Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Kuna kipindi Humphrey Polepole akiwa katibu mwenezi wa CCM alisema Tanzania ina mitambo ya kuiona Congo DRC pale.Huu ndio ukweli wenyewe, na msema kweli ni mpenzi wa Mungu..mkuu kongole kwa kuuweka ukweli peupe kbs! Tumebaki tunajimwambafai kwa historia zilizopita lkn kiuhalisia, siasa ya sasa ime compromise our military ability and intelligence
Lakini najiuliza iweje vikosi vinodaiwa ni vya Rwanda viingie Goma upande wa mashariki na sasa Goma ipo chini ya M23. Ilipaswa JWTZ kuona hata ile kunyatia tu kusogelea eneo la mpaka.
Na ikiwa itawekwa Buffer Zone pale haitakuwa rahisi kufanya lolote ndani ya Congo DRC upande wa Mashariki.
Jamaa wana "Jamming System" na DS ya "Iron Dome".
Mfumo ulokamilika wenye kompyuta, radar na mitambo minne ya kurusha makombora wagharimu dola 100 milioni.
Rwanda wamefanikiwa vipi kuwa na mitambo hiyo, na je ni hiyi tu au kuna mitambo ingine kama Arrow na David Sling, je majasusi wetu wa MI wamefanikiwa kitambua kinoendelea kwa majirani zetu?