya chelsea na Barcellona refa alikuwa ovrebo aliwanyima penati chelsea.keita aliushika mpira ndani ya box. Drogba na Ballack walikasirika.na mechi ya old traffod Real madrid ya Mourinho Cuney Cakir alimpa kadi nyekundu Luis Nani. Na mwaka jana Real Madrid na Bayern wote munaikumbuka.mwisho kabisa bila kuisahau mechi ya barcelona na inter milan kuna kiungo wa inter milan ya mourinho alipewa kadi nyekundu kisa Sergio busquets naye alijifanya kaumia huku yupo chini anamchungulia refa kwa jicho moja,alikuwa anagalagala chini kiasi maamuzi akampa mcheza wa inter kadi nyekundu kama sikosei alikuwa tiago motta.
 
IMG_0255.JPG
 
Daaah, jana imedhihirika juventus upande wa kiungo bado tunasafari ndefu sana. Yan jana kwa mara ya kwanza nimeona pjanic akipotezwa Katikati. Yani Alegri jana alipiga mahesabu vibaya sana. Kumuanzisha Howedes kulia alafu Chielini alivyoumia ndio hesabu zikakatamazima, kamrudisha Howedes kati acheze na Benatia, Benatia kaficha sana makosa ya Howedes jana upande wa defence. Anamtoa dyabala anamuingiza Cuadrado wakati timu imezidiwa katikati huku akijua Cuadrado maji kupwa maji kujaa Yan hapa Alegri ali Hedge kabisa. Pale ilibidi aingie bernadeschi tu, Alafu angemtoa Khedira akamuingiza Bentancur ili amsaidie Pjanic kukaba ili pjanic acheze free asikabe kabisa sababu tayari alikua na Kadi ya njano.
 
Scudeto imekua on tena. Juve anamechi ngumu sana zilizobaki, I think mechi ijayo anacheza na Inter then atacheza na Bologna, Roma alafu anamaliza na Verona. Hapa muhimu ni kuwaza mechi na Inter tu. Kuhakikisha timu inashinda iwe uwanjani au nje ya uwanja. Nachofurahi mechi ya mwisho napoli anacheza na kibaraka wetu Crotone alafu anapambana asishuke daraja. Kaeni kwenye TV jamani Lega Calcio mechi hizi za mwisho ipo hot balaa.
 
Dah kocha kazingua sana kumtoa Dybala...ila tusikate tamaa kiongozi wangu...tumebakiza mechi ngapi tutangaze ubingwa?
 
Mechi bado nne kiongozi. Wiki hii tuna mechi na Inter Giuseppe Meaza pale. Baada ya hapo tutacheza na timu anayoshabikia Baba yangu Bologna FC pale ndio kipo Chuo kikuu kikubwa na Kikongwe duniani. Mechi ya tatu tutacheza na watoto wa Papa As Roma, mwisho kabisa tunamaliza na Helas verona. FORZA JUVENTUS. Napoli yy atacheza na Fiorentina, Sampdoria, Torino na Crotone ya Trotta na Madragora.
 
Nashkuru sana kiongozi wangu.

Forza Juvee
 
Ila ufike wakati kocha wa juve aache mapuuza jamani. Mm inanikera sana siku hizi pjanic anapewa Kadi mapema sana alafu anatoka kwenye mchezo. Kama jana Mandzukic aliumia mapema akamlazimisha acheze. Pale ilibidi dyabala aingie. Mapema kipindi cha pili angeingia Bentancur
 
Back
Top Bottom