Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
📌KUTOKA KUIKUTA IKIJENGWA VIPANDE VIWILI, LEO CHINI YA RAIS SAMIA SGR VIPANDE VYOTE 6 VINAJENGWA NA WANANCHI WAMEANZA KUPATA HUDUMA.
Na Bwanku M Bwanku.
Juzi Ijumaa Septemba 11, 2026 kwenye Gazeti namba moja kwa ukongwe Tanzania, Gazeti la Uhuru ukurasa wa 14 kuna makala ya Ndugu Bwanku M Bwanku akichambua mradi mkubwa wa reli ya kisasa (SGR) uliopo Dar es Salaam kupitia Morogoro- Dodoma- Singida- Tabora- Mwanza hadi Kigoma ikitarajia kupasua hadi Congo, Rwanda na Burundi.
Wakati Rais Samia anaingia madarakani, mradi huu mkubwa wa kiuchumi ulikua unatekelezwa vipande viwili tu kutoka Dar hadi Morogoro na Morogoro hadi Makutupora (Dodoma) na vilikua havijakamilika lakini leo chini ya Rais Samia vipande hivi viwili vimekamilika na vimeanza kutoa huduma ya usafirishaji na vipande vingine 4 vinajengwa kutoka Dodoma hadi Mwanza kuelekea Kigoma.
Reli hii inarahisisha usafiri wa umma na kupunguza masaa ya safari kutoka 9 hadi matatu na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi na usafirishaji wa mizigo ukanda mzima wa Afrika Mashariki na maziwa makuu.
Soma sasa Gazeti la Uhuru leo Ijumaa usome makala hii uone Serikali ya Rais Samia inavyoukamilisha mradi huu kwa nguvu kubwa.