JWTZ cyber warfare unit

Ulishawahi kuona maonesho ya kijeshi hapo Kigali?
 
Kagame ana kitu gani cha maana ? maana mna mpa sifa sana
 
Huwezi kuwa na jeshi bora bila uwekezaji mkubwa hizo nchi zimewekeza mfano kama USA wizara ya Ulinzi ndo ina budget kubwa kuliko wizara zote na hata mfumo wao wa ajira ni tofauti Tz anaajiriwa Raia asie na vinasaba vya nchi tofauti, ila Usarmy utakuta hadi mchina, mnyakyusa, mkorea yuko ndani ya jeshi lao wao wanazingatia uwezo wa mtu haijalishi asili yake ni wapi lazima jeshi liwe bora.

Kwetu hapa uwekezaji ndani ya jeshi bado mdogo sana, Technology ni 0 maana hata vifaa vinavyotumika vyote ni vya kuletewa vingine hata marekebisho hatuwezi hadi tuombe msaada
 
Wenye akili Hawaoneshi uwezo wao kıvıta!! Mnaonesha silaha nyie serikali dhalimu kuwatisha raia wenu ili wawe waoga mzidi kuwa Tawana kama kondoo .
Hizo zinafanyika sehemu nyingi duniani, sio jambo geni na tanzania sio nchi ya kwanza na pekee kufanya hivyo

Kama raia upo nyuma hivi kufahamu maswala mbalimbali ya kidunia, sasa unashangaa nchi yako kuwa masikini? Au afrika kwann masikini?
 
Ni wazuri sana kwenye show off kipindi cha maadhimisho ya shughuli za kitaifa
 
Wakiondoa hiyo system ya kuajiri, kesho watakuja kutoa tangazo kuombq raia wazaane

Unazani wao wajinga kuwa na sera za namna hiyo huku nchi zingine zikiwa zinapambana raia wao waongezeke?
 
Wakitoe wapi?
Labda kitengo cha kudeki mtaani wakisikia tetesi za maandamano.
 
Huku kwetu Cyber pekee wanaoijua ni kuombana connection za ngono zilizovuja.

Bado wana tactics za kizamani za kuvunja matofali kwa kichwa, wenzetu unakuta kiwete yupo ofisini anafanya maangamizo kwa computer tu.

Vijana wanaosomea mambo ya mitandao wanaishia kuwa watengeneza simu kariakoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…