JWTZ: Wasioitakia mema nchi yetu wanahamasisha kufanya vurugu, hatutasita kuchukua hatua

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wananchi kupuuza wito wowote unaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaohusika na vitendo hivyo.

Katika taarifa yake kwa umma, JWTZ imesema kuwa ina jukumu la kulinda usalama wa nchi na wananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Taifa Sura ya 192.

Jeshi hilo limeeleza kuwa litaendelea kushirikiana na vyombo vya dola kukabiliana na matukio yoyote ya vurugu, ghasia na uvunjifu wa amani.

Aidha, wananchi wamehimizwa kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiji, mitaa na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu viashiria vya uchochezi ili kudumisha utulivu nchini.

JWTZ pia limewahakikishia wananchi kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda mipaka, Katiba na mamlaka ya nchi sambamba na kushirikiana na wananchi katika kuimarisha amani, umoja na maendeleo ya taifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Sylvester Mangure.

sijaelewa, wanaposema "hatutawlinda" wanamaanisha nini? kwamba hawatowalinda against who? je, ni hawatawalinda against the regime, au? hiyo lugha peke yake inaonyesha kabisa kwamba muelekeo ni mzuri hata kama siyo 7/7 lkn siajabu maandamano yatakayofwatila lugha itakuwa nyingine kwani jeshi sijawahi kusikia wakitumia lugha kama hiyo kwamba "hatutawalinda" ina maana kuna adui yetu na wanamjua hivyo ni swala la muda tu watakuwa upande wetu ...
 
sijaelewa wanaposema "hatutawlinda" wanamaanisha nini? kwamba hawatowalinda against who? je, ni hawatawalinda against the regime? hiyo lugha peke yake inaonyesha kabisa kwamba muelekeo ni mzuri hata kama siyo 7/7 lkn siajabu maandamano yatakayofwatila lugha itakuwa nyingine kwani jeshi sijawahi kusikia wakitumia lugha khiyo kwamba "hatutawalinda" ina maana kuna adui yetu na wanamjua hivyo ni swala la muda tu watakuwa apande wetu ...
"hatutawalinda" Aisee, very straight.
 
eshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wananchi kupuuza wito wowote unaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaohusika na vitendo hivyo.

Katika taarifa yake kwa umma, JWTZ imesema kuwa ina jukumu la kulinda usalama wa nchi na wananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Taifa Sura ya 192.

Jeshi hilo limeeleza kuwa litaendelea kushirikiana na vyombo vya dola kukabiliana na matukio yoyote ya vurugu, ghasia na uvunjifu wa amani.

Aidha, wananchi wamehimizwa kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiji, mitaa na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu viashiria vya uchochezi ili kudumisha utulivu nchini.

JWTZ pia limewahakikishia wananchi kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda mipaka, Katiba na mamlaka ya nchi sambamba na kushirikiana na wananchi katika kuimarisha amani, umoja na maendeleo ya taifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Sylvester Mangure.
Wangekuwa wanalinda usalama wa wananchi na nchi 29/10 raia wasio na hatia wangewindwa kama wanyama? Vijana wanaotekwa kila siku na wengine kupotezwa mbona hawajitokezi kuwalinda?
 
eshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wananchi kupuuza wito wowote unaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaohusika na vitendo hivyo.

Katika taarifa yake kwa umma, JWTZ imesema kuwa ina jukumu la kulinda usalama wa nchi na wananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Taifa Sura ya 192.

Jeshi hilo limeeleza kuwa litaendelea kushirikiana na vyombo vya dola kukabiliana na matukio yoyote ya vurugu, ghasia na uvunjifu wa amani.

Aidha, wananchi wamehimizwa kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiji, mitaa na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu viashiria vya uchochezi ili kudumisha utulivu nchini.

JWTZ pia limewahakikishia wananchi kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda mipaka, Katiba na mamlaka ya nchi sambamba na kushirikiana na wananchi katika kuimarisha amani, umoja na maendeleo ya taifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Sylvester Mangure.
JWTZ hawana nguvu tena zama hizi nakumbuka mwaka jana Kuna baazi ya wanajeshi waliteswa sana na police wasiokuwa na mafunzo
 
Back
Top Bottom