Hapana JWTZ isiingie mashariki ya Kongo, wajikite tu kulinda mipaka yetu kwa nguvu kubwa. Viongozi wetu wasiongee chochote kuhusu huo mzozo wa DRC. Tuwe neutral kama Switzerland, ikiwezekana hata kwenye mazungumzo ya amani sijui nini tusijihusishe au tuwe washiriki tu but no comment. Tuhakikishe tu nchi yetu ni salama alafu fokasi yetu iwe kuajiri walimu mahiri kwenye mashule yetu ili kutengeneza kizazi cha wataalamu baadae.
Elimu ndio itatutoa kwa habari ya maendeleo ya kiuchumi, kiteknolojia, kijamii hata kisiasa. Si mmeuona mtaala mpya, hiyo ni step ya kwanza, angalia syllabus ya computer science kuanzia form one mpaka six, imagine tukiajiri walimu mahiri wakafundisha kwa umahiri na kujitoa kabisa, kuwe na exhibitions na maonyesho ya wanafunzi na mashindano baina ya shule na shule. Shule za private zitasaidia sana kwenye hili, hasa hasa hizi shule kali kali hapa Dar es Salaam na sehemu mbalimbali hapa nchini. Shule za private zikipata walimu wazuri ziwalinde, ziache kuwaondoa kwa upumbavu, ujeuri na ujinga hatuna mda wa kupoteza we have a generation to build.
Wahitimu wetu wa BSc Computer Science, IT, IT systems, ICT with business, na wale wa BSc with Education kwenye hayo mambo ya IT wakafundishe wasione soo hamna kuwaza mshahara wa ualimu mdogo ela kitu gani tujenge kizazi kijacho imara. Mbali na kufundisha wapoteze mda wao mwingi Github, Stack Overflow wakazane sana kusoma the Bootstrap documentation, Oracle documentation na kujifunza modern frameworks kama vile angular javascript n.k
Najua wengine watasema hatuhitaji walimu tunahitaji wajasiriamali, ooh! sijui jiajiri jiajiri jiajiri. Hapana walimu ni muhimu sana sana sana kuliko wajasiriamali. Ikiwezakana watu wenye uwezo wagawe au wauze maduka yao wakafundishe. Ualimu, ualimu ualimu. Ikiwezekana kila mtu atake kuwa mwalimu siyo kwasababu inalipa bali kwasababu itaikomboa Tanzania yetu kwenye ishu za maendeleo kiuchumi, kijamaa n.k
Wazee waache kuwafanyia vijana mauzauza yaani mtu ukipiga stori za kisiasa siku moja ukamkosoa kiongozi wa kisiasa siku moja basi unafuatiliiiiwaaaa mauzauza mauzauza mauzauza, ina maana haturuhusiwi tena kuzungumza habari za nchi yetu.
Ndivyo hivyo aisee kwenda Rwanda sijui Kongo hakutusaidii chochote, hata kama Rwanda anataka Kongo iwe koloni lake muacheni si inatuhusu nini bana. Kitakachotusaidia ni kuwekeza kwenye elimu.
Sijawahi mtukana rais naweza taja jina langu. mm ni mwalimu Robert Mdee namba zangu ni
0685967259 - airtel
0655980538 - tigo
Moja wapo ya kazi zangu ni hii hapa
Mdee Academy nisaidie tafadhali kupromote kazi yangu, kwa bahati mbaya vijana wetu wako bize kumuangalia Kagame badala ya kuangalia vitu vya maana. Kagame Kagame, Kagame bongo mm mwenyewe ni mrefu na mwembamba vilevile.