Serengeti kuna ile Hotel ya 5 star nadhani mna ifahamu sitaki taja jina maana najua hapo Jamaa zangu watataka nao wakalale so itakuwa nime ipromote na haitakuwa fair kwa hotels nyingine.
Tulienda na Helkopta kuangalia wanyama. Kwa kweli nlitokwa na machozi. Niliona jinsi ambavyo Nyati,Pundamilia etc wanapata shida. Hawali kwa raha. Wanakula huku wana kazi ya kujifukuzia tsetsefly wasiwasumbue. So vijana nawaajiri wanakuwa wanawapepea tu wale kwa raha bila usumbufu.
Nliwaza sana, niliuliza kama wanaruhusu nifanye fumigation mbuga nzima maana kuna Makampuni makubwa Ulaya na Marekani yanapuliza viuatilifu kwa ndege au helkopta. Wale watu wa maliasili wakasema hapana hiyo haitaruhusiwa. Si sawa ki ecolojia.
Sasa hilo suala lilinipa shida akilini maana nikaona ndo maana kuna wanyama wamekonda maana hawana raha kabisa. Fikiria unakula huku unafukuza tsetseflies au unajikuna kupe.
Nimepata wazo. Nimeambiwa kuna madaktari wengi wa mifugo na walimu, wanasheria hapa Tanzania hawana kazi za maana. Mimi nataka nianzishe kampuni kuwapa ajira wawe wana kazi ya kupiga kupe na kupepea/kufukuza tsetseflies kwa hawa wanyama.
Kwa masaa matatu ntalipa usd 3,000 tu kwa kuanzia. Ili nione kama hilo suala lina tija ama sivyo tushauriane tu tusaidiaje hawa wanyama nao waishi kwa amani.
Lengo ni kuwa keep watu busy at the sametime wanasaidia wanyama hawa ambao naona ni kama wanatelekezwa nobody cares about them. Watahitajika vijana walio tayari hata ukiweza kwa saa 1 si mbaya usd 1000 kama utataka kuwasaidia swala,nyati,pundamilia etc unasema.
Lengo ni kuhakikisha hawa wanyama wanastawi na kuishi kwa raha mustarehe.