Kuna hatari moja kubwa sana naiona inakuja Tanzania.
Rwanda na Uganda zinajiimarisha sana kwenye maeneo ya Teknolojia ya kivita na Intelejensia.
Hivi karibuni Rwanda amesaini mkataba wa mashirikiano katika masuala ya Ulinzi na Uturuki. Nchi inayosifika kwa kutengeneza vifaa bora kabisa vya teknolojia mpya za kiulinzi mfano Drones na Makombora mbalimbali. Inasemwa vifaa hivi vimekisaidia sana Jeshi la Rwanda na M23 katika kuziteka Goma na Bukavu huko Congo.
Pia ameingia makubaliano ya Ethiopia katika masuala ya Ulinzi na hivi Karibuni Ethiopia kupitia Uwekezaji wa Kampuni za Ulinzi za Ubelgiji wameanza kutengeneza vifaa bora vya kijeshi vya teknolojia mpya ikiwemo Drones.
kwa utafiti wangu, nchi pekee zinazotengeneza silaha nzuri na za kisasa zinazoweza kupambana na silaha zinazotengenezwa na Mataifa haya ni Israel, Marekani na Uingereza.
Lord denning ninaamini miaka si zaidi ya 30 inayokuja, yanayotokea Congo Mashariki yataanza kutokea mpaka wa Magharibi wa Tanzania hasa mikoa ya Kagera, Kigoma hadi Geita na Shinyanga.
Lord Denning naamini kwa namna mifumo yetu ya kiulinzi na usalama ilivyokuwa compromised na siasa na mapandikizi haitakuwa rahisi sana kwa Tanzania kuweza kupambana na hiyo hatari.
Hivyo ni ushauri wangu kuwa;
1. Kuanzia sasa tuachane na siasa uchwara na kuwaunga mkono Palestina na Iran na tujikite kutengeneza mahusiano mazuri ikiwemo ya mafunzo ya kiulinzi na usalama na Mataifa ya Israel, Marekani na Uingereza
2. Tuwekeze sana kununua teknolojia za kisasa za kivita kutoka Mataifa haya na mafunzo ya umahiri kwa wanajeshi wetu katika teknolojia hizo
3. Tuwekeze sana kuimarisha kamand Iya Wanamaji hasa katika Maziwa ya Tanganyika, Victoria na Nyasa bila kusahau Bahari ya Hindi. Vifaa vya Kisasa kabisa vinavoendana na teknolojia mpya vinunuliwe na kuwekwa maeneo hayo. Kambi za kisasa za kijeshi zifunguliwe maeneo hayo.
Tujifunze sasa kutokana na aibu tuliyopata Congo baada ya Jeshi letu kushindwa vibaya na vikosi vya Rwanda na M23.
Mwisho ni ushauri wangu kuwa;
1. Jeshi likatae kuingiliwa na Wanasiasa na lijiweke kando na Siasa.
2. TISS ifumuliwe na kuunda upya. Baada ya Mchakato wa Katiba Mpya utakaowaondoa Wanasiasa kwenye ku control Watendaji na Mifumo ya Utendaji.
View attachment 3270062View attachment 3270063