JWTZ liwe na kitengo cha elimu kwa raia, kuna upotoshaji mkubwa kulihusu

Unatengeneza disconnection kubwa kati ya wananchi na jeshi lao hii ni hasara kubwa katika vita.

Wananchi watakuwa wanaliogopa jeshi lao na kulichukulia limekaa kishari shari tu na halina upendo juu yao.

Huwezi nipiga mitama mimi uraiani halafu siku mpigane na maadui nikuunge mkono sahau kuhusu hilo.
 
ukizingua unapigwa na huna pakwenda kusema
Haipaswi kuwa hivyo.

Majeshi ya hivi ni ya walevi, waliofeli na wasiojitambua hata kidogo.

In short akili zao ni punje hawana wanacho jua, hata fikra zao hafifu wanacho fahamu ni kupiga tu wananchi.

Si ajabu CCM kuwatumia katika chaguzi kupiga wapinzani na Wazanzibari ili CCM iendelee kukaa madarakani hawafahamu kuwa ni hasara hata kwako.

Stupid
 
maana ya neno ulinzi sio kuua,wala wanajeshi hawafundishwi kuua usiwe kama kasuku unabeba kauli jumla jumla.
Ulinzi wa jeshi katika nchi yake ni uwepo wake kwanza,kuua hayo sio malengo ya jeshi,hujiulizi kwanini kabla ya vita kuna hatua nyingi tu zinatakiwa zipitiwe kabla ya kufika huko??kwa sababu hiyo ni hatua ya mwisho kabisa kunyanyua silaha na kuua mtu mwingine.
Isijekuwa hata mnavyosikia jeshi linalinda katiba mnadhani limekaa na hicho kitabu pale ngome mtu asiibebe.
Au linasubiri mtu aivunje tu limuue kama mbu,NO.

Mtazamo huo wa abiria na wananchi wengi hauko sahihi,elimu ya zaidi inahitajika kabisa,
Konda wa daladala anayeona gwaride la askari wa navy ktk TV anasema ni traffic police hawezi kuwa na uelewa wa jambo kama hili sawa sawa.
 
Mtu mwenyewe unaitwa Restless Hustler halafu unajipendekeza kupita maeneo ya jeshi, ulitegemea wakuache? Jeshini siyo soko la Tandale au Station ya Mwendokasi ambapo hata wazembe utawakuta. Lile ni eneo la wakakamavu tu
Nchi zinazo jitambua zina alika mpaka watoto na watu wazima wasio wanajeshi kuona ufahari wa jeshi lao na jinsi walivyo jizatiti kulinda nchi yao.

Wananchi wao na watoto huwa wana furahi sana na wanatamani wakiwa wakubwa wawe wanajeshi kama hao makamanda wanaowapigisha misele katika Kambi zao.

Sisi huku kwetu jeshi linaogopeka kama ukoma sijui kwa sababu tupo outdated ndio maana tuna ogopa kuwa exposed.
 
Hakuna uongo hapo hata kidogo.

Jeshi ndio nchi.
Ukitaka maelezo tofauti na hayo ndio unataka upotoshaji wènyewe.
Hata huko Ulaya au mbinguni kazi za jeshi na hizohizo tuu.
Hivi unajua kuna nchi hazina jeshi kabisa???
Jeshi sio nchi,nawewe ni muumini wa zile story za rais akitoka nchini anamwachia nchi CDF!!!!
 
Wanachoniudhi hao jamaa ni kuonea raia kwa mambo madogomadogo lakini wakienda Congo huko wanatolewa kamasi na M23.
Mtu anayedhani ukiwa mwanajeshi basi ni kunyoosha silaha na kuua,aulize askari wanaokwenda mission😁😁.atajifunza jambo jipya.

Kule ukienda ukarudi ndio unajua kumbe kazi ya jeshi sio kuua kabisa.
 
Mkuu hiyo ni siasa tuu.
Uhalisia ni kuwa dola ndio nchi
Hii ni siasa kabisa.

Wananchi wao ndio wanauwezo pekee wa kuamua nchi yao iendeshwe vipi ? Iwe wapi au ilindwe vipi ?

Kitu chochote kile wananchi wasipo kubaliana nacho hata kama jeshi likipinga halina uwezo wa kuzuia.

Majeshi yenyewe hata robo za population huwa hayafiki una utani na population ya wananchi.

Serikali nyingi tu duniani zimeangushwa pamoja na majeshi yake.

Ufaransa, China hii ni mifano ya haraka zaidi tena hao wachina ndio wananchi waliitandika serikali na jeshi lake na kuunda serikali yao hii unayo iona sasa hivi.

Jeshi sio chochote mbele ya wananchi, wananchi wao ndio wamebeba roho ya nchi siku wakivurugwa hata jeshi halitaweza zuia mafuriko ya wananchi.

Ni muhimu jeshi kuheshimu wananchi tena kuwaheshimu sana siku wakicharuka watazikimbia hizo kambi nakuambia.
 
Mtu kwa ujinga wake tu anaweza karopoka kwamba jeshi ndio kila kitu,jeshi,serikali,mahakama,polisi,bunge si kitu si lolote kama wananchi hawajawa radhi na kuvibariki hivyo.

Wakati jeshi linaingia barabarani misri kuua waandamanaji,wakakutana na jambo la kutisha kabisa,wananchi wako tayari kuuawa na jeshi lao,jeshi likakumbuka jukumu lake la msingi sio kuua wananchi ni kuwalinda,hawaitaki serikali basi nao inabidi waungane na wananchi tu.

Huko haiti polisi aliyefukuzwa amefunga mitaa ndiye CIC,CDF, na kila kitu,sababu wananchi wamemruhusu awe😁😁,hakuna jeshi wala polisi wanaopambana na jamaa wote wametawanyika.
 
Mwanaume mwingine wa makamo akasema hapo huwezi kutofautisha kati ya mwanaume na mwanamke, cha ajabu mimi nilikuwa naona tofauti hiyo tena niliona mabinti wengi tu warembo sana katik hao wanajeshi.
Teh teh 😃 kazi kweli kweli
 
Acha kutetea upuuzi mjinga wewe.

Wanapopiga na kuua watu wakati wa uchaguzi huwa wamekosewa nini ?

Hawa wajinga kwa misifa yao ya kipuuzi huwa wanapiga abiria, askari wa usalama barabarani, makondakta, madereva vile wajisikiavyo sijui hii ni nidhamu ya wapi ?
 
Haya mambo huwa kama volcano tu siku ya kiripuka unabaki kushangaa ndio hawa wabongo
kuna trend ya wabongo wengi ni ma keyboard warrior, ujasiri online ila kwenye field hawatokei. Na wanao tokea hawaungwi mkono wanapigwa vita.
Siku mkiwa wamoja ndio siku mtaweza pata matoke until then labda kizazi kijacho
 
Chakuongezea.wananchi wanapenda jeshi lichukue Nchi.
Hawa wapuuzi hawapaswi kuongoza nchi maana hata wao hawajitambui watu wanaotumiwa na CCM hama kondomu wakati wa uchaguzi kuiba kura na kulinda tena hawa wa JKT na mwisho kutemwa hawajitambui hata kidogo
 
Sijui una elimu gani kwanza ndugu? Kama ni kusoma na kuandika hili siyo jukwaa lako
 
kuna trend ya wabongo wengi ni ma keyboard warrior, ujasiri online ila kwenye field hawatokei. Na wanao tokea hawaungwi mkono wanapigwa vita.
Siku mkiwa wamoja ndio siku mtaweza pata matoke until then labda kizazi kijacho
Wape silaha hao wabongo ndio upime ujasiri wao wa kunyukana na jeshi lenu la CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…