GE2025 JWTZ: Tunafuatilia kwa ukaribu hali ya ulinzi na usalama kuelekea Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tamko rasmi likieleza kuwa linaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya Ulinzi na Usalama nchini katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 na 29 Oktoba 2025, kama ilivyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa (INEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Katika taarifa iliyotolewa Tarehe 15 Oktoba 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Bernard Masala Mlunga, Jeshi limeeleza kuwa kwa ujumla linaridhishwa na hali ya usalama nchini, ambapo kampeni za uchaguzi zinaendelea kwa amani na kwa kuzingatia sheria, maadili ya kisiasa, kuheshimiana na kuvumiliana miongoni mwa wagombea na wafuasi wao.

JWTZ limevitaka vyama vyote vya siasa, wagombea pamoja na wafuasi wao kuendeleza mazingira ya utulivu, ili taifa liendelee kuwa na uchaguzi huru, wa haki na wa amani. Pia, Jeshi limepongeza juhudi za Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa kusimamia vizuri hali ya usalama katika kipindi hiki muhimu kwa taifa.

Aidha, Jeshi limewapongeza wananchi kwa kutumia haki yao ya msingi ya kisiasa kwa kushiriki katika mikutano ya kampeni, kusikiliza sera za vyama na kujitayarisha kufanya maamuzi sahihi ya kuwachagua viongozi wa kuwaongoza.

Hata hivyo, JWTZ limeeleza kusikitishwa na ongezeko la taarifa potofu zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati, kutoka ndani na nje ya nchi, wakilenga kulihusisha Jeshi na masuala ya kisiasa kwa nia ya kuchafua taswira yake na kupunguza imani ya wananchi kwa chombo hicho cha ulinzi.

Jeshi limewahimiza wananchi kupuuza taarifa hizo za upotoshaji na kuendelea kuwa watulivu. Limeeleza kuwa taarifa zote rasmi kuhusu Jeshi zitakuwa zikitolewa kupitia Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ.
​
===

1760612872323.png

1760612882568.png
 
Chanzo: CrownTv
Tarifa rasmi iko wapi isije kuwa yale yale ya barua gushi!
 
Mbona Jeshi hawasemi kuhusu watu wanaopotea? Wao mbona Kama wako upande wa utawala? Hivi hawaoni Hali tunayopitia Kama watanzania Kwa Sasa? Nachukia wapindisha haki, hovyo kabisa nonsense
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tamko rasmi likieleza kuwa linaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya Ulinzi na Usalama nchini katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 na 29 Oktoba 2025, kama ilivyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa (INEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Katika taarifa iliyotolewa Tarehe 15 Oktoba 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Bernard Masala Mlunga, Jeshi limeeleza kuwa kwa ujumla linaridhishwa na hali ya usalama nchini, ambapo kampeni za uchaguzi zinaendelea kwa amani na kwa kuzingatia sheria, maadili ya kisiasa, kuheshimiana na kuvumiliana miongoni mwa wagombea na wafuasi wao.

JWTZ limevitaka vyama vyote vya siasa, wagombea pamoja na wafuasi wao kuendeleza mazingira ya utulivu, ili taifa liendelee kuwa na uchaguzi huru, wa haki na wa amani. Pia, Jeshi limepongeza juhudi za Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa kusimamia vizuri hali ya usalama katika kipindi hiki muhimu kwa taifa.

Aidha, Jeshi limewapongeza wananchi kwa kutumia haki yao ya msingi ya kisiasa kwa kushiriki katika mikutano ya kampeni, kusikiliza sera za vyama na kujitayarisha kufanya maamuzi sahihi ya kuwachagua viongozi wa kuwaongoza.

Hata hivyo, JWTZ limeeleza kusikitishwa na ongezeko la taarifa potofu zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati, kutoka ndani na nje ya nchi, wakilenga kulihusisha Jeshi na masuala ya kisiasa kwa nia ya kuchafua taswira yake na kupunguza imani ya wananchi kwa chombo hicho cha ulinzi.

Jeshi limewahimiza wananchi kupuuza taarifa hizo za upotoshaji na kuendelea kuwa watulivu. Limeeleza kuwa taarifa zote rasmi kuhusu Jeshi zitakuwa zikitolewa kupitia Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ.
Chanzo: CrownTv
Rudini kwa mwalimu wenu wa kugushi, hamjafuzu!
 
Kama litakuwa kweli obviously litakua tamko la mkunda na wachache waliojaziwa madafu kwa akaunti zao. Tamko la wanajeshi kila afisa na askari analo moyoni mwake! Sio kwa kikaratasi na clip ya hivi...

Jipu lishaiva hili wandugu, lisipopasuliwa litapasuka lenyewe tu muda tayari!
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tamko rasmi likieleza kuwa linaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya Ulinzi na Usalama nchini katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 na 29 Oktoba 2025, kama ilivyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa (INEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Katika taarifa iliyotolewa Tarehe 15 Oktoba 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Bernard Masala Mlunga, Jeshi limeeleza kuwa kwa ujumla linaridhishwa na hali ya usalama nchini, ambapo kampeni za uchaguzi zinaendelea kwa amani na kwa kuzingatia sheria, maadili ya kisiasa, kuheshimiana na kuvumiliana miongoni mwa wagombea na wafuasi wao.

JWTZ limevitaka vyama vyote vya siasa, wagombea pamoja na wafuasi wao kuendeleza mazingira ya utulivu, ili taifa liendelee kuwa na uchaguzi huru, wa haki na wa amani. Pia, Jeshi limepongeza juhudi za Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa kusimamia vizuri hali ya usalama katika kipindi hiki muhimu kwa taifa.

Aidha, Jeshi limewapongeza wananchi kwa kutumia haki yao ya msingi ya kisiasa kwa kushiriki katika mikutano ya kampeni, kusikiliza sera za vyama na kujitayarisha kufanya maamuzi sahihi ya kuwachagua viongozi wa kuwaongoza.

Hata hivyo, JWTZ limeeleza kusikitishwa na ongezeko la taarifa potofu zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati, kutoka ndani na nje ya nchi, wakilenga kulihusisha Jeshi na masuala ya kisiasa kwa nia ya kuchafua taswira yake na kupunguza imani ya wananchi kwa chombo hicho cha ulinzi.

Jeshi limewahimiza wananchi kupuuza taarifa hizo za upotoshaji na kuendelea kuwa watulivu. Limeeleza kuwa taarifa zote rasmi kuhusu Jeshi zitakuwa zikitolewa kupitia Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ.
1760614100440.jpg
 
Back
Top Bottom