Hili jambo la Congo linanifikirisha sana tena kwenye mambo matatu!
a) Limepamba moto sana tukiwa tunaandaa mkutano wa Nishati hapa DSM,mpaka siku ya kufanyika kwa mkutano tarehe 27-28 waasi walikuwa wameshafika Goma. Sisi tuko busy na mkutano wa Wakuu wa nchi wa Afrika,Rwanda na M23 wako wanaitaabisha DRC.
Swali langu, kwanini iwe nyakati hizo?
b) Kabla ya mkutano wa Nishati kufanyika hapa DSM,kuna ugonjwa unaosemekana ni 'Marburg' umezuka eneo la Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera,umeua watu,ila inasemakana huu ugonjwa umetokea Rwanda.
Nchi ikawa busy kufuatilia huu ugonjwa,viongozi wengi wa ndani mpaka 'WHO'nao wako huko mpaka leo hii.
Swali langu,je, ni kweli umetokea Rwanda? Je, huko Rwanda huu ugonjwa upo? Na je, kama siyo 'Marburg' ni kirusi gani,na kwanini kitokee Rwanda,kwanini kitokee sasa hivi wakati Rwanda wako 'busy' kuitwaa Goma,wakati sisi tuko 'busy' na mikutano ya chama (CCM),CHADEMA,na NISHATI?
c) Watu wakijaribu kuhoji kwanini Rwanda anaisumbua Congo, kwanini Tanzania isiingilie kati kuwakomboa Wakongo, kwanini JWTZ isiwarudishe nyuma M23?
Angalia majibu kutoka kwa wachangiaji.
1.M23 ni jeshi imara sana Tanzania msiende mtakufa.
2.Kagame ni mzoefu wa vita Tanzania hamumuwezi.
3.Kagame ana Intelijensia kali ,ana silaha kali sana,ana drone ataiteketeza Tanzania na JWTZ.
4.Kwani tukipigwa na kufa lakini tumeikomboa Congo kwa faida kuna shida gani,mnatuonea huruma ya nini? Kwanini ikitajwa Tanzania na JWTZ kwenye mgogoro wa Congo watu mnatahayari? Hivi,Kinyago tulichokichonga wenyewe kinaweza kututisha kweli!?
Swali langu,tunauliza kwanini JWTZ isiwafurushe M23,wanaojiita Watanzania ndivyo wanajibu hivyo, tena wengine hawajui hata Kiswahili vizuri lakini eti nao wanajifanya ni Watanzania.
Kama Rwanda hahusiki, mbona likija jambo la M23 kupigwa anahusishwa Kagame? Kwahiyo Kagame siyo Mnyarwanda ila ni Kiongozi wa M23?
Mtoa hoja nakuunga mkono.Ila naongezea tena tuwe na mipango ya muda mrefu,Burundi awe sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama alivyo Zanzibar, halafu tuwe na 'access' ya kuingia Congo pasipokuwa na kuzuizi chochote.
Ahsante.